Wanasayansi naomba mnisaidie maana Quran inaniambia mtoto anaumbwa baada ya sperm kuingia kwenye damu iliyoganda

Wanasayansi naomba mnisaidie maana Quran inaniambia mtoto anaumbwa baada ya sperm kuingia kwenye damu iliyoganda

Mkuu unafahamu kiarabu?
Maana neno lilotumika kwenye aya ile ni “maa” ambayo hufasirika kama “fluid” kwa kiingereza…

Na nimekueleza kuwa damu iendayo kwenye pumbu hutoka maeneo karibu ya ini… hivyo ni kweli manii huzalishwa kwenye pumbu lakini Quran imesema “maa” kwa maana ya “fluid” ambayo damu na manii pia huwa katika mfumo huo.
Quran imesema mwanadamu anaumbwa kwa fluid inayotokea kwenye maeneo kati ya mbavu na uti wa mgongo.

Mkuu hapa kuwa muungwana na kukubali kwamba quran imedanganya. Huo ndio ukomavu.

Baada ya hapo kimbilia kwa Yesu Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhambi, uokolewe na kuupata uzima wa milele.
 
Unachanganya mambo. Waliomsulubisha walifanya vile kama sehemu ya kumhukumu mtu waliyeona ni mhalifu kwa mtazamo wao.

Lakini Yesu mwenyewe alikuwa anajua kusudi la kusulubiwa kwake na aliwafundisha wanafunzi wake na baadae mtume Paulo alilielezea kwa undani zaidi. Ndio maana Yesu hakufanya utetezi wowote wakati wa mashtaka yake kwasababu ilikuwa muhimu apitie msalabani.
Alifanya utetezi ila alikosa kumbuka alipiga kelele akisema e Mungu wangu mbona unaniacha hapo alikua anata nini
 
Afu Qur'an hiyohiyo inakataa kwamba mungu Hana shirki Yaan hafany kaz na mtu na wanaupinga Sana utatu mtakatifu lakin katika haya iyoapo tunaona mungu anashirikiana na mtu au watu katika uumbaji sasa wadau hiyo imekaa vipi ni nan huyo anaeshirikiana na mungu kuunda mbegu kuwa damu Hadi pande la nyama mpaka mifupa?
Soma mwanzo 1:26 uje uulize tena swali lako
 
Mh! Mi naona kama maelezo ya Quran yana kaufadhali kidogo kwani yanaendana na sayansi hata kama hayako clear sana. Hofu yangu iko kwenye kitabu changu. Kinasema Maria ambaye 'hakumjua' mwanaume kwani alikuwa bikira alipata mimb!
Mbona hushangai kuwa Qur'an inatabiri kuwa waliokufa watafufuliwa me naamini kama hujawahi kuona bikra akizaa bila kumjua mwanaume pia hujawahi kuona mtu akifufuliwa na Kwa jibu lolote utakalonipa usitegemee majibu yangu mengine maana nahitimisha Kwa kusema hizo ni kazi za ajabu za mwenyezi mungu
 
Quran imesema mwanadamu anaumbwa kwa fluid inayotokea kwenye maeneo kati ya mbavu na uti wa mgongo.

Mkuu hapa kuwa muungwana na kukubali kwamba quran imedanganya. Huo ndio ukomavu.

Baada ya hapo kimbilia kwa Yesu Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhambi, uokolewe na kuupata uzima wa milele.
Hapana Mkuu, Siwezi fanya hivyo kwa maana wewe hujaelewa aya Mkuu nami sitajifanya sijaelewa sababu tu wewe hujaelewa. Nitakupa link ya Dr. Zakir Naik akijibu swali hili
Video ina dakika 3 tu.
 
Uzi umehamia kwa Yesu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]wabongo ni watu wasioweza tatua changamoto bali huzihamisha
 
Mwanzo nilidhani uko ‘objective’ lakini kwa madai haya ninagundua hapana, upo kishabiki.
Unaweza kuleta mada kwenye maeneo utakayoona yana makosa tutakujibu.

Ila hapa nikupe briefing muhimu. Kwenye biblia huwezi kukuta sehemu yoyote iliyoandikwa, "Bwana Mungu akasema..." ambayo itakuwa na chembe ya mashaka.

Kuna maeneo ambayo unakuta mtu anashupalia kwamfano idadi ya vyombo vinavyotajwa wakati ni clear kabisa hizo zilikuwa ni narratives za matukio ya kihistoria ya taifa la Israel.

Kuna maeneo kwenye injili ambapo uwasilishaji umekuwa na perspectives tofauti watu wanasema ni contradiction ambapo ukiangalia kwa karibu hamna contradiction yoyote.

Ndani ya biblia kuna maneno yaliyotamkwa directly na Mungu, yapo ya wanadamu, ya shetani, ya mapepo nk lakini ujumbe collective wa biblia umesimama thabiti ukiwa ni mmoja tu nao ni uumbaji, kuingia kwa dhambi, mpango wa ukombozi na uzima wa milele.
 
Soma mwanzo 1:26 uje uulize tena swali lako
Mimi nauliza sasa Kwa nini Qur'an inakataa shirki then inakuja kuisapot tena hapa? unanirudisha tena kwenye biblia shida ni wale wanatutesa ooh wakristo mnakufuru mungu hashirikian na mtu sasa je hapo kwenye hiyo haya mungu anashirikiana na nan huyo?
 
