Wananchi wamfukuza Mbunge Angelina Mabula mkutanoni, hali yake mbaya jimboni kwa kutoleta maendeleo kwa wananchi

Wananchi wamfukuza Mbunge Angelina Mabula mkutanoni, hali yake mbaya jimboni kwa kutoleta maendeleo kwa wananchi

Mbunge ndio daraja la wananchi na serikali kama kero za wananchi hazifanyiwi kazi anafanya nini Bungeni ? Mwanza mji umekua mchafu sana, barabara ni tatizo, usambazaji wa maji miji mipya changamoto, mishahara kiduchu sekta binafsi, halafu wao wanazidi kujitafutia mali na kutudanganya Mama anaupigwa mwingi ! Tukutane kwenye box la kura, kura yangu halali haiwezi kwenda CCM wao washinde na kura zao za wizi kama kawaida yao.
Nimeuliza wana uhakika gani hakupeleka kero yao bungeni au mahala panapohusika?

Kwani Tanzania kuna sehemu isiyo na kero ya wananchi? Masaki tu kule wanapokaa mabalozi na washua kuna kero hadi za takataka kutokusanywa kwa wakati!

Nchi hii wananchi kutokana na ujinga wenu mnapigana na msichokijua. Mbunge hakusanyi kodi, mbunge sio afisa masuhuli. Kwa katiba yetu hii mbunge ni boshen tu.

Siku mkipata akili vizuri mtajua shida ni Katiba yetu ndo mtafanya maamuzi sahihi. Ila kwa kuwa kwa sasa bado mna ujinga mwingi, endeleeni tu na ujinga wenu. Na mkiweza mtafukuza wabunge wote kila siku.
 
Kuna jamaa alioa binti yake miaka ya mwisho mwisho wa uhai wa JPM kisa alikuwaga waziri wa nini nini vile! Mara paap akakata moto, mama mkwe kachechemea kwenye uwaziri baadae katolewa saiv anajiliza mke hakumpenda alipenda status ya mamkwe, sasa ukiongeza na hii aroooo kazi anayo
Hatari sana, halafu akiwa Waziri alimtelekeza mume wake ambaye alikuwa anaumwa, hakumsaidia chochote hata kununua panado, jamaa amefariki, na yeye hana Uwaziri, na ubunge ndio unamponyoka hivyo
 
Wanaweza kuwa ni WA mtaa au kata Fulani tuu sio Jimbo Zima.

Mwisho Huwa mnanishangaza sana ,tuchukulie mnaleta Wabunge wa Upinzani Sasa watafanya nini na hela zinatoka Serikali ya CCM?

Hayo mambo Yana maana kama mtashika Dola kinyume na hapo mtasalia hivyo hivyo bora mrudishe ccm hao hao.
Kosa la marehemu hakuvaa kondomu !!
 
Hatari sana, halafu akiwa Waziri alimtelekeza mume wake ambaye alikuwa anaumwa, hakumsaidia chochote hata kununua panado, jamaa amefariki, na yeye hana Uwaziri, na ubunge ndio unamponyoka hivyo
Eeeh na bamkwe akafariki tena!! Wanawake tuna nyodo na kusahau haraka sana
 
Back
Top Bottom