Ndio maana tunaita injili habari njema. Injili inakuambia kwamba kuna mtu mwenye dhambi na aliye kifungoni ambaye amelipiwa deni na yupo huru kutoka kwa amani na furaha.
Yesu alikuwa anapenda kusema enenda zako kwa amani, imani yako imekuponya. Hii ni habari njema kwamba sitakiwi kuingia motoni kwasababu ya dhambi zangu kwasababu tayari nimelipiwa deni na niko huru kuishi kwa amani.
Ukimwamini Yesu Kristo unahesabiwa haki. Mbele za Mungu unakuwa mtakatifu kwasababu yeye anachukua nafasi yako na wewe unachukua yakwake. Alihukumiwa ili wewe na mimi tusihukumiwe. Alichukua nafasi zetu. Sasa tukiamini, tunaokolewa.