Protector
JF-Expert Member
- May 20, 2019
- 422
- 893
Kumekuwa na mijadala mingi sana inayowazuia vijana kuoa au kuolewa, kubwa sana ni kukataa kuoa. Hiyo ni kutokana na mfumo wa maisha ya sasa yalivyo. Ndoa nyingi hazidumu na uaminifu ndani ya ndoa umepungua sana kiasi kwamba wanandoa kusalitiana limekuwa jambo la kawaida na ndio sababu ya ndoa nyingi kuvunjika.
Pamoja na yote hayo haipaswi kuwepo na mjadala wa kuhamasishana watu wasioe/kuolewa au wasiingie kwenye ndoa. Katika hilo kuna watu wanaingia mkenge kwa kufata mkumbo au kumuiga mtu fulani kwa kuwa hataki kuoa/kuolewa nami sioi/siolewi. Hiyo sio poa kabisa kwa sababu watu wanatofautiana na kila mtu ana changamoto zake, changamoto za mke wa fulani haziwezi kuwa sawa na changamoto za mke wa fulani au za mume wa fulani haziwezi kuwa sawa na mume wa fulani. Halafu wengi wanaokataa kuoa/kuolewa wana changamoto za kisaikolojia ambazo wamezipata either kwa kushuhudia au kusimuliwa.
Kwahiyo nawaomba vijana ambao hamjaoa au kuolewa msiogope kuingia kwenye ndoa. Usiangalie na kulinganisha na ndoa ya fulani kwani ndoa yako haiwezi kufanana na hao wengine.
Kubali Ndoa
Ndoa ni Baraka
Ndoa ni Furaha
Ndoa ni Heshima