Bwana acha mbwembwe haya makundi hata mkoani yapo, mwanza lilikuwepo linaitwa nyamirizo kahama lilikuwepo wanajiita sijui jeshi la nini.
Tena huko kote wanaishi wasukuma wakakamavu. Na wote hao walikuwa watoto wadogo tu wanatembea na visu, wembe, mapanga.
Mwaka 2009 nikiwa A level pale mwanza, kuna dogo shuleni kwetu sijui alikuwa kamchukua demu wa mojawao. Siku ya disco pale shule si wakatimba eti kunsaka huyo dogo.
Aisee, kipigo walichopewa na wanafunzi hawatokaa wasahau maisha yao yote.
Yani eti watu 18 wanataka kuteka shule ya boys watupu kuanzia form 1 mpaka 6.
Washukuru hakