- Thread starter
- #121
Mimi siyo mwanasheria, ila kwa ulewa wangu, nafikiri Law School ingalikuwa na viwango tofauti kwa watahiniwa. Mathalani, kama ilivyokuwa kwa CPA, tuseme wanafunzi wanapomaliza shahada zao za kwanza katika vyuo vikuu vinavyotambulika, basi waingie katika daraja fulani, tuseme "entry level B" na hapo itampasa afanye masomo machache tu ya daraja hilo.
Endapo akafaulu katika daraja hili, itampasa afanye mitihani mingine ya daraja la juu zaidi, tuseme "final level A". Hapo nafikiri itakuwa njia rafiki ya kuwatahini watahiniwa, kuliko kuwabebesha zigo la masomo mengi kibao na kumtaka ayafaulu yote kwa mpigo mbele ya watahini ambao ni wanoko kupindukia.
Ni kweli kabisa "professional bodies" zina viwango vyake vya kimataifa ilivyojiwekea ili kuilinda hadhi na maadili kwa watahiniwa. Lakini ni ukweli pia lengo la kuwatahini watahiniwa si kuwafelisha wengi kwa pamoja, na tena kwa kiwango cha kutisha, isipokuwa ni kuchagua "the right teaching methodologies" ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Nakumbuka enzi hizo nikiwa katika elimu yangu ya kuungaunga, alitokea mhadhiri mmoja ambaye alikuwa akifundisha somo la "statistics" na ambalo lilikuwa limejaa kanuni nyingi sana za kimahesabu. Na kama ilivyo kawaida, umahiri wa kukokotoa hesabu una changamoto nyingi sana kwa wanafunzi ambao wana "background" ya "ungwini"
Basi alikuwa na kawaida ya kutunga mitihani migumu sana, na siku ya mtihani wake ilipofika, ni dhahiri alionyesha kupania kichizi ili madenti wafeli kwa wingi. Alipoona wanafunzi wengi wanakodolea tu karatasi za mtihani pasipo kuanza kufanya. Kwa furaha kubwa alitoa kicheko cha kejeli na kubwatuka kwa sauti kubwa sana,
"AT LEAST I HAVE KILLED ONE"
Hapo ndipo utapata picha ya watahini waliokuwa wanoko na "sadists" ambao hawajali chochote kile kuhusu kufeli kwa idadi kubwa ya watahiniwa kwa mpigo.
Wanafunzi hawa wanaofeli LST ni first class material. Hadi hapo unasema je?
Kadhia ya Law School "Wasomi Nguli" wasikilizwe
Unasema je pia kuhusu wasomi nguli hawa?