PostGE2025 Wanasheria watinga ICC na kufungua kesi dhidi ya Rais Samia na wakuu wa Vyombo vya Usalama Tanzania

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hapa chura kiziwi hana pa kuponyokea. Lazima akanyee debe. Atafungwa jela moja na Joseph Kony na wauaji wengine wa aina yake.
 
Hahahaha mbavu zangu jamani hiyo haiwezi saidia kitu!! Watu wameuawa wengi tena kikatili dunia haiwezi nyamaza
Kuna vinchi huko vimeanza kujitoa kwa visingizio hivi na vile.

Al Bashir alishitakiwa ila kuna vinchi ikiwemo South Africa ikagoma kumkamata alipokwenda kwao. List ya watuhumiwa ikiwa ndefu tunaenda kuwa "Pariah State". Hawa wamekataliwa hadi na majirani.

Tufunge mikanda, mbele ni kugumu sana.
 
Tutashinikisha waende hapa hakuna ukaidi hii ya kwao ni tofauti na sudani make kule ilikuwa makundi ya kikabila na vikosi vya serikali hapa kwetu wameua wenyewe,sometimes unawaza hivi hawa wakwetu waliwaza nini kuua watu vile kiholela tena hadharanj ina maana huko majeshini hamna msomi anayejua sheria za kimataifa zinakataza kupiga mtu risasi asiye nq sulaha??? Angalia kama ile picha ya mwanamke wa arusha aliyekuwa anakimbia watajiteteaje sasa
 
Ila ccm na machawa wanafiki sanaa wamemsusa mama kama sio yule waliekua wanampamba kila siku sijui mitano tano sijui mama hana den na nk now kimyaaaa yuko pekee yakee
Wote wanaogopa, hakuna anayekubali kutumika sasa hivi maana tumefika zama za life and death.
 
Sijui walifikiria nini. Kiburi kikizidi kinakupa upofu. Unakuwa hauoni, hausikii wala haufikiri kwa usahihi.
 
Acha kutisha watu,Mimi Niko tayari kutoa ushahidi,tunaishi mara Moja tu
 
Huwa nahisi mama anahujumiwa na yeye ni kama hajui hilo, hivi kweli askari wako waue watu kivile, halafu upige kimya, kwenye Ulimwengu wa sasa, utatoboa kweli???
Mama hotuba ya kwanza tu, angedenounce hadharani mauaji, watu wakaswekwa ndani, kesi zikafunguliwa, watu wakavuliwa vyeo, tume huru ikaundwa etc.angeruka huu mtego.Sasa wahuni wamemtupia zigo tayari.Na zaidi ni kipindi chake cha mwisho, mpaka kesi inashika speed atakuwa karibu anatoka, urais unaishi..watu wanakula naye sahani moja...
Akili za kuambiwa changanya na zako, yaani watu wauwe kisa wanakupenda, uongo wa wapi..mtego huo...na wamemsisha mama wa watu
 
Ule uzi wa humu jamii forums uliokuwa unakusanya picha na video za mauani uko wapi?? Naombeni link.

Ule unaweza kutumika kuchota ushahidi
 
Kabisa, naunga mkono hoja
 
Media za Tanzania zitaripoti?

JamiiForums jukwaa huru linafanya kazi nzuri

 
Hivi karibuni itasikika sana. Swali langu ni - Je, nini itakuwa hatma ya kesi hii?

Samia na wenzie wajitayarishe kwenda kujitetea wao binafsi kwa ushiriki wao katika mauaji ya raia.

AG Hamza Johari awaambie Samia na wenzie ukweli wa jinsi mambo yalivyo magumu, hakuna namna ya kujiokoa wasifike The Hague Uholanzi kujitetea kuwa hawana hatia.

Kesi hizi za the Hague ICC Huwa zinarushwa mubashara live tena hata kwa KiSwahili watapewa wakalimani na wasikilizaji wanaweza kufuatilia mwenendo live / mubashara wa kesi hii ya kihistoria,


 
Kesi hizi za the Hague ICC Huwa zinarushwa mubashara live tena hata kwa KiSwahili watapewa wakalimani na wasikilizaji wanaweza kufuatilia mwenendo live / mubashara wa kesi hii ya kihistoria,

TOKA MAKTABA :

ICC The Hague Uholanzi

Jenerali Bosco Ntaganda kesi iliyooneshwa mubashara kwa lugha kadhaa ikiwemo kiSwahili kama video hii ya mahakama ya ICC ili umma uweze kufuatilia mubashara kuona haki ikitendeka


View: https://m.youtube.com/watch?v=v7YAk0V01U4
 

Amiri jeshi mkuu aliyekuwa kila wakati anakumbushia yeye ndiyo mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama Samia Suluhu Hassan
 
Vipi utaratibu wa kumfikisha mahakamani Samia, Wambura, na wengine wakingoma kuitikia wito wa Mahakama, Je mahakama ya ICC ina njia zipi na zipi za kuweza kuwafikisha?

Tayari Samia Suluhu Hassan anaogopa hata kwenda Zambia, Angola, South Africa anamtuma kaimu rais Emmanuel John Nchimbi

ZIARA ZA KAIMU RAIS NCHIMBI, SAMIA AKIJITAYARISHA KWENDA ICC
19 November 2025
Lusaka, Zambia


Makamu wa Rais Emmanuel Nchimbi awasili Zambia

Kushiriki utiaji saini wa makubaliano ya ufufuaji wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania – Zambia (TAZARA)

Makamu wa Rais wa Tanzania, John Nchimbi, amewasili nchini Zambia kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.​

Vyombo vya habari vinaripoti kuwa Dk Emmanuel Nchimbi aliwasili kupitia Uwanja whttps://m.youtube.com/shorts/MQOeHmaK_6ca Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, kwa ndege ya Air Tanzania.

Alipokelewa na Waziri wa Afya, Elijah Muchima, sambamba na Meya wa Lusaka Chilando Chitangala, Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Ltuteni Jenerali Matthew Mkingule na viongozi wengine waandamizi wa serikali ya Zambia na Tanzania.

Dk Nchimbi anatarajiwa kushiriki utiaji saini wa makubaliano ya ufufuaji wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania – Zambia (TAZARA) unaotarajiwa kufanyika kesho mjini Lusaka.

Anatarajiwa kurejea Tanzania mara tu ratiba yake ya kazi itakapokamilika.

View: https://m.youtube.com/watch?v=TN6y0xGp8d8




24 November 2025
Luanda, Angola

Dr. Emmanuel John Nchimbi awasili Angola kwa kikao cha taasisi mbili muhimu duniani kikao cha EU Umoja wa Ulaya na Umoja wa AFRIKA AU


View: https://m.youtube.com/shorts/MQOeHmaK_6c




 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…