Wanaume gani watakubali kuingia na wanawake wao kwenye chumba cha kujifungulia?

Wanaume gani watakubali kuingia na wanawake wao kwenye chumba cha kujifungulia?

howardlite

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2016
Posts
242
Reaction score
392
Nimemsikia raisi wetu SSH jana akiwa hospital ya CCBRT akisema kuna vyumba ambavyo vitatumika wakati wa mke akiwa kwenye kujifungua mume awe hapo akimtia moyo,akiona shughuli wanawake wanapitia😀😀 ili wapange uzazi,atoe mahitaji na vinavyofanana na hivyo.

Mimi sipingi ni jambo zuri lakini tuwe makini wajameni, haya mambo yana athari gani chanya na hasi.
Nimewahi kuwa karibu na labour siku nilimpeleka mke wa rafikiyangu hospital moja Mwanza kujifungua nikasikia kinachoendelea kule ndani, mwingine alikuwa anatukana mfululizo, anataja jina la mwanamme na kushushia na tusi, mara sikupi tena, nimekoma mimi, mara nesi nataka kunya. Jamani jamani leo ndio mwanaume uwe hapo pembeni na mke awe wale wanachukia mwanaume wake hataki hata kumuona kipindi cha ujauzito si itakuwa Ukraine ndogo?

Lakini kuna point nyingine nimewahi kuisikia kwenye dini ya ndugu zangu kuwa mume hupaswi kuutazama utupu wa mke wako😀😀. Sasa tufikiri kweli mume uko hapo unaona lile tukio mwanzo mwisho kweli mh?
Nauliza kwa ambao wamewahi kuwa na wake zao kwa kipindi hicho mpaka wanajifungua,ivi baada ya hapo inatokea nini? Kumbukumbu inakuwa vizuri kabisa na hamna shida? Wanawake wa JF mnaonaje hili lilivyokaa?

Naamini ni kipindi ambacho wanaume tunapaswa sana kuombea wake kipindi choche cha ujauzito kwa kuzidi sana kipindi hiki, kuwatia moyo, kuwajali na kuonyesha upendo mara dufu na staha ya hali ya juu.

Lakini pale ndani kuwepo kwakweli usisikie sio mchezo. Mtakaokuwa mnaenda kila la kheri lakini mkumbuke kuleta mrejesho pia na wanawake mlete ushauri mapema tujue la kufanya kwa hekima.
 
Nimemsikia raisi wetu SSH jana akiwa hospital ya CCBRT akisema kuna vyumba ambavyo vitatumika wakati wa mke akiwa kwenye kujifungua mume awe hapo akimtia moyo,akiona shughuli wanawake wanapitia[emoji3][emoji3] ili wapange
Sishauri wanaume waingie labour room mke wake anapojifungua. Inabidi muwe mnawaombea zaidi mke na mtoto muda huo, maana ni kipindi kigumu sana muda ule.

Pia majukumu yenu myafanye kwa ufanisi sana hasa malezi ya watoto na familia kwa ujumla maana nyie ni vichwa vya familia.
 
Nimemsikia raisi wetu SSH jana akiwa hospital ya CCBRT akisema kuna vyumba ambavyo vitatumika wakati wa mke akiwa kwenye kujifungua mume awe hapo akimtia moyo,akiona shughuli wanawake wanapitia😀😀 ili wapange uzazi,atoe
Kutiana moyo sio lazima uwe naye karibu wakati wa kujifungua, vitu vingine tusiige wazungu jamani, hii inaweza kuwa na athari kubwa sana kiakili, haina tofauti na kumwangalia mwanamke huko akiwa kwenye siku zake, hii inaweza kukuvuruga sana ukapoteza muelekeo. Vitu vingine sisi wanaume hatupaswi kutizama isipokuwa tu vinapokuwa kwenye hali nzuri......
 
Mimi ni wa kwanza, nitaingia nikiipata hiyo nafasi

Wakunga wa kiume wanazalisha na hawaogopi, iweje wewe mwanaume uogope.

Vijijini mbona wanaume huitwa pindi mke anapotaka kujifungua ili wakatoe msaada, mara nyingine unakuta mwanaume pekee anamsaidia mke wake kujifungua japo inaweza kuwa ni sababu ya kukosa msaada kutoka kwa wengine.

Hii kitu kama vipi itungiwe sheria iwe ni lazima tuwe tunawashuhudia wake zetu wakiwa wanajifungua[emoji1751][emoji1751][emoji1751][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Ni jambo zuri sana kuona bao ulilomwaga linatokaje maana linavyotoka linaonyesha maisha yake yatakavyokuwa kwa ujumla. Maana wengine wanatoka miguu kwanza, wengine wanatoka kichwa kwanza, wengine wanatoa mkono kwanza, wengine wanatoka matako kwanza......
Kila mtu apambane na hali yake sitaki maswali.
 
Sasa tufikiri kweli mume uko hapo unaona lile tukio mwanzo mwisho kweli mh?

Jana niliulizwa swali hili na mke mtarajiwa, nikamjibu kuwa SITAWEZA.

Akauliza “Kwanini?” Nikamueleza kuwa ‘Nachelea nikikuona labor nitapoteza hamu ya kushiriki tendo nawe’.

Kimsingi ninaamini kuwa utamu wa penzi (kujamiiana) unaenda sawa na saikolojia, yani vile unavyomchukulia mtu unaeshiriki nae. Na Penzi huwa tamu zaidi pale unapokuwa hujui hasa cha kutegemea (being not familiar, not knowing it to the T). Hii inaeleweka vyema kabisa wakati wa penzi jipya.

Mbali na kuwa nitakuwa namjua mke ila bado sitakuwa naijua hasa tabia ya Uke wake mpaka nitakapoingia huko ‘Labor’.

Binafsi sitaingia kwa kuchelea nitapoteza hamu na mke wangu jambo litaloweza hatarisha ndoa yangu na ustawi wa mtoto wetu.
 
Binafsi KUINGIA huko na kushuhudia Live hilo haina tatizo,,,,BUT kuna ulazima gani wa kwenda kushuhudia....??...Nini hasa kilichokosekana ambacho Suluhu lake ni kwenda Labor kuangalia Mkeo anapojifungua....??tutabadilisha nini haswa...

WANAUME siku hizi tunapoteza direction kabisa,,, tunaweka vipaumbele kwenye mambo yasiyokuwa na Msingi wowote,,,,Mwanaume utashuhudia mkeo akijifungua pale ambapo Mazingira yatataka iwe hivyo(Emergency),,,,na sio kuwa manipulated kama hivi KWA HISANI YA WATU WA MAREKANI....

Nina mengi ila acha niishie hapa,

MWANAUME,,, Yajue ya kuzingatia....
Be a Man.
 
Inategemeana sana na mahusiano yenu na akili zenu nyie wawili.

Kama unaona ni sawa na mkeo anaona atapata morali zaidi haya nendeni wote, lakini kama mmoja wenu hataki hicho kitu bac achana nacho hataka kama ww unakitaka zaidi.
 
Back
Top Bottom