Wanasheria na Wataalamu wa Miliki (mali) Njooni mnipe ushauri Kuhusu hii Kampuni yangu na Warithi wangu.

Mara unasema wanasaidianaga kisela,mara unasema Tena hawajuani nawala hawataki kujuwana..nilitaka kujifunza kitu kutoka kwako..ila nimekuona chenga tu...
 
Fikiria pia wanaweza kufa watoto, au mama zao kabla yako. Andika usia wa kugawa mali kwa kila mmoja. Usiache kubainisha ukifa unazikwa wapi, na nani... hatutaki vurugu la kugombea maiti mtaani kwetu. Na kama hutakufa mapema ukizeeka utatunzwa na nani.. la sivyo utazeeka vibaya na mali zako hazitasimama zikusaidie wakati huo. Na watu kama ninyi huwa hamfi mapema ili mdhalilike na kupokea adhabu zenu hapa hapa duniani.
 
Wamiliki wa kampuni wawe watoto wako na wewe mwenyewe full stop. Wape shsre zao ns amdika wosia ukifa share wagawiwe watoto. Kila kitu weka kwa kampuni. Watoto ndio watatunza mama zao jinsi watakavyo.
 
hapo no.3 huyo msichana ndio atakuwa mke kwa kuzuia huo moto uliopendekeza, lazima atahakikisha anazaa
 
1. Hakuna mwanamke anaweza kuendeleza ndoto za mwanaume hii ni ya kiasili, kimsingi mtoto wako ndo anaweza endeleza ndoto za baba yake angalia matajiri wengi hata wahindi mfumo ni mtoto anakabidhiwa mali kuziendeleza mfano Mo Dewji yeye ndo amekabidhiwa kampuni za METL na anaziendeleza ndugu zake wale wote ni wafanyakazi wake
2. Kuhusu kukatamoto wakati huu au wakaribuni hilo lipo nje ya uwezo wake kwaio halina namna
3. Mke inaonekana umempa nafasi kubwa wakati nyakati zinabadilika, usisahau naturenya wanawake ni kuweka vitu moyoni na kutosahau wakati huu unamhitaji yeye atakua ameshajitenga na watoto wameshachukua upande na kuaminishwa mabaya yako(siku zote ukiwa na mzigo kila kitu kama mbele)
4. Hili limejibiwa na point ya hapo juu
 
Kwa usalama wa mali zako toa hao mama zao wape shares watoto wako tuu. Kuweka mali zako zote kwenye kampuni in way ziko mikononi mwa wanahisa amboa ndio hao wamama na wao kama wanahisa wana uhuru wa kugawa hisa zao kwa yeyote so mali yako haiko salama kivilee.
 

Mtoto chini ya miaka 18 anaendelezaje ndoto za Baba yake?

Sio kweli kwamba wanawake hawawezi kufanya hivyo. Huo ni mtazamo wa kitamaduni usio na ushahidi wa kisayansi. Ni Mapokeo.
Haina tofauti na waliosema mwanamke hawezi kuwa Daktari, rubani n.k.

Kwa kijana wa sasa msomi hawezi fikiri kwa namna hii.
2. Kuhusu kukatamoto wakati huu au wakaribuni hilo lipo nje ya uwezo wake kwaio halina namna
Ni kweli. Na ndilo linampa Hofu.
Ndio maana kuna Wosia


Mke ananafasi kubwa Sana kama vile mume. Huwezi zungumzia mwanaume, familia na kizazi Bora bila kumzungumzia Mke Bora.

Mwanaume hata uwe Bora vipi kama huna mke Bora hatua zako ni kama mbio za sakafuni
4. Hili limejibiwa na point ya hapo juu

Kwa ujumla, jamaa atafute tuu pesa kwaajili yake, kuhusu muendelezo wa utajiri hiyo ni ngumu Sana kama hakuna Familia.

Na hapo ndipo Waarabu wanapogeuka tishio kwa Jamii za wazungu ambao wamepuyanga kwenye kipengele cha Familia
 
1. Huko juu nimesema kwamba akishaangalia mtoto yupi anafaa kuendeleza mali atachagua..tupe uthibitisho wa kisayansi wa mwanamke kuendeleza mali za mumewe...maswala ya rubani na udaktari hayo hayana uhusika maana hizo sio biashara maana ni profession hazirithishwi zinapotea mtu asipo kuwepo

2. Nafasi ya mwanamke na umuhimu wake inategemea na mtazamo ulionao kama umeshaoa lazima uone kwamba ana umuhimu ila kama hujaoa kama mleta mada hawezi ona umuhimu huo maana ndoa nyingi zimeangamiza na kudidimiza ndoto za watu 1 wakorintho 7: 26-29 utapata majibu

3. Maadamu mlera mada ametaka kupewa ushauri wa kuendeleza mali pasi na kua na mketubakie tu humo humo tusiingize maswala asiyoyataka

4. Sasa waarabu kua tishio ni sababu wanaoa mke zaidi ya mmoja na kua na watoto wengi pia
 
Aliyekuambia udaktari sio biashara ni Nani? Na aliyekuambia haurithishwi ni Nani?

Wapo wanawake wengi tuu ambao wameendeleza na kuendeleza Mali za waume zao.

Nafasi ya Mwanamke haitegemei maoni au mtazamo wa MTU. Ni kama nafasi ya mwanaume ndani ya Jamii au maisha ya mtu.
Mwanamke ni key figure ambaye huwezi kumkwepa kama ilivyo kwa mwanaume. Tunasema ni kama Maji. Umuhimu wake uko Bila kutegemea maoni ya mtu.


3. Maadamu mlera mada ametaka kupewa ushauri wa kuendeleza mali pasi na kua na mketubakie tu humo humo tusiingize maswala asiyoyataka

Hapa upo sawa.
Hapa tulikuwa tunatanua mjadala
4. Sasa waarabu kua tishio ni sababu wanaoa mke zaidi ya mmoja na kua na watoto wengi pia
Waarabu licha ya kuwa na watoto wengi lakini hawafikii Wachina na Wahindi.

Ishu kubwa ambayo ni tishio kwa wazungu ni mfumo wa kiarabu ambao unaifanya Jamii zao kuwa na nguvu kuanzia kwenye Familia
 
Kwanza hongera kufunguka, na hii itawasaidia wengi.
Watanzania wamezoea will ya kumrithisha mke na watoto. Ukifa watoto hawawezi kuendesha kampuni au biashara zinakufa!, kwa influence ya mama zao, wataishia kugombana kugombea mali!.

Badala ya kuandika will kurithithisha watoto, mali zako zote ziandike kwenye kampuni, kisha rithisha trust , hiyo trust itaendesha kampuni zako na watoto wako wote watakuwa well taken care off ndivo wanavyofanya matajiri wenye akili!.

Ila kwa sasa wakati bado una uwezo, kwanza waandalie kila mtoto land, ukiweza kuwajengea nyumba wajengee, na badala ya kuwawekea watoto fedha bank, nunua bonds na kuwaandika kama warithi.

Mimi mwenyewe ninayekushauri nina watoto 9!, Changamoto za kupata mtoto mchanga ukiwa umri wa kustaafu, unakuwa ni Baba Babu. Dawa ni kujipanga kabla, vinginevyo ni kubebesha watu mizigo yako
P
 
Huyu ndiye raisi wetu wa kataa ndoa, mimi ni katibu mwenezi wa kataa ndoa πŸ˜‚πŸ¦…
 

Nakaziaa kwenye Mkee Avute Jiko
Hivyo anza kuwaza kuhusu future yako
 
Asante sanaa boss UMETISHA.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…