Bwana acha mbwembwe haya makundi hata mkoani yapo, mwanza lilikuwepo linaitwa nyamirizo kahama lilikuwepo wanajiita sijui jeshi la nini.
Tena huko kote wanaishi wasukuma wakakamavu. Na wote hao walikuwa watoto wadogo tu wanatembea na visu, wembe, mapanga.
Mwaka 2009 nikiwa A level pale mwanza, kuna dogo shuleni kwetu sijui alikuwa kamchukua demu wa mojawao. Siku ya disco pale shule si wakatimba eti kunsaka huyo dogo.
Aisee, kipigo walichopewa na wanafunzi hawatokaa wasahau maisha yao yote.
Yani eti watu 18 wanataka kuteka shule ya boys watupu kuanzia form 1 mpaka 6.
Washukuru hakuna aliyeuawa waalim waliwaokoa
Umenikumbusha kauka camp, wazikuzi, manyirizu, wazabe..
2009 na tisa makundi mengi yalikuwa yamekufa..
Hii ilikuwa ni fassion kwa vijana ili uonekane hardcore na haikusika na wizi.
Haya yalikuwa sio makundi ya uporaji bali ilikuwa ni vikundi vya vijana wa
mtaa kama brother hood flani hivi na walikuwa wanatokea kwenye familia za mtaani hapo hapo
ili uwe hardcore ilikuwa lazima uwe na kundi,
asilimia kubwa walikuwa wanafunzi miaka hiyo shule ya msingi mtu anandevu na shule za kata zinachipuka sana
japo ilicombine wote hata wakishua wanaosoma private schools, miaka hiyo mtoto wa kiume kumpeleka shule
ya private ni mpaka utumie nguvu..
Karibia kila kijana wa mtaa alikuwa na kundi lake ndani ya mtaa kama si wewe basi kaka yako.
Vijana wa mtaa flani walikuwa hawezi kutoka mtaa flani kuja kuteka mtaa flani.
Ilikuwa kijana ukipita mtaa sio wako na hufahamiki na kundi hilo lazima uwe mpole na heshima.
Ila walikuwa wanaweza kutoka na kwenda kupigana na kundi flani tena kwa sababu wala hawakuhusika na wizi
japo ilikuwa kawaida mtu kuchomwa kisu ndani ya hayo makundi.
Miaka hiyo mwanafunzi wa shule flani akipigwa na mwanafunzi wa shule flani shule nzima inaenda kupigana...
Miaka hiyo mwanza mtoto akikushinda tabia unampeleka saqafa au taqwa, shule ambazo asubuhi fimbo zina
pelekwa na gari.
Nadhani hivi vitu vilichochewa sana na uhasama wa wana hiphop huko marekani kuwepo kwa makundi kama wutaang clan...