Wanafunzi Jenipher na Caren wa Iringa girls wanahitaji ushauri wenu,enyi GREAT THINKERS

Acha kumchimba mkwara madam wa watu,tuchimbe mkwara watu kama sisi,we fear nothing rather than fear itself.
 
Hao wadada waache upuuzi, yaan wanawaza bata na uhuru wa chuo, hawana lolote, wabaki hapo shule wapige kitabu. Huo wanaofanya ni ulimbukeni unawasumbua

Nwei kupanga ni kuchagua. Kazi kwao.
Kitu huelewi, pita kimya. Nakupa mfano, mtoto kapata C ya Physics na kama kawaida Biology na Chemistry ana C au zaidi. Huyu kwenda PCB anapoteza muda maana ni ndoto za ndalia kuibuka na A ya Physics form Six ili aweze kuchukua MD. Sana sana akijitahidi atapata C au D au S. Hapo kama amekamia MD lazima arudi kuchukua CMT ambapo aliokuwa nao wakaenda Chuoni, watakuwa mwaka wa tatu wakati yeye akianza mwaka wa kwanza. Ili achukue MD atatumia miaka 5 na kama akikatisha form four atatumia miaka 3 tu. Amina68 nimekupa nondo
 
Acha kupotosha umma, yaani sisi serikali hatuajiri wenye degree? Hizi sasa ndio dalili za ugonjwa wa diploma.
 
Mpaka hapa mada ilipofikia, Amina umeshika fungu lipi kati ya hayo machaguo mawili?
 
Madam unaishi wapi nnashida na wewe sio hao wapuuzi .
 
Mimi kama degree holder na mwalimu ambaye kagwaya ajira, Nina maona yafuatayo.

Kama watoto wamewiwa kwenda chuo naona wako sawa na wana maono mazuri sana. Ila ni vzr na wazazi wakawasikiliza ili kujua wanachotaka kwenda kusoma huko chuo. Make kuna course zingine unaweza kusoma kama kutimiza wajibu tu.

Ila kama wazazi wakikaza nawaomba hao mabinti wakomae tu kwani miaka 2 siyo mingi. Na watakapo hitimu didato cha 6 watakuna vyuo vipo tu. Washarakie maisha
 
Reactions: Cyb
Sayansi sio theory uongo

Mainjinia wa ujenzi mbona wanachora majengo na kujenga? Kusema wamekariri uongo

Mainjinia wa umeme mbona wanafanya mifumo ya umeme kuanzia majumbani,viwandani nk uongo kusema mainjinia wa umeme wanakariri masomo sio kweli


Madaktari na theory wapi na wapi
Operation hazifanani mbona wako vizuri?
Migodi mikubwa nchini wanaoendesha ni watanzania sio wazungu huyo.mtu wako hopeless

Mechanical engineers wa TRC nenda pale vijana wadogo na wako.fit

Nenda wizara ya Maji water Engineers vijana wadogo na wako fit


Hizo theory zenu za makaratasi za kukariri ziko masomo ya Arts sio ya sayansi

Field mtukachukua Civil Engineering halafu hajui chochote nani atampokea? Hayupo

Unajiliwaza kwa vitu hewa
 
Are you serious? Haya mbona ni mambo ya kifamilia na binafsi? Mimi nilipomaliza form four nilikuwa nalilia sana eti nikasomee ufundi wa magari japo nilifaulu na kuchaguliwa kwenda kidato cha tano. Baba yangu akanijia juu sana na sasa namshukuru kwani aliniongoza vizuri. Hao bado ni watoto na wazazi wao wameona wakienda high school ndiyo njia sahihi. Wao bado akili za kitoto zinawasumbua.
 
Acha kupotosha umma, yaani sisi serikali hatuajiri wenye degree? Hizi sasa ndio dalili za ugonjwa wa diploma.
Hakuna bosi mwenye diploma Serikalini

Degree huajiriwa kuwa level ya management

Vi diploma ni vya kutumwa na mabosi wenye digrii. Sema mleta mada anapihia debe Vyuo vya diploma kutafuta wateja ni makerting strategy!!

Lakini kwa wazazi wanaojitambua mtoto huwezi mpeleka diploma uwe akili huna
 
Nipe namba zao kama upo serious kuwatukana watu sio poa mtu akikwama anahitaji ushauri mzuri na ideas na waone watu waliochukua hayo maamuzi wapo wapi nawanafanya upuuzi gani mpaka sasa
 
Haya ni mawazo ya kijima na yanawakilisha mawazo ya vijana wengi wa kibongo wasiojua maana ya elimu. Kusoma theory kunafanya mtu ajue mambo kwa deep zaidi na kuweza kuendeleza pale sayansi ilipoishia. Hebu fikiria kitu kama electronics. Bila kuchimba theory yake na kuelewa mambo kwa undani pasingekuwepo maendeleo kwenye utengengengezaji wa vifaa advanced vinavyoendana na tecknology kama ilivyo sasa. Sasa ndugu zangu ninyi mliozoea elimu ya kukariri na kufanya kwa kukariri ndiyo mnakuja na mawazo fyongo ya kutaka kila mtu afanye kitu kwa kuangalia na kukariri badala ya kuwa na knowledge pana ya kufanya na kuendeleza pale sayansi ilipofikia.
 
Matusi yanini degree nini unaweza ukawa bossy na huna nyumba unapanga unaweza ukawa na madegree na huna maendeleo yeyote unasimamia makampuni ya ya watu mpaka mwisho wa pumzi yako.
Kingine nikuambie kuna utofauti wa kufaulu na kutofaulu ukifaulu fuata process ila kama hujafaulu nenda veta .
 
Wazo lako hili ni zuri, hata hivyo jukwaa uliloleta sio ulilokusudia (great thinkers). Umemhukumu jamaa hapo juu kuwa unachelea kuamini kama yeye ni great thinker, lakini yuko kwenye viwanja vyake vya kujidai.

Anyway, hii ni issue ya academic, social, lakini pia psychology. Kwa hivyo, utatuzi wake ungehusu zaidi walimu wa hapo shuleni na wazazi wakilizungumza jambo hili kwa pamoja.

Lakini kwa ushauri wangu mimi, naona hao mabinti waachwe wakasomee machaguo yao. Yawezekana wameona mbali, labda kulingana na changamoto ya ajira kwa wakati huu.

Wameona wakasome chuo na kutunukiwa diploma, ambapo huko mbele watakuwa na options mbili; kuajiriwa, maana watakuwa na profession, au kuendelea na elimu ya juu.

Wapo wengine, walichagua mkondo huo, baada ya kuhitimu diploma, wakapata kazi, walipofikisha miaka miwili kazini, wakaomba kusoma chuo kikuu, ambapo waliruhusiwa huku wakisomeshwa na kulipwa mishahara yao, maana wanasomea kazi zao. Na walipomaliza, walirudi makazini kwao, huku walipandishwa vyeo na masilahi.

Hivyo, wacheni hao mabinti wakasome wanachotaka, kuliko kuwalazimisha wasichotaka. Inasemekana, mtu hupata mafanikio makubwa kama atafanya kitu anachokipenda, kuliko kumlazimisha kufanya jambo asilopenda. Itakuwa sawa na kumlazimisha ng'ombe asiye na kiu kunywa maji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…