BANDOKITITA
JF-Expert Member
- Oct 4, 2022
- 1,484
- 2,852
Ulikuwa na hoja. Ulitakiwa uje km kuomba ushauri juu ya huyo mumeo. Siyo ku-generalize badala ya ku-specify wa kwako pekee. Hata hivyo inaonekana wewe mwenyewe una madhaifu maan wewe ndiyo mshauri wake namba moja na mwenye kumbadilisha kwa sababu wewe ndiye unamfaham vyema (unalala naye shuka moja, unampikia, unamfulia, unampa maji ya kuoga nk) lakini umeshindwa kutueleza hadi sasa wewe mwenyewe binafisi umefanya jitihada gani kumbadilisha tabia zake.
Pia kumbuka ktk ndoa maendeleo hayaletwi na mwanaume tu, ulitakiwa utuambie wewe binafisi umefanya juhudi kadhaa za kuwaletea maendeleo lakini mwenzio pesa zake anapeka kwa mahawala(kwa mjibu wako). Inashangaza unaposema hao watoto anaokuzalisha akifa utawapeleka wapi. Kwa nini usiseme siku wewe ukifa hao watoto anaokuzalisha atawapeleka wapi. Kwa nini umfikirie mwenzio kufa kwanza kabla yako. Hii inaonesha wewe ni mbinafisi na umekuwa unamuombea mabaya mumeo. Wewe ni miongoni mwa wanawake ambao mkijengewa nyumba na kuwa na vipesa tu vya kubadilisha mboga unaanza kumuazia jinsi ya kumuondoa mumeo Duniani ili ubaki na urithi. Pengine mumeo keshalibaini hili ndiyo maan hanunui hata kiwanja kukukomoa.
Pole sn, toa kibanzi kwenye jicho lako kwanza kabla ya kumcheka mwenye chongo. Maendeleo yanaletwa na wote siyo MUME tu. Siyo kila siku wewe unakula vizuri nyumbani kwako na unaletewa zawadi kemkem na mumeo na hukatai leo unakuja kulia eti hamna maendeleo. Km nasema uongo twambie lini uliletewa zawadi km nguo, mkoba, kijora, au viatu ukakataa ukamwambia avirudishe hizo pesa mzitunze ili mkusanye kidogo kidogo kwa ajili ya kununua uwanja. Au vipi akikwambia akutoe out na huko mkatumia lakini moja utakataa?
Acha lawama, mwanamke bora (wife material) siyo kuwa na sura za Kisudan au Kinyarwanda au kuwa na matako makubwa km kifusi cha barabarani, mwanamke bora ni mwenye akili za kuwaza, kuamua, na kutenda kwa usahihi. We mbadilishe mumeo mwenyewe akikushinda waachie hao mahawala unaosema wakusaidie kumbadilisha.
Nimemaliza: Bandokitita.