Wanafunzi Law School mnayo nafasi ya kujipigania

Wanafunzi Law School mnayo nafasi ya kujipigania

Mimi siyo mwanasheria, ila kwa ulewa wangu, nafikiri Law School ingalikuwa na viwango tofauti kwa watahiniwa. Mathalani, kama ilivyokuwa kwa CPA, tuseme wanafunzi wanapomaliza shahada zao za kwanza katika vyuo vikuu vinavyotambulika, basi waingie katika daraja fulani, tuseme "entry level B" na hapo itampasa afanye masomo machache tu ya daraja hilo.

Endapo akafaulu katika daraja hili, itampasa afanye mitihani mingine ya daraja la juu zaidi, tuseme "final level A". Hapo nafikiri itakuwa njia rafiki ya kuwatahini watahiniwa, kuliko kuwabebesha zigo la masomo mengi kibao na kumtaka ayafaulu yote kwa mpigo mbele ya watahini ambao ni wanoko kupindukia.

Ni kweli kabisa "professional bodies" zina viwango vyake vya kimataifa ilivyojiwekea ili kuilinda hadhi na maadili kwa watahiniwa. Lakini ni ukweli pia lengo la kuwatahini watahiniwa si kuwafelisha wengi kwa pamoja, na tena kwa kiwango cha kutisha, isipokuwa ni kuchagua "the right teaching methodologies" ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Nakumbuka enzi hizo nikiwa katika elimu yangu ya kuungaunga, alitokea mhadhiri mmoja ambaye alikuwa akifundisha somo la "statistics" na ambalo lilikuwa limejaa kanuni nyingi sana za kimahesabu. Na kama ilivyo kawaida, umahiri wa kukokotoa hesabu una changamoto nyingi sana kwa wanafunzi ambao wana "background" ya "ungwini"

Basi alikuwa na kawaida ya kutunga mitihani migumu sana, na siku ya mtihani wake ilipofika, ni dhahiri alionyesha kupania kichizi ili madenti wafeli kwa wingi. Alipoona wanafunzi wengi wanakodolea tu karatasi za mtihani pasipo kuanza kufanya. Kwa furaha kubwa alitoa kicheko cha kejeli na kubwatuka kwa sauti kubwa sana,
"AT LEAST I HAVE KILLED ONE"
Hapo ndipo utapata picha ya watahini waliokuwa wanoko na "sadists" ambao hawajali chochote kile kuhusu kufeli kwa idadi kubwa ya watahiniwa kwa mpigo.

Wanafunzi hawa wanaofeli LST ni first class material. Hadi hapo unasema je?

Kadhia ya Law School "Wasomi Nguli" wasikilizwe

Unasema je pia kuhusu wasomi nguli hawa?
 
Wewe ni mwanafunzi pale isije kua wewe umeliwa kichwa unakuja kutafuta huruma huku mtandaoni! Ni masomo mangapi unatakiwa kurudia!?
 
Wewe una kitu gani cha kujivunia?
Unadharau watu wakati hujafanya jambo lolote la kutisha katika hii nchi.
Nani asiyefahamu kuwa wahitimu wa sasa wengi wao huwa wanazima moto mitihani yao?
Nani asiyefahamu kuwa wahitimu wachache tu wa siku hizi ndo wako vizuri sana na wengi wametawaliwa na kutaka attention mitandaoni baada ya kusoma?
Kwanza una GPA ya ngapi wewe unayewadharau watu?

Kwamba wewe kumbe unacho cha kujivunia? Mimi nukuu zangu zinatoka huku:

Kadhia ya Law School "Wasomi Nguli" wasikilizwe

Zako zinatoka wapi ndugu?
 
Law School wako sawa kabisa! Hatutaki mawakili vila.za mtaani!
Wanafunzi wengi ni vila.za sana, hawasomi, wanakariri mambo tu!
Kujenga hoja hawajui na hata Kiingereza tu ni shida kwao!
Kuna mawakili mtaani uwezo wao uko chini kiasi kwamba unajiuliza wamepita Shule ipi ya Sheria!
Vipi walimu, madaktari, wafamasia, wahasibu nk?

Vilaza ni sheria tu?
 
Wanafunzi hawa wanaofeli LST ni first class material. Hadi hapo unasema je?

Kadhia ya Law School "Wasomi Nguli" wasikilizwe

Unasema je pia kuhusu wasomi nguli hawa?
Hata katika katika CPA pia wapi "first class materials" lakini hupaswa kuanzia daraja la chini kidogo kwa masomo kadhaa, na hatimaye huja kumalizia umahiri wao kwa daraja la juu kabisa.

Ni lazima wafanye "harmonization" kwanza kwa kuwa shahaha katika vyuo vikuu tofauti hutofautiana kabisa. Ni kweli wote wanaweza kuwa na "lower second divisions" au "upper second divisions" ama hata "first divisions" lakini hadhi za hizo shahada ni tofauti kabisa.

