On thecontrary.
Ngoja nikueleze jambo pengine utaanza kuona mwanga na haya yote yanayoendelea. Vinginevyo utanipa usumbufu mkubwa wa kueleza kirefu zaidi ya hivi nitakavyoeleza hapa.
Ni hivi: Tambua kwamba kuna waTanzania wengi tu wametekwa, kuuwawa au hawajulikani walipo kwa sababu tu ya "walitukana. walitumia maneno yasiyo na staha, n.k. kuhusu hawa msiotaka watangaziwe hayo hata kama ni ya uzushi.
Sasa naomba unieleze hapa mwenyewe; kama maneno ya vijana tu kama akina Mdude Nyagali yanawanyima raha mioyoni mwao kiasi cha kuwapoteza; haya ya "taarifa za uzushi" (kama mnavyopenda kuziita, inawaacha wakiwa na hali gani hao wahusika?
Hata kama hawajafa, au kupata hayo majanga wanayozushiwa, jiulize hali zao kiakili zitakuwa vipi? Haya siyo mateso ya kutisha kwa watu ambao wanapenda kuabudiwa kama miungu?
Na hata ukiachana na hali hiyo ngumu wanayokutana nayo kiakili, wewe unadhani watakuwa na utulivu gani dhidi ya hayo wanayotangaziwa kwamba yataendelea kuwa "uzushi" kila mara?
Tuliambiwa humu JF "Magufuli alikuwa anachapa kazi badala ya kuzurura Kariakoo"!