Baadhi ya wanawake hamna shukrani na mnapenda kuishi maisha ya watu wengine , Unatakiwa kushukuru Mungu hata kwa maisha mnayoyaishi, kuna wanaume wametelekeza familia zao na hawajawahi kurudi nyuma kujua familia inaendeleaje , unachopaswa ni kumshauri mumeo kwa hekima, mpe ushauri kwa utulivu! Kama hatafanya wala usilazimishe, anza wewe kumuonesha hiyo njia na yeye ataona aibu kisha ataungana na wewe ! Mwisho wanawake muache tamaa ya kutamani mambo yaliyo nje ya uwezo wenu au nje ya uwezo wa mume wako ! Mtafanya wenza wenu wafanye mambo yasiyompendeza Mungu wala jamii kisa tu kuwaridhisha nyie.