Sidhani kama wahitimu wa shahada za sheria kutoka UDSM, UDOM, Mzumbe, SAUT na kadhalika (mpangilio haupo katika kigezo cha ubora wala "accreditation" ya chuo) kuwa wa ubora unaofanana pale watahiniwapo kwa mitihani inayofanana. Uzoefu unanionyesha kuwa, hata ukichunguza hayo matokeo kwa undani ni lazima utakuta vipanga waluofaulu kwa "single sit" karibu wote wanatoka katika chuo kimoja, wanao "suppliment" utakuta ni mchanganyiko wa baadhi ya vyuo, na wale walio " discontinue" wanatoka katika baadhi ya vyuo tu.
 
Kumbuka wanafunzi hawa hawaendi kufanya mitihani LST. Bali wanakwenda kusoma tena na baadaye kutahiniwa.

Hata first class material waliotoka chuo hicho hicho wanakumbwa na matokeo tata ya aina yake hapo LST.

Kwa maana nyingine hata walimu pale wakitahiniwa pale anonymously kama wanafunzi watafeli pia.

Kadhia ya Law School "Wasomi Nguli" wasikilizwe

Kulikoni mawazo hayo ndugu?
 
Law school ilipaswa ifundishwe na majaji na mahakimu na wanasheria wastaafu sio walimu wa vyuo vikuu.

Mwalimu ambae hana practical experience hasa walimu wetu wa kitanzania ni mwalimu tu. Akili ya walimu wengi kama sio wote inajulikana, ni kutunga mitihani migumu na kuona wanafunzi wanashindwa kufaulu ndio raha na faraja yao.

Walimu wetu wana mentality ya kwamba ukifaulu mitihani migumu basi wewe ni genius ama una akili sana.

Mitihani ya elimu za ulaya ni rahisi sana, sana na bado wana akili na uwezo kuzidi wataalamu wetu. Kama mitihani migumu ingekua ndio ugeniou basi Tanzania ingekua imejaa magenious tupu.

Walimu wa level ya post graduate wanapaswa kua ni wale wenye practical experience na sio hawa wakariri makaratasi wasiojua ulimwengu halisi unaendaje.

Nilisoma postgraduate degree hivi karibuni, yaani walimu wetu ni weupe vichwani balaa, wao wamekariri mi theory ya kizamani isiyo na uhalisia wowote kwenye ulimwengu wa kibiashara ama corporate world lakini wamekomaa wanafunzi wakariri hivyo hivyo. Ukijaribu kuwachallenge wanawaka balaa.

Tunahitaji kufanya reforms kwenye mfumo wetu wa elimu hasa postgraduate level. Haiwezekani kwenye level ya postgraduate watu wafundishwe kwa kukaririshwa ama wakaririshwe, haiwezekani.

Tatizo vichwa panzi wako Kila mahali. Waone hata kwenye uchangiaji humu.

Ninakazia:

"Ni muhimu kutambua Tanzania ni jamii ya watu waliojaa wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, upumbavu na ujuaji uliopitiliza."
 
Kumbuka wanafunzi hawa hawaendi kufanya mitihani LST. Bali wanakwenda kusoma tena na baadaye kutahiniwa.

Hata first class material waliotoka chuo hicho hicho wanakumbwa na matokeo tata ya aina yake hapo LST.

Kwa maana nyingine hata walimu pale wakitahiniwa pale anonymously kama wanafunzi watafeli pia.

Kadhia ya Law School "Wasomi Nguli" wasikilizwe

Kulikoni mawazo hayo ndugu?
Duh! Hapo mkuu kweli ni tatizo. Pengine kuna ukweli uliojificha, na huo ni kwamba, lengo kubwa ni kufelisha na wala si kufaulisha wanafunzi.
 
Hiyo Law School ndio chuo pekee hapa duniani ambacho kinachofelisha wanafunzi wengi kisha walimu wake kupongezwa.

Huku wajinga wakiwatetea hao walimu kwamba wanafunzi wa siku hizi ni wavivu, hawapendi kujihangaisha, wanafunzi wale ambao wametokea undergraduate kwa walimu walioridhishwa na ufaulu wao.

Au ndio mnataka kusema walimu wa undergraduate nao ni wajinga kama hao wanafunzi waliofaulu kwao? kwamba walimu wa undergraduate wa sheria nao wakipewa mitihani ya Law School nao watafeli?

Wengine wanasema tatizo ni kule wanafunzi walikotoka, kama kule walikotoka ni tatizo, hao walimu wa Law School kazi yao ni ipi? mbona bado wanafunzi wanafeli wengi hata wakifundishwa nao? kama muda ni mdogo basi uongezwe, lakini sio huu wizi wanaowafanyia wanafunzi.

