Tulipiga kelele kuhusu Tume yenye Mwenyekiti Mwakyembe kuwa siyo mahali penye integrity ya kutukuka ya kutupatia majibu wakati kunao watu taifa hili linalowaheshimu kutokana na kazi zao. Ni muda muafaka tuwe na namna ya kufanya vetting kama taifa kwenye mambo muhimu kama haya. Wakina Professor Shivji, Chris Peter, majaji wastaafu wakina Robert Makaramba, Professor Ruangisa, akiwemo jaji Mkuu Mstaafu Sumata na wengine wengi other than how ma serial wenyeviti wa Tume zisizo na tija, wangeweza kutusaidia kupata ufumbuzi wa jambo hili maana kwa sisi tusio wana sheria lakini watu wenye akili timamu tunachokiona ni kuwa waliofeli ni wote, wanafunzi wa Law school, walimu wao, na mfumo mzima wa law school ni 'failure' ab initial. Hili ndio tatizo llingine na kukosekana kwa agenda za kitaifa hata kwa waathirika. Wakati wa mwaka jana walipokumbwa na madhili, hawa wa mwaka huu walikaa kimya. Yote ni yote, hii ni kashfa nyingine kubwa kwa taifa, na hasa tasnia muhimu kama hii. Nashingaa hata wanasheria wenyewe ikiwemo TLS wamefunga midomo.