Marko 10:19 inazungumzia kuhusu amri na yule bwana alieambiwa kua auze vitu vyake vyote hapo inasisitiza umuhimu na ulazima wa kufuata amri huyo ni yesu mwenyewe hatimae anawaambia wanafunzi wake kua ni ngumu mno kwa alie na mali kuuona ufalme wa Mungu
Sasa wewe unapata ujasiri gani uone ukia amin tu unaenda peponi bila kufuata amri we uoni unapingana na maandiko au maneno yake mwenyewe Yesu
Nimekuandikia kuwa ukiwa ndani ya Kristo unapata nguvu ya kutimiza sheria yote. Kwahiyo ukiwa ndani ya Kristo unayafanya maagizo yote kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.
 
Sisi kukubali miujiza si geni ila nikuulize wewe unaeikataa miujiza wakati yesu mwenyewe hakuja kwa hali ya ki biology ujue uhalisia sahihi na hiyo biolojia yako ya research ya miaka mia ndio jibu linatoka
Wapi nimekataa muujiza?
 
Unaweza kuleta mada kwenye maeneo utakayoona yana makosa tutakujibu.
Kiukweli siko interested kuanzisha mada hii kwa sasa.
Ila hapa nikupe briefing muhimu. Kwenye biblia huwezi kukuta sehemu yoyote iliyoandikwa, "Bwana Mungu akasema..." ambayo itakuwa na chembe ya mashaka.
Mbona waweka sharti? Kwani si biblia yote ni neno la Mungu? Au kuna maneno ya Mungu na ya Waandishi?

Ila wale waandishi si walikuwa inspired na Mungu ?
(Si lazima unijibu mkuu)
Kuna maeneo ambayo unakuta mtu anashupalia kwamfano idadi ya vyombo vinavyotajwa wakati ni clear kabisa hizo zilikuwa ni narratives za matukio ya kihistoria ya taifa la Israel.
Kwahiyo Mungu hakuwainspire Kuandika?
Au wamaanidha kuwa penye mikanganyiko basi hapo Mungu hakuhusika? Sijakuelewa mkuu

Kuna maeneo kwenye injili ambapo uwasilishaji umekuwa na perspectives tofauti watu wanasema ni contradiction ambapo ukiangalia kwa karibu hamna contradiction yoyote.
Kama kweli wewe ni mtu ‘Objective’ katu usingeandika madai haya kuhusu Biblia.
Ndani ya biblia kuna maneno yaliyotamkwa directly na Mungu, yapo ya wanadamu, ya shetani, ya mapepo nk lakini ujumbe collective wa biblia umesimama thabiti ukiwa ni mmoja tu nao ni uumbaji, kuingia kwa dhambi, mpango wa ukombozi na uzima wa milele.
Mpaka shetani katia maneno yake kwenye kitabu kitakatifu?

Nifafanulie mkuu hii point sijaielewa vyema.

Au kabla ya yote unazungumzia biblia gani, maana hapa ninazo nyingi sijui nianze fungua ipi
 
Nani aliekwambia utaenda mbiguni mji wa yerusalem utashushwa toka mbinguni kuletwa duniani Pepo itashushwa hapahapa na jehanam itashushwa hapahapa wewe wala mim hakuna mwenye hadhi ya kukaa mbinguni huko ni patakatifu sheikh, na tutazaa tutapewa miili mipyaa soma ufunuo wa yohana,revelation afu njoo na uongo mwingine
Kwanza umekosea kwasababu kutakuwa na mbingu mpya na nchi mpya na sio dunia hii hii. Tutakaa pamoja na Mungu katika nchi mpya.
 
Mimi nauliza sasa Kwa nini Qur'an inakataa shirki then inakuja kuisapot tena hapa? unanirudisha tena kwenye biblia shida ni wale wanatutesa ooh wakristo mnakufuru mungu hashirikian na mtu sasa je hapo kwenye hiyo haya mungu anashirikiana na nan huyo?
Ujafahamu kuhusu shirk sio kushirikian bali kumuabudia asiye kuwa yeye pia kuona utendaji wake ulio mkuu kuna mtu au kiumbe mwengine anaweza kufanya mithili yake au zaidi yake kushirikiana ni kufanya jambo kwa ushirikiano na mtu kitu fulani
 
Uzi umehamia kwa Yesu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]wabongo ni watu wasioweza tatua changamoto bali huzihamisha
Badala ya kujibu hoja dhidi ya quran wanaamua kusema mbona hata biblia ina makosa!! Tatizo hawawezi kuonesha kosa lenyewe kwenye biblia.
 
Mbona hushangai kuwa Qur'an inatabiri kuwa waliokufa watafufuliwa me naamini kama hujawahi kuona bikra akizaa bila kumjua mwanaume pia hujawahi kuona mtu akifufuliwa na Kwa jibu lolote utakalonipa usitegemee majibu yangu mengine maana nahitimisha Kwa kusema hizo ni kazi za ajabu za mwenyezi mungu
Hata Biblia inaamini katika ufufuo.
 
Kwanza umekosea kwasababu kutakuwa na mbingu mpya na nchi mpya na sio dunia hii hii. Tutakaa pamoja na Mungu katika nchi mpya.
kila kitu ni hapahapa upya wake ni kwamba itafanyiwa utakaso yaani kila takataka itatolewa itasafishwa haswaa Kwa mujibu wa vitabu vya dini
 
Back
Top Bottom