Tetesi: Walimu wamegeuza Shule za Serikali kuwa Vitega Uchumi vyao

Huwa kuna vikao vya kujadili maendeleo ya wanafunzi huwa unaenda mkuu maana sio kulalamika. Mnataka watoto wafaulu sasa kuna extra hours walimu wanatoa mitihan hizo hela zinatumika kununulia maji ya kunywa wakisahisha au kufundisha masaa ya ziada mm naona ungefocus kuangalia maendeleo ya mwanao zaidi ya kulalamikia hzo hela
 
Kipato Chao hakikidhi mahitajii na muda wakufanyaa mambo mengine njee ya shulee pia imekuwa ngumu kwao ,hvyo wameonaa Bora wale huko huko wanakofundisha...
Wafunge masoma saa 8 mchana, waombe ruhusa rasmi ya tuition, baadala ya kujichosha na vimia mbili mbili vya wanafunzi, na kukaa na watoto hadi saa 12:30 jioni muda ambao ndio wa kufanya shughuli zao.
 
"wateja wetu ni wanafunzi" kauli ambayo walimu wengi wanaitoaa ikidhihirisha kutotosheleza kwa mishahara yao.. hapo suluhisho sio sheria ni fungu tu
 
Ni kweli, lakini je Serikali kuu inalijua hilo? Maana mambo hufanyika chini chini, kitu ambacho sijui kama ngazi za juu wanajua, mfano mzuri vile vitabu vilivyo katazwa kutumika na Serikali, inamaana ndio haya ya tamaa za walimu kuhamasishwa watu kutumika vitabu bila kufuata utaratibu wa Wizara husika
 
Kila mtu kazi uomba yeye mwenyewe, ukiona unakwazika una achia ngazi unahamia Airtel
Ni sahihi Mkuu, ila kuwapa motisha Walimu ni jambo lenye Tija sana.

Tuliosoma miaka ya zamani, ilikuwa kawaida Wanafunzi kwenda kulima kwenye shamba la Mwalimu, kwa kufanya hivi ilikuwa Wanafunzi wanajifunza Kilimo na kujitegemea pamoja na motisha kwa Walimu
 
Ukiona elimu ni ghali jaribu ujinga!! Hivi Huwa mnalipa sh ngapi!?? Mbona milio mingi!?
 
Asante kwa kuwasilisha uhalisia uliopo na ni kweli hali ndivyo ilivyo sasa fanya hivi;
Ishinikize serikali iboreshe maslah ya waalimu uone kama hayo ulioandika yataendelea kufanyika
 
Hivi Huwa mnalipa sh ngapi jamani!?? Mbona milio mingi!?tafuteni pesa nyie watu!! Dahh Yani inalipa sh 10,000 Kwa mwezi unalialia!??
Sasa bia utakunywa kweli!?
 
Ni kweli kaka, ujira ni mdogo, lakini hatuwezi kuruhusu walimu wawekeze kwenye michango,tutaumiza watu, na ajira hizi ni hiari kwa hiyo umeridhia kufanya kazi ya ualimu ridhika na mshahara wako
 
Wewe unataka mtoto afaulu au serekali kuu ijue? Achana na wanasiasa ndugu hao hawasomeshi huko watoto wao.

Unakumbuka suala la Makambi ya shule Mkuu wa mkoa Mtaka alijibu nini? Alijua umuhimu wa kutenda sio kusikiliza wanasiasa.

Hebu tenga siku moja kashinde shule na hao walimu unaowalalamikia then utupe mrejesho kama unaibiwa Hizo 200 unazotoa.
 
Kila mtu kazi uomba yeye mwenyewe, ukiona unakwazika una achia ngazi unahamia Airtel
Walimu wenyewe wanatamani watoke mapema wakafanye mambo yao, Ila wanakaa shule mpaka jioni kuwasaidia watoto wenu.

Nenda kwenye kikao cha shule mkubaliane wazazi hamtaki remedials/vipindi vya ziada uone walimu watakavyoshangilia..
 
Hivi Huwa mnalipa sh ngapi jamani!?? Mbona milio mingi!?tafuteni pesa nyie watu!! Dahh Yani inalipa sh 10,000 Kwa mwezi unalialia!??
Sasa bia utakunywa kweli!?
Ndugu kama una pesa Jenga shule yako, somesha watoto wako na ajiri Waalimu wako uwalipe vizuri, si una pesa sana, fanya hivyo, sisi hatuna uwezo huo. Ukifuatilia sana ninyi kazi zenu za ziada ni rushwa na upigaji.
 
umaskini wako unakutesa
 
Tanzania siasa ndo inasababisha watu kutowajibika.
Unazaa mtoto afu unataka usomeshewe bure
nashangaa mwambie wkt wa kut o m b a n a alifurahia hakukumbuka kuna malipo ya mtoto unataka aende shule bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…