Pia tuambiwe, kwani hao walimu wa Law School ni malaika walioteremka duniani kutokea sayari ipi? maana inaonekana wanakijua wao pekee kile wanachokifundisha, au ndio walifundishwa mbinguni?!

Kama nchi tuna matatizo:

"Ni muhimu kutambua Tanzania ni jamii ya watu waliojaa wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, upumbavu na ujuaji uliopitiliza."
 
Duh! Hapo mkuu kweli ni tatizo. Pengine kuna ukweli uliojificha, na huo ni kwamba, lengo kubwa ni kufelisha na wala si kufaulisha wanafunzi.

Haikufikirishi kuwa shule inayofelisha hakuna mzazi anayepeleka mwanafunzi hapo.

Shule inayofelisha inakuwa graded mwisho.

Shule inayofelisha huwajibishwa.

Nk, nk.

Yote hayo ni kweli isipokuwa LST.

"Ni muhimu kutambua Tanzania ni jamii ya watu waliojaa wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, upumbavu na ujuaji uliopitiliza."

Huo ndiyo ulio ukweli.
 
Tatizo wabongo niwavivu Sana wanakawaida yakuchukulia poa kila kitu imagine mtu anaanza kusoma one day before exam unafikr kitatokea Nini. Hyo hata makazini kwenye kutoa huduma wanajivutaaa utadhan wanafanya bure

Hudhani mzizi uko hapa ndugu:

"Ni muhimu kutambua Tanzania ni jamii ya watu waliojaa wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, upumbavu na ujuaji uliopitiliza."

Kwa nini kutengeneza hitimisho zito kama lako bila kuwa na ufahamu wowote wa mambo pale?

Kwa nini usiache yakawa angalau maoni huru?

Kwani hawa nao unasema je?

Kadhia ya Law School "Wasomi Nguli" wasikilizwe
 
Haikufikirishi kuwa shule inayofelisha hakuna mzazi anayepeleka mwanafunzi hapo.

Shule inayofelisha inakuwa graded mwisho.

Shule inayofelisha huwajibishwa.

Nk, nk.

Yote hayo ni kweli isipokuwa LST.

"Ni muhimu kutambua Tanzania ni jamii ya watu waliojaa wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, upumbavu na ujuaji uliopitiliza."

Huo ndiyo ulio ukweli.
Naongezea kidogo na sifa za ziada za ukuda, unoko na "sadism"
 
Mawazo duni kabisa. Unafundisha chuo gani ndugu kuja kauli hollow kama hii?

Kwamba elimu ya mwaka 47 ilikuwa bora zaidi kuliko ya leo siyo?
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sasa hivi kimeja wauza sura wengi sana. Asilimia kubwa sana wanamaliza vyuo sasa Kingereza kinawapiga chenga sana, hawajui mambo mengi sana ambayo ni basic na pia hata wanavyojenga hoja unaona kabisa uwezo wao critical thinking uko chini sana. Tofauti ni kwamba sasa hivi wanaomaliza vyuo ni wengi.
 
Achana na mimi Mburumundu wewe. Nani kakuita hapa?
Toa kulia Lia eti school of law inawaonea, Sasa kilaza kama wewe ulitaka upitishwe bwelele na huku badala ya kusoma unakalia boda zako na kubeti. Naomba WALIMU w school of law WAENDELEE kukaza kabisa,kabisaaa. Maana elimu inaenda kupoteza kabisa. Ifike mahala heshima ya degree na masters viwe na heshima kama zamanii
 
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sasa hivi kimeja wauza sura wengi sana. Asilimia kubwa sana wanamaliza vyuo sasa Kingereza kinawapiga chenga sana, hawajui mambo mengi sana ambayo ni basic na pia hata wanavyojenga hoja unaona kabisa uwezo wao critical thinking uko chini sana. Tofauti ni kwamba sasa hivi wanaomaliza vyuo ni wengi.
Naunga hoja saana ndugu yangu, ifike kipindi watu waone elimu sio kitu Cha kucheza. Nawapongeza Kwa kukaza kabisaa, mpaka ifike mahala mtu afanane na degree au masters.
 
Toa shombo zako za kulia Lia eti school of law inawaonea, Sasa kilaza kama wewe ulitaka upitishwe bwelele na huku badala ya kusoma unakalia boda zako na kubeti. Naomba WALIMU w school of law WAENDELEE kukaza kabisa,kabisaaa. Maana elimu inaenda kupoteza kabisa. Ifike mahala heshima ya degree na masters viwe na heshima kama zamanii

Kuna tofauti kubwa baina ya law school na school of law. Haya mambo siyo size yako. Huku mawazo ya maprofesa yanazingatiwa siyo yenu wenye ajira za laana
 
Back
Top Bottom