Wanaopinga ndoa wana matatizo au wamekulia kwenye familia zenye mgogoro

Wanaopinga ndoa wana matatizo au wamekulia kwenye familia zenye mgogoro

Watu badala ya kupeana mbinu za kutoboa haya maisha wanashauri watu waoe utalawalisha hao watoto nn? Utawasomesha na nn? Lazima ufikirie haya kama kipato chako ni Cha kusuasua, usichukulie advantage ya mababu zetu walikua wakilima hata robo Heka gunia 20 Leo hii mvua hakuna, shamba bila mbolea havioti, pembejeo ghali, ukisoma ajira hakuna.

Labda mtuandikie mnayaendeshaje haya maisha? Mnafanya kazi gan?
Wale wanao enjoy national cake [emoji512][emoji512] labda wasiache kuoa.

Usiige kwa kua Fulani kafanya hivi na ww ufanye kama hujui njia anazopita, don't apply the same way even if you know where s/he passes through....

Oa kwa ajili ya kujenga kizazi Bora sio uzalishe watoto wa mitaani au umtese mtoto wa mtu ( mke). Usioe kwa ajili ya ngono tu. Ndoa ni taasisi kubwa Sana kwa ambao hawajui Siri.

Usipoa sio dhambi Bali ni pale utakapoa na kushindwa kutekeleza majukumu ya taasisi hio. Kamwe usitengeze laana na vizazi vya ajabu.

Kama unawezo wa kutunza familia oa mapema kwa sababu utatengeza kizazi Bora, mtoto apate elimu nzuri, matibabu, afya njema kwa ajili ya kizazi cha baadae. Create the best generation, the grateful children who will not blame their parents that they make them in bad situation.

The children who will not cry because of poverty. Create the way for them to enjoy the life of this world [emoji288][emoji288].

Alisikika mzazi mmoja akisema "acha tu wakikua watajitafutia" wamekua kuku wa kienyeji?

Hao wanaosema Wanaokataa ndoa ni mashoga wao ndio wanazalisha mashoga kwa sababu ya kutowaandilia watoto maisha Bora japokua ushoga wakati mwingine inasababishwa hormone.
Umemaliza yote mkuu...uzi ufungwe
 
Wengi wao ni

Wazazi wao walikwepa majukumu ya malezi bora eg Mume kuendekeza michepuko na kusahau familia,Mke kuwekeza kumlisha limbwata Mume na kusahau kujaza upendo kwa watoto

Watoto waliotelekezwa kwa ndugu

Watoto wa michepuko

Mimba zisizo tarajiwa kisha zikakanwa

Waliopatikana kwa matokeo ya ubakaji. Mabazazi yanayobaka yalaaniwe yanatuharibia jamii

Waliokacha shule na kukimbilia kuvuta vijiweni,dating za kipuuzi,kula kimasihara

Waliopatikana vilabu vya matapu tapu

etc etc etc
Watu wamezaliwa na kulelewa kwenye ndoa zilizofungwa kwenye kanisa takatifu la mitume katoliki,msikitini na ndoa zinavunjika mapema tu,yaani miaka mitano mingi
 
Kumekuwa na mijadala mingi sana inayowazuia vijana kuoa au kuolewa, kubwa sana ni kukataa kuoa. Hiyo ni kutokana na mfumo wa maisha ya sasa yalivyo. Ndoa nyingi hazidumu na uaminifu ndani ya ndoa umepungua sana kiasi kwamba wanandoa kusalitiana limekuwa jambo la kawaida na ndio sababu ya ndoa nyingi kuvunjika.

Pamoja na yote hayo haipaswi kuwepo na mjadala wa kuhamasishana watu wasioe/kuolewa au wasiingie kwenye ndoa. Katika hilo kuna watu wanaingia mkenge kwa kufata mkumbo au kumuiga mtu fulani kwa kuwa hataki kuoa/kuolewa nami sioi/siolewi. Hiyo sio poa kabisa kwa sababu watu wanatofautiana na kila mtu ana changamoto zake, changamoto za mke wa fulani haziwezi kuwa sawa na changamoto za mke wa fulani au za mume wa fulani haziwezi kuwa sawa na mume wa fulani. Halafu wengi wanaokataa kuoa/kuolewa wana changamoto za kisaikolojia ambazo wamezipata either kwa kushuhudia au kusimuliwa.

Kwahiyo nawaomba vijana ambao hamjaoa au kuolewa msiogope kuingia kwenye ndoa. Usiangalie na kulinganisha na ndoa ya fulani kwani ndoa yako haiwezi kufanana na hao wengine.

Kubali Ndoa
Ndoa ni Baraka
Ndoa ni Furaha
Ndoa ni Heshima
Ndoa ni baraka
Ukioa au kuolewa tu utapata
1. BMW X7 brand new
2.Audi A8 brand new
3. Billion 10 bureeee
4.Luxury mansions Kama 5 hv
 
Kumekuwa na mijadala mingi sana inayowazuia vijana kuoa au kuolewa, kubwa sana ni kukataa kuoa. Hiyo ni kutokana na mfumo wa maisha ya sasa yalivyo. Ndoa nyingi hazidumu na uaminifu ndani ya ndoa umepungua sana kiasi kwamba wanandoa kusalitiana limekuwa jambo la kawaida na ndio sababu ya ndoa nyingi kuvunjika.

Pamoja na yote hayo haipaswi kuwepo na mjadala wa kuhamasishana watu wasioe/kuolewa au wasiingie kwenye ndoa. Katika hilo kuna watu wanaingia mkenge kwa kufata mkumbo au kumuiga mtu fulani kwa kuwa hataki kuoa/kuolewa nami sioi/siolewi. Hiyo sio poa kabisa kwa sababu watu wanatofautiana na kila mtu ana changamoto zake, changamoto za mke wa fulani haziwezi kuwa sawa na changamoto za mke wa fulani au za mume wa fulani haziwezi kuwa sawa na mume wa fulani. Halafu wengi wanaokataa kuoa/kuolewa wana changamoto za kisaikolojia ambazo wamezipata either kwa kushuhudia au kusimuliwa.

Kwahiyo nawaomba vijana ambao hamjaoa au kuolewa msiogope kuingia kwenye ndoa. Usiangalie na kulinganisha na ndoa ya fulani kwani ndoa yako haiwezi kufanana na hao wengine.

Kubali Ndoa
Ndoa ni Baraka
Ndoa ni Furaha
Ndoa ni Heshima
Kukataa ndoa tafsiri yake NI kukataa kushinda mahaka Mani,kukataa kuumia,kuuwa,au kuu Wawa,

Na kchagua kuishi kwa hakili na PESA badara ya mwanamke

Mwanaume unapo andika kataa ndoa una maanisha unataka kuolewa ama🤷🏼‍♀️
 
Wengi wamepandikizwa sumu na wazazi wao yaani wamelelewa na mzazi mmoja,

Ogopa sana mwanaume aliuelelewa na mama peke yake huyo ni zaidi ya koboko[emoji23],
 
Mkuu serikali ifanye haya ILI kuokoa ndoa

👉 Kwanza matatizo ya ndoa yamalizwe na wazee wa koo za Wana ndoa wenye mgogolo

badara
ya mahakama na WATU wa ustawi

Kwasababu
👉Kwanza wazee wa koo wana zielewa vema tabia za Wana ndoa

Kwamba

Yupi
Malaya,yupi mkolofi,yupi mvuta bange,yupi mlevi,yupi ana mdomo na yupi mpole

Hakika wata hukum kwa haki

Lakini Hawa ma barozi,ustawi wa jamii na mahakama/mahakimu,wapo kilushwa za ngono na kupata asilimia kadhaa
Kwahiyo Hawa jengi Wana bomoa
Kwa masrah

Na hawaUstawi wa jamii washughurike na Haki za vipofu, viziwi ,wafungwa,viwete na WATOTO wa mitaani

nikukumbushe kwamba mashoga niwale WANAO ingiliwa kinyume na maumbile na sababu zinaweza kuwa

Kuzaliwa hivyo/ulithi,tamaa ya Mali,uvivu na kupenda bule bule
Umeongea point na nimeielewa sana. Huko kote umeeleweka ila bado haisababishi watu kushawishi wenzao kukataa ndoa.

Hiyo point ya uvivu sasa ndo tunarudi kule kule kwangu. Wanaoshawishi wenzao wasioe wao ni wavivu wa kila kitu ndo maana wanataka wawekwe wao ndani
 
Vijana wana matatizo hata hivyo inachangiwa na ugumu wa maisha ndio maana unaona vitu vya msingi vinapotezewa na kukwepa majukumu haya yote sio familia tu ni pamoja na Serikali hawana maandalizi mazuri kwa vijana wao wao wanandaa Viongozi tuu..
 
Umeongea point na nimeielewa sana. Huko kote umeeleweka ila bado haisababishi watu kushawishi wenzao kukataa ndoa.

Hiyo point ya uvivu sasa ndo tunarudi kule kule kwangu. Wanaoshawishi wenzao wasioe wao ni wavivu wa kila kitu ndo maana wanataka wawekwe wao ndani

Unazungumzia kuhusu kataa ndoa?

Kuhusu hili siungi mkono
Na kuhusu wavivu kuwekwa ndani hili pia siungi mkono

Ila ushauri wangu ili kuubadili huu upepo wa wimbi la WATU kukataa kuowa ndiyo huo hapo mkuu
 
Ujue Mwanamke ukimkataa bhana anaanzaga kukukejeli anadhani ni yeye tu anakataaga watu. Tumekataa kuwaoa wanaanza ooh Upindee ooh nyeto ooh. Sa hao walowapa Mimba mpaka mkawa Masingo Maza nao ni Upinde au? Tulizeni Komwe Birthday mnazosheherekea kila Mwezi zinawatosha ndoa Waachieni Bibi zenu.
 
Back
Top Bottom