Wamisionari waliofika Tanganyika walikuta watu wamestaarabika na wanajua kusoma na kuandika

Wamisionari waliofika Tanganyika walikuta watu wamestaarabika na wanajua kusoma na kuandika

Sho...
Kijerumani kilifundishwa shule wakati wa utawala wa Wajerumani.
Unasema madrasa kulikuwa kinafundishwa kuwa hisabati, kiswahili,kiarabu na kijerumani kabla wakoloni wa kizungu kuja ikiwemo hao wamisionari akina Krapf Sasa hivi Mbona madrasa hawafundishi hayo masomo ni kiarabu tu?
 
Kwa uongo hujambo umeeleza kuwa waislamu ndio Walikuwa wa kwanza kuelimika wakijua kusoma na kuandika Kwa herufi za kiarabu
Halafu eti walimu wa kwanza wa shule za misionari Walikuwa waislamu waliosoma madarasa.Sijawahi ona shule yeyote Wala kusikia ya Kanisa iliyowahi fundisha kiarabu darasani Cha kusoma Wala kuandika Wala kuongea
Pili kama elimu yenu Iko juu Mbona Sasa hivi madrasa Bado zipo mnaendelea nazo hiyo elimu ya juu ya madrasa ilipotelea wapi Serikali mtasingizia kuwa ilikuja misikitini kubadilisha syllabus au?
Sho...
Ungesoma paper ya Ishumi ungeongeza maarifa yako katika hili.

Haya mambo yanahitaji utulivu wa akili na kusoma.

Tofauti kati yetu ni kuwa mimi nimetafiti historia ya Tanganyika na nimeandika vitabu na vinasomwq kwingi.

Wewe unajiandikia tu kama akili yako inavyokutuma.

Katika walimu wa kwanza kufundisha shule za Wajerumani walikuwa Alfred Omari na Charles Suleiman ambao walibatizwa na kusoma shule ya Wajerumani.

Alfred Omari ni baba yake Dunstan Omari Mwafrika wa kwanza kuwa District Officer 1955 na District Commissioner 1958.

Haya nimeeleza katika kitabu cha Abdul Sykes.
 
Unasema madrasa kulikuwa kinafundishwa kuwa hisabati, kiswahili,kiarabu na kijerumani kabla wakoloni wa kizungu kuja ikiwemo hao wamisionari akina Krapf Sasa hivi Mbona madrasa hawafundishi hayo masomo ni kiarabu tu?
Sho...
Hawafundishi kwa kuwa hayo masomo yalihamia shuleni na madrasa zikabakia kusomesha dini.
 
Sho...
Hawafundishi kwa kuwa hayo masomo yalihamia shuleni na madrasa zikabakia kusomesha dini.
Madrasa zilikuwa na syllabus zake ikiwemo kusoma hisabati,kiswahili , kijerumani na kiarabu

Nani aliyehamisha Wakati madrasa ni independent Sio sehemu ya serikali.Nani aliyetoa maamuzi hayo huko misikitini kuwa yasiendelee kufundishwa madrasa?
 
Sho...
Hawafundishi kwa kuwa hayo masomo yalihamia shuleni na madrasa zikabakia kusomesha dini.
Huu ni Uongo uliokubuu😂 Katika nchi zote za Kiislam Madrasa ni kwa ajili ya kufundisha Quran na Kiarabu. Katika tembea yangu kiasi Duniani hapa sijaona Madrasa inafundisha zaidi ya hivi viti viwili. Madrasa zilianzishwa miaka kadhaa baada ya Kuanzishwa Dini ya Kiislam. Muhamad akusoma Madrasa. Asili ya Kufundisha Watoto ilianzia Misri enzi za Falao na ata ukisoma maandiko .Musa alisoma katk shule za Misri,,Elimu ambayo ilimwezesha kufanya vikao na majadiliano na Farao mpaka akawapa rukhusa Waisrael watoke Misri, Pia Elimu hiyo hiyo Ilimsaidia Musa Kuwaongoza Kuhukumu na kuwatawala wana Israel Jangwani wakiwa wanaelekea Jerusalem kwenye nchi yao. (Hapa unaona kuwa Musa alikuwa na Elimu zaidi ya moja ikiwemo Sheria, Uongozi etc)Israel waliendeleza utamaduni wa Kusomesha watoto wao.... na ata Yesu Aliweza Soma katika shule hizo na Yeye kujua kusoma na Kuandika pamoja na mambo mengine kama Sheria n.k,,,(Bibilia ina ushaidi wa Yesu kujua kusoma na kuandika na pia kuwa na Elimu tosha ya Dini na pia Siasa- Kitu ambacho kilimwezesha kuhubiri na kufanya kazi zake Kisomi na umakini wa hali ya juu) Warabu wakakopy ila wao ikiwa ni mafundisho ya kitabu kimoja tu... hu ndo ukweli
 
Madrasa zilikuwa na syllabus zake ikiwemo kusoma hisabati,kiswahili , kijerumani na kiarabu

Nani aliyehamisha Wakati madrasa ni independent Sio sehemu ya serikali.Nani aliyetoa maamuzi hayo huko misikitini kuwa yasiendelee kufundishwa madrasa?
Sho...
Kawaida yangu ni kueleza yale ambayo hayafahamiki si kuingia katika ubishi.
 
Huu ni Uongo uliokubuu😂 Katika nchi zote za Kiislam Madrasa ni kwa ajili ya kufundisha Quran na Kiarabu. Katika tembea yangu kiasi Duniani hapa sijaona Madrasa inafundisha zaidi ya hivi viti viwili. Madrasa zilianzishwa miaka kadhaa baada ya Kuanzishwa Dini ya Kiislam. Muhamad akusoma Madrasa. Asili ya Kufundisha Watoto ilianzia Misri enzi za Falao na ata ukisoma maandiko .Musa alisoma katk shule za Misri,,Elimu ambayo ilimwezesha kufanya vikao na majadiliano na Farao mpaka akawapa rukhusa Waisrael watoke Misri, Pia Elimu hiyo hoyo Ilimsaidia Musa Kuwaongoza Kuhukumu na kuwatawala wana Israel Jangwani wakiwa wanaelekea Jerusalem kwenye nchi yao. (Hapa unaona kuwa Musa alikuwa na Elimu zaidi ya moja ikiwemo Sheria, Uongozi etc)Israel waliendeleza utamaduni wa Kusomesha watoto wao.... na ata Yesu Aliweza Soma katika shule hizo na Yeye kujua kusoma na Kuandika pamoja na mambo mengine kama Sheria n.k,,,(Bibilia ina ushaidi wa Yesu kujua kusoma na kuandika na pia kuwa na Elimu tosha ya Dini na pia Siasa- Kitu ambacho kilimwezesha kuhubiri na kufanya kazi zake Kisomi na umakini wa hali ya juu) Warabu wakakopy ila wao ikiwa ni madundisho ya kitabu kimoja tu... hu ndo ukweli
Chipukizi,
Nimekusoma.
Ni Farao si Falao.
 
Wamishionari na wakoloni wakawa wanatoa elimu kwa ubaguzi.

Hii ndiyo sababu Waislam wakawa mstari wa mbele katika kupambana kwanza na Wajerumani kwa silaha kisha na Waingereza kupitia vyama.

Nimeeleza haya yote katika kitabu cha Abdul Sykes.
Kwa maana hiyo kama wamisionari/ wakoloni wangetoa elimu kwa usawa, waislamu (wa kipindi hicho) wasingejihusisha au kuwa mstari wa mbele katika harakati za uhuru??
 
Kila anayekwenda kuangalia onesho la mwanazingaombwe hujua anachokwenda kuangalia ni mazingara, Lakini huenda...

Chambo hunasa werevu wadadisi na waroho wasio na simile...
 
Kwa maana hiyo kama wamisionari/ wakoloni wangetoa elimu kwa usawa, waislamu (wa kipindi hicho) wasingejihusisha au kuwa mstari wa mbele katika harakati za uhuru??
Chat...
Umejaribu kufanya deduction kupata jibu lakini ulichokosea ni kusahau kulitazama tatizo hili katika uhalisia wake.

Haiwezekani kwa ukoloni kuufanyia haki Uislam.
 
Chat...
Umejaribu kufanya deduction kupata jibu lakini ulichokosea ni kusahau kulitazama tatizo hili katika uhalisia wake.

Haiwezekani kwa ukoloni kuufanyia haki Uislam.
Uislam ni Nini??

Maana inawezekana Unadhani watu Wa pwani ndiyo uislam!!!
 
Allen...
Nifafanulie lile unaloona nakosea katika kumithilisha Uislam na watu wa pwani.
Keshou Mungu akijaalia nitaendeleza huu mjadala. Hivi Uarabu ni uislam au uislam ndiyo uarabu!!!??

Yaani unawezaje kuutenganisha Uarabu na Uislam ama Uislam na uarabu??
 
Mzee Said acha kupotosha hapa JF.
Elimu ya kujua kusoma na kuandika ni elimu ya kikoloni kwa 100%. Hakuna mtanganyika aliyejuwa kusoma na kuandika bila kupewa elimu hiyo na mkoloni. Kama mjerumani alipofika Tanganyika alikuta watu wanajua kusoma na kuandika hiyo inamaanisha kuna mkoloni mwingine alitangulia hapo kabla kuipandikiza. Hakuna kitu kilizuka chenyewe.
 
Elimu rasmi (kujua kusoma na kuandika) na dini za kigeni (Ukristo na Uislamu) ni matunda (matokeo) ya ukoloni kwa 100%. Bila mkoloni hakuna kitu (elimu au dini) kingeota hapa Tanganyika.
 
Ni uongo mkubwa kusema madrasa za dini za kiislamu ndio chimbuko la kuzalisha wasomi wa mwanzo wa Tanganyika. Hii ni kamba nyepesi mnoo.

Embu tujiulize, mbona mpaka leo hii madrasa za kiislamu zipo nchi nzima lakini hakuna wasomi wa kiislamu wanaozalishwa kupitia hizo madrasa? Yaani maamuma (wasiokuwa na elimu, ufahamu mpana au uwezo wa kufaulu vya kutosha) ndio utawakuta wamejazana humo.
 
Back
Top Bottom