Pengine majibu ya swali hili yanaweza kuwavutia wanaume waliyo single kuamua kuoa na hivyo kupunguza tatizo la wadada wanaotaka kuolewa kukosa waume.
Wanaume walio single ukiwauliza wanasema:
1- Utelezi unapatikana kwa wingi mtaani.
2-Wanaweza wazalisha wadada kisha wakatunza mtoto/watoto
3-Kupika siyo ishu tena, siku hizi kuna vifaa kibao vimerahisisha mapishi(e.g rice cooker, electric boiler, n.k)
4- Kufua siyo tatizo kuna mashine za kuoshea.
5-Usafi wa nyumba kuna makampuni siku hizi ukitoa buku 30 nyumba inakuwa safi mwezi mzima
On top of that kuna mahusi gals na mahausi boyz wanaweza wakaajiriwa kufanya kazi na 2, 3, 4 na 5.
Ndiyo sababu wanauliza waoe kutafuta nn?
Hebu fungukeni faida kuntu mnayopata kwenye ndoa. Ni ipi?
FAIDA ZA NDOA
1. KUPATA MSAADA KUTOKA KWA MKE WAKO/MUME WAKO PINDI UNAPOPATWA NA MAGONJWA MAKUBWA NA MAZITO YA MWILI WOTE KWA UJUMLA HUSUSANI SEHEMU ZA SIRI.
-Hapa ieleweke kuwa kama ni mwanaume na ikatokea umepatwa na magonjwa mazito na makubwa kama tezi dume, unaharisha, umepata kilema cha mikono au miguu. Hapo mtu pekee wa kukuogesha na kutoa kinyesi chako kitandani na kusafisha kitanda wakati wewe hujitambui ni mke wako tu na hakuna namna, tena itokee huyo Mke wako uliishi nae vizuri kwa kumjali possibility ya kukuhudumia vizuri kwa asilimia 90% hadi 99%.
Hapo kumbuka hata dada wa kazi kuna vitu atashindwa tu kukuchamba chamba na kukutawadha. Alafu itokee umelazwa hospitalini tena kwa muda mrefu sana hata mwaka au miaka miwili, mtu pekee ambaye kuna uwezekano wa kuwa anakuja kukuona hadi mwisho ni Mkeo au Mumeo, Ndugu wa kawaida wanaweza waka Give up.
Nafahamu hii point namba moja kuna vijana wa hovyo watakaoipinga kwa kusema mke au mume huwa wanabadilika. Sasa endelea kuamini huo upumbavu kaa usioe, alafu siku upo Geto kwako unaumwa ukose kuhudumiwa kwa dhati, sijui atakuja Mama yako Mzazi kuja kukomaa na hilo rungu lako na uchi kwa ujumla kukusafisha.
2. WATEGEMEZI WENU KUENDELEA KUWA NA FURAHA ENDAPO MWANANDOA MMOJAWAPO ATAPATWA NA MATATIZO.
Wategemezi wa wanandoa ninaowazungumzia hapa ni WATOTO mliozaa.
Chukulia Baba umepata ajali hadi ikapelekea umelazwa hospitali kwa muda mrefu na hauongei wala husikii. Sasa hapa Mke wako pekee ndio anayetakiwa kujua kila kitu tena inapaswa umuandae hata kabla ya matatizo yako kukupata ikiwemo Password ya Bank na vyanzo vingine vya Mapato yako.
Kwa kufanya hivyo basi wakati wewe umelazwa, huku mkeo ataendelea kulipia watoto ada kama kawaida ili wasisimame shule, kama una madeni atayapunguza, kama kodi ataendelea kulipia.
Kwahiyo Watoto atleast wataendelea kuwa na furaha kidogo ingawa Baba au Mama ana matatizo hospitalini. N:B. Wategemezi wengine ni wazazi wenu.
Sasa ukiwa hujaoa, taarifa zako nyingi zinakuwa ni siri yako, siku ukifa unafaidisha Bank na watu wengine. Alafu wanao watakufa kwa umaskini unaonuka
3. KUTOKUINGIA KWENYE KESI ZA JINAI AMBAZO SI ZA LAZIMA
Chukulia nyinyi ni wanandoa usiku mmelala na kuamka asubuhi mmoja amefariki kwa bahati mbaya labda kwa pressure, mawazo au ugonjwa wa ndani kwa ndani wa mda mrefu. Hapo kwa kawaida mwanandoa mmoja aliyebaki atakuwa hana kesi otherwise awe kafanya uhalifu kweli na majirani na ndugu wawe wanajua kuwa ndoa hiyo ina hitilafu na maugomvi. Lakin kama ni kifo cha kawaida kesi hakuna hapo
Sasa wewe Mwamba chukua Demu mpeleke Guest House au Ghetto, kumbe ana stress zake siku hiyo kazimia tu au kafa kabisa ukizingatia hujaoa hapo ndipo utakapojua Segerea ni Gereza au Nyumba ya kulala wageni.
Tena sikuhizi wanaume mnachukua mademu na kukaa nao magetoni bila wazazi kujua, siku kikiumana ndio utajua kwanini MANDONGA MTU KAZI ana maneno mengi kuliko vitendo.
Na wewe Demu siku unaenda kwa mwamba Ghetto, kumbe siku hiyo mwamba kanywa Mikonyagi, kapaka mkongo ili hiyo Mbususu unayompa aikomoe ukichanganya na weakness zingine za mwili, mapigo yake ya moyo yanaenda mbio mara anakuzimikia kifuani kwako, hapo ndio utajua kwanini Nyege huwa zinatoweka ghafla.
Faida za kuoa au kuolewa ni nyingi sana ila kwa leo acha niishie hapa.