Wanangu msiogope kujenga, hapa nimetumia 6M

Wanangu msiogope kujenga, hapa nimetumia 6M

Kama umefyatua tofali wewe mwenyewe, ukajenga mwenyewe kwa nguvu zako, mchanga ukachimba hapohapo, cement ukanunua chini ya elfu 10, basi inaweza kuwa kweli ni kwa gharama hiyo. Kinyume na hapo, haiwezekani!
 
Kwani hapo kimefanyika nini zaidi ya mawe msingi,kujenga nyumba yenyewe,madirisha na kupiga plasta pamoja na hizo nondo za madirishani ndio wewe hayo madirisha wanakwambia milioni tatu na hela unatoa...
Mkuu hata kama ila ni zaidi ya milion 6. Hayo mabati na mbao alizotumia kuezeka na ela ya ufundi vinakula zaidi ya milioni 3, sasa hlo pagale na msingi inawezekanaje alijenge kwa milion 3 iliyobaki
 
Kama umefyatua tofali wewe mwenyewe, ukajenga mwenyewe kwa nguvu zako, mchanga ukachimba hapohapo, cement ukanunua chini ya elfu 10, basi inaweza kuwa kweli ni kwa gharama hiyo. Kinyume na hapo, haiwezekani!
Naunga mkono hoja
 
Apana kwa ujenzi wa sasa ,tena pwani ambako asilimia kubwa watu wanajenga kwa tofali za block ,na kuezeka japo bati sio za rangi lakin izo nazo dukani bei yake sio ndio imepoa kivile .. million 6 inafikirisha labda kama fundi wemwenyewe ..🤣
 
Mleta mada kaoa mwaka jana mwishoni upande wa zawadi ulikuwa hivi
Wazazi : Tumemzawadia kijana wetu uwanja ataamua mwenyewe kujenga

Kamati: Bwana harusi tumemzawadia bati 30 na Lori 3 za mchanga

Wakwe: Hawa walimpa binti yao mifuko 50 ya saruji na matofali elfu 2000 na cash 3m

Wafanyakazi wenzake: Nondo

Wanafunzi wenzake: Tutamlipa Fundi

Majirani: Tutamuingizia umeme na kumlipia mbao

Kwa kifupi mtoa mada alipata changizo ndiyo maana kaweza kujenga kwa hela hiyo ila kiuhalisia kwa hiyo hela hpn
 
Hahahaaa! Swahiba sema mleta uzi amekuwa mkali sana.

Angedadavua hata kwa uchache hiyo milioni sita yake sababu mwisho wa siku anaeza fanya watu waamini ujenzi ni kitu rahisi hali ambayo sio kweli.
Yan hapo kwa muonekano wa ile itakua vyumba 3 na sebule,nyumba kama ile kuanzia gharama za uchimbaji msingi hadi mkanda kajibana sana mln 3,bado boma,kupaua hata kama ni bati za kawaida gauge 32,plasta,wiring,madirisha n.k,kwa kweli mln 6 hapana 😀
 
Mkuu hata kama ila ni zaidi ya milion 6. Hayo mabati na mbao alizotumia kuezeka na ela ya ufundi vinakula zaidi ya milioni 3, sasa hlo pagale na msingi inawezekanaje alijenge kwa milion 3 iliyobaki
Hiyo nyumba ni kweli haizidi 6m. Mimi nimejenga nyumba ya vyumba vitatu 4×3m, sebule 5×4m, jiko 2.5×4m, store 2×2m, wc 1.2×3m, kupaua bati 70, grill 8 za 5×6m kwa 10m. Na nimeijenga klm mwezi wa 8/22
 
Mkuu hata kama ila ni zaidi ya milion 6. Hayo mabati na mbao alizotumia kuezeka na ela ya ufundi vinakula zaidi ya milioni 3, sasa hlo pagale na msingi inawezekanaje alijenge kwa milion 3 iliyobaki
mkuu, kibanda changu ( size kinafanana na icho muundo tofauti kidogo) wakati ipo hatua hiyo iligonga hapo hapo 6m give or take ( mwaka jana mwezi wa 3 )
nakumbuka upauaji kila kitu mpaka ufundi ilikuja 2.7m ( bati la kawaida geji 30 Alaf )

trick ni kuachana na ujenzi wa whatsapp na kufata materials mwenyewe, mtoa mada yupo sahihi kabisa na hiyo bei
 
Mkuu ina sqm.
 
Hiyo nyumba ni kweli haizidi 6m. Mimi nimejenga nyumba ya vyumba vitatu 4×3m, sebule 5×4m, jiko 2.5×4m, store 2×2m, wc 1.2×3m, kupaua bati 70, grill 8 za 5×6m kwa 10m. Na nimeijenga klm mwezi wa 8/22
So jumla ilikuwa na sqm ngapi mkuu? Kwakweli mnanistaajabisha
 
kama ya OP hapo juu, maana design ya paa ni hivyo hivyo, chini ndiyo kuna utafauti,
vyumba vitatu(4x3), sebule(5x4), jiko dogo, yaani haina tofauti na ya Algore hapo juu
Labda mkuu, dar au wapi? Mimi msingi tu umekula 4.85 na badi tu zitanila kama 4.5 ml hapo bila ufundi wa la mbao sema ina sqm 132. Ndio maana nikauliza
 
Back
Top Bottom