Umeongea point nzuri sana. Naomba kuongezea ili iweze kueleweka zaidi.
Unajua kipindi cha wazazi wetu si kwamba wanaume wakorofi hawakuwapo, walikuwapo na hata mimi nimewashuhudia sana. Unakuta mdingi anakuwa mtemi kwa mke mpole na mtii. Majibu makali, kufokea kujibu kwa dharau na hata kufedhehesha ila walivumilia na kuendelea kutii wanaume zao na kutumikia ndoa.
Shida ilikuja baada ya wanajamii walipoona kuwa kuna uonevu unatokea kwa kada ya wanawake na kama wanajamii inabidi kuchukua hatua. Tatizo ni hapo lilipoanza. Wanaharakati wakawabrand wanaume wote kuwa ni wabaya na wananyanyasa wanawake.
Hivyo serikali, taasisi na asasi zikashika huo wimbo na kuubeba kama ulivyo bila kufanya tafiti za maeneo gani ambapo wahanga ni wengi na maeneo gani ambapo hakuna sana matukio ya unyanyasaji wa wanawake.
Hii imekwenda kwa muda mrefu kiasi kwamba sasa imekuwa invested kwenye akili ya kila mwanajamii kuwa wanawake wanaonewa na wanaume na hivyo ni wa kutetewa muda wote. Hii ikashape kila sera, movement na hata harakati ikawa sasa mwanamke ndie mhanga na mwanaume ndie mkorofi.
Leo tunazungumza ni mwaka 2022 kipindi ambacho mbegu ya hizi harakati za miaka ya 1980's mwishoni kuja 1990's yote hadi 2000's kufikia leo vizazi vya watoto wa kiume na wa kike wamehutubiwa, kuklemishwa, kuimbiwa mapambio na nyimbo za kuambiwa mwanamke ni mhanga wa mfumo dume.
Watoto wa kike wamekuzwa wakiaminishwa wanaume ni maadui zao na wao ni wahanga. Hii sasa ndilo zao au matokeo ya zile harakati na ndipo wewe umezungumza kwa kina kuhusu tofauti ya wanaume kizazi hiki na kizazi cha baba zetu.
Kimsingi upo sahihi sana kuhusu watoto wa kiume kuwajibishwa kwa makosa ambayo hawakukosea wao. Leo hii unakutana na binti nyote mkiwa bado wachanga kabisa kimaisha. Unamwambia tupange maisha tuanzie chini anakwambia tukishafanikiwa utanigeuka na kuniacha na kutafuta mwanamke mwingine.
Ukiwa na pesa mwanamke anakuja kwa lengo la kutwa mali na pesa zako kwa gia ya kuwa mkeo kuzaa na wewe watoto ambao malengo yake ni baadae awapandikize chuki wakutenge ufe kwa presha yeye abakie na watoto wamhudumie na mali zako azitawale.
Na ndio maana ukitazama vijana wengi wa kizazi cha 1980 na 1990 (millennials) ndio ambao wanavilio sana kwa wake zao tofauti na wa miaka ya 1970 kurudi nyuma (generation X na babyboomers). Tazama madogo wa miaka ya 2000 (generation Z) ndipo utajua kuwa hii ni effect ya zile harakati.
Watoto wa kike wa kizazi cha miaka ya 1980's hadi 1990's hawawezani na watoto wa kiume wa miaka hiyo sababu wameshakuwa na corrupted mindsets juu ya mahusiano, ndoa na familia in general hakuna wanalojua majority by 90% ni zero when it comes to relationship its like wamekuja kutalii tu hapa duniani na kusubiri kuzeeka na yote ni matokeo ya hizo harakati za kutetea wanawake ambazo zilikuwa propagated kwa namna potofu na ya kuwavuruga watoto hawa wa kike ongezea na western 3rd wave feminism ndio imekuwa Petrol kwenye moto wa gesi.
Mabinti wa miaka 1980's hadi 1990's wanatumika na wanaume wa kizazi cha miaka ya 1970's kurudi nyuma sababu wengi ni watu wazima kwa sasa,na miaka yao uchumi haukuwa mgumu sana so wana rasilimali na uwezo kiuchumi so hutake Advantage ya kuwa nao kimaslahi sababu bado wanaume wa miaka ya 1970's kurudi nyuma wana misingi ya kuhumia mwanamke bila kuhoji.
Mabinti wa miaka ya 1980's hadi 1990's hawapo tayari kujenga maisha na wanaume wa kizazi chao sababu ya hofu walizojazwa na hizi harakati za wanawake and therefore wanaona bora kuishi kijasusi ili kuipata salama wanayoitafuta ambayo hatari yake wameibebelea kwenye hisia na akili kutokana na mapokeo ya story za kutisha za mama zao na bibi zao kinyume na uhalisia.
Ukirudi kwa mabinti kizazi cha 2000s kuja leo hii, ambao kwa sasa ndio washika soko, hawa sasa hawana ramani na hawana cha kujifunza kwa dada zao maana ndio walikuwa wawape kijiti ila sasa wanawapa taarifa ambazo hazishabihiani na ukweli zinawachanganya. Wanaambiwa wanaume ni wanyanyasaji yet wakitazama dada zao majority hawakuwahi kuolewa ila wanawatoto hayo ya ndoa wameyapitia vipi.
Wanasema wanaume sio waowaji ila wakitazama mitandaoni wanastaajabu kuona wanaume ndio wanabembeleza ndoa na wanawake ndio wanaongoza kwa kuikwepa na majukumu yake.
Wanasema wanataka mapenzi ya dhati na ya kweli kusema mapenzi si pesa wala mali bali mapenzi ni kujaliana yet hawapo tayari kuanza chini na wapo tayari kulala na wanaume wa watu wenye ndoa na kuzaa hovyo nao.
Hii inawapa nafasi ya kuona picha halisi ya kuwa kuna tatizo na ndio maana ukitafiti vibinti vilivyozaliwa miaka ya 2000 kuja mbele vina akili ya maisha na ukiwa na direction ya maisha kama mwanaume mnakwenda sawa na vinafuata maagizo vema na utii bila shida ila kama ni mwanaume ambae haujitambui hautawezana nao.
Mwanaume wa miaka 1980 na 1990's anaweza kudate na kuoa binti aliyezaliwa kuanzia 1998,1999,2000, hadi 2004 bila shida na wanaendana bila shida.
Kwa upande wa mabinti waliozaliwa 1980's hadi 1997, wapo kwny red zone na lala salama ya mahusiano ya ndoa. Kuoa au kuolewa haishindikani ila haitakuwa ya ndoa serious bali ile ya kuonesha kuwa na mimi nipo kwenye ndoa.
Mwanamke ana nafasi ya kuscore mahusiano serious ya ndoa katika umri wa kuanzia 16 hadi 25 (prime age) baaaasi (kama kuna ataebisha mimi sitopoteza maneno sababu ukweli upo wazi ni swala la kutazama kwa macho sio kuhisi tunatishana).
Nje ya umri huu wa kuanzia 26 kuendelea mbele hadi uzee jua tu ni lala salama, imeanza ukielekea 30 ambayo ni umri wa toba na kutumikia adhabu. Kuolewa inawezekana ila ndoa ya afya huwa ni changamoto sana kuipata hapo sababu Historia huwa inakuja kumhukumu muhusika na pia mwanaume,kama ni mkubwa, anakuwa tayari ameshapitia misukosuko ya mahusiano na kukataliwa na kuharibu sana so ana ganzi hawezi hisi mapenzi tena. Mwanaume akiwa mdogo then hapo inakuwa ni kuweka punda nyuma ya mkokoteni, atauvutaje, mwanaume ndie kiongozi sasa mwanamke ni mkubwa unaongozaje mtu mwenye experience ya maisha.
Mambo ni mengi sana uelewa ni mdogo. Tunahitaji kujielimisha zaidi.