Wanaharakati wakae mbali na taarifa za vifo vya viongozi vinahawaribia reputation.

Headline yako ni click bait? Umeiandika kwamba ni habari za vifo na maelezo yako yanahusu habari za ugonjwa? Haufahamu kama kuna tofauti kati ya ugonjwa na kifo?
 
ki kawaida ni jukumu la serikali kuondoa taharuki.

wanaoitaka serikali ife wala haina haja ya kuwahi kushangilia alafu mu anatokea kesho yake.

kama kavuta atatangazwa tu , kafa magu hapa katangazwa sembuse hawa wengine
Kisaikolojia inasaidia wananchi wenye hasira.

Ikiwa ni kweli ikatangazwa ndo utashangaa wanafanya sherehe kabisa.
 
Shida haiko hapo unaposema.

We hushangai kwanini taarifa hizo zinapokelewa kwa furaha na wananchi walio wengi?

Hilo ndo la kujiuliza, mara zote unakuta bado watu wanatamani ingekuwa kweli.

That’s where the problem lies.
Lakini pia on the other way round huyo anayesingiziwa huwa anaumia kujua kwamba kumbe watu wanafurahia wakisikia anaumwa, maana yake anachukiwa sana !
 
Lakini pia on the other way round huyo anayesingiziwa huwa anaumia kujua kwamba kumbe watu wanafurahia wakisikia anaumwa, maana yake anachukiwa sana !
Exactly, ndo maana wanatumia nguvu nyingi kuaminisha watu kuwa wako fit.

Ndo utagunduwa kuwa pamoja na madaraka na pesa walizonazo, bado wana “insecurities”
 
Hao watu wenu ni wapumbavu, Kiongozi kama binadamu atafariki siku mda wake ukifika sio siku wao wanavyotaka maana hawakuwapa uhao wenyewe.

Wao waendelee na chuki na uzushi kuwadanganya wapumbavu wenzao.

Sio tuu hawa wanaharakati Kuna wale wapumbavu wengine wanaitwa Manabii huko Makanisani.

Msichokijua ni kwamba mtu unaemchukia sana sana inaishia Kumpa heri na Maisha marefu,hii ni kanuni ya ulimwengu Ukiwa mpumbavu huwezi jua maana wewe utaumia yeye utampa heri Kwa kutumia energy Yako.
 
Enemy of your enemy

Ukiona utabiri mwingi wenye matamanio ya watu wengi wakitaka watawala wapatwe na mambo mabaya ikiwemo magonjwa na vifo, basi tambua kuwa uongozi uliopo ni "hopeless & useless"
 
Ukweli ni kwamba kilio kijubwa cha Watanzania ni kwamba apatwe na mabaya
 
Wasaka tonge hao, tumeshawazoea
 
Unakumbuka zile simulizi za fisi hua anamnyemelea binadamu akiwa na matumaini ile mikono itadondoka jinsi inavyo tikisika? Ndio hii sasa ya wanaharakati wetu.
Majibu mnayo,, msijitoe ufahamu.

Nyerere alikufa, hakuna aliyefanya sherehe. Mkapa hakuna aliyefanya sherehe. Mwinyi hakuna aliyefanya sherehe.

Magufuli waliofanya sherehe walitendewa unyama. Na huyu wanaotamani apite hivi, ili washerehekee wana machungu moyoni ya vifo, mateso, manyanyaso, matusi na vifungo jela.
 
Majibu mnayo,, msijifanye hamjui chanzo na sababu.

Historia ya Marais kusherehekea vifo vyao, ilianzia kwa Magufuli. Na huyu akifa watu watashangilia wazi wazi au kimya kimya.

Nyerere alikufa hakuna aliyefanya sherehe. Mwinyi hakuna aliyefanya sherehe. Mkapa hakuna aliyefanya sherehe, vipi iwe Hawa wawili. Kila mtu atavuna alichopanda.

Msilazimishe kupendwa mkijua mnaendelea kuteka, kuua na kunyanyasa.
 
Wapumbavu ni wale wanatumikishwa na hao wanaharakati
 
Hivi ni wewe unayeandika haya leo, au kuna mwingine anatumia jina?
maneno hayo ni yangu na ninaweza kuyatetea, kuhusu anayeyasikia anayaelewaje au kuyapokeaje inaweza kua na mvutano , ila mimi binafsi naweza yatetea vyema sana. Kitu pekee nachosikitika sio muandishi mzuri

CHADEMA wakishabikia habari za "uzushi" kama ulivyouita, wanakuwa wamejiondoa katika uaminifu wao kupambania taifa hili; kirahisi tu hivyo?
Chadema can do better mkuu, kwa platform waliyonayo na influence waliyonayo wanaweza fanya makubwa zaidi, mikakati yao iko poor, tunaweza sema hili hata wao wenyewe wameliona ndo maana wakamuweka Mbowe pembeni, --- hili ni jambo la maana sana kutokea lakini ujio wa TAL nao umeleta shida, lengo la kufika ikulu kwa haraka ndo matokeo yake yale 2025, (shida ninyi mnaona lawama pekee kwa ccm tu, effect ya chadema kwenye sakata lile hamuioni)

TAL kama alikua yupo tayari SSH aendelee beyond 2025 bila election ili tupitie mchakato huo wa mabadiliko ya kweli, alikua na shida gani kumuacha SSH ajipitishe in peace na tukaendelea na hiyo michakato. badala yake ni nini. Nilikuambia kipindi kile heri kuandamana Post Election kuliko siku ya uchaguzi , nikisema hivi unakuja sema nafurahia mauwaji, vipi vijana wachadema walikua wanahimiza watu , huoni hapa victims ni wananchi kwa ujumla wao na waliokua wanasubiri matokeo ya sakata lile ni CCM na CHADEMA mkuu --- mimi huu ndo msimamo wangu, na huku uraiani nilipo wanaonizunguka nawapa mtazamo huu na wanaanza kunipata mdogomdogo


Wanaharakati, hivyo vyama vinavyojiita upinzani wa kweli wa kweli wafocus na practical solutions, Hii mimi nimefanya bado nafanya na nitaendeea kufanya na inafanya kazi, na naiona ina manufaa zaidi na ufanisi mkubwa.

general public iliyo desperate kuiondosha ccm, yenyewe ipo tayari kufata sheria? inajitahidi kufata sheria? inademand kutengenezwa sheria? / kanuni? kama jamii kwa ukubwa wake vitu hivyo haivifanyi basi bado hata huyo samia asuse yeye mwenyewe sasahivi arudi kizimkazi matatizo haya yataendelea tu hivihivi.

Kuna muda hata ACT walikua wanajitahidi kuliko hata chadema kwenda kutafuta matatizo ya kuyaandikia mapendekezo sijaona hiyo tanganyika watu wanaililia humu watu wakiunga mkono ACT kwenye juhudi zao zile, mimi binafsi nimeanza kufanya mambo hayo na nitaendelea kufanya mambo hayo changamoto zipo ila ni heri njia hii,

Hawa watu wanaotangaziwa uzushi wana maana kubwa kiasi hicho kwako?
hao kama kujifia watajifia tu wenyewe wala haihitaji kuhangaika kuomba wala kuandika sana. Umuue kiongozi kwa kufungua thread, na kuingia instagram live, ni kuendelea kupumbaza jamii tu


Huo mstari na nusu wa mwisho, inamaana uliunga mkono sana Samia alipopata ushindi haramu, na kuua waTanzania kwa mategemeo tu kwamba ataiua CCM?
kama lengo ni kuimaliza ccm , mtu yeyote tofauti na SSH kuchukua kiti 2025 ile ingekua tumepiga hatua nyuma. wapumzike kwa amani wote waliokufa kutokana na kadhia ile.
SSH angekaa pembeni kwenye chaguzi ile angeiruhusu ccm kufufuka
 
Kisaikolojia inasaidia wananchi wenye hasira.

Ikiwa ni kweli ikatangazwa ndo utashangaa wanafanya sherehe kabisa.
mi naona tusubiri tu afe ndo tuanze shangilia, kushangilia hii iliyopo sasa ni sawa na kushangilia goli la kusawazisha ama la ushindi alafu VAR ije kulifuta , sidhani kama mtu atasema "aaah atleast nilifurahi" zaidi kuongeza machungu tu.

wewe Imagine Netanyahu baada ya uvumi wote kwamba kafa lakini yupo hai, unataka kusema wale waliopata faraja wakati wa uvumi wanaifurahia faraja ile wakati netanyahu bado anazurura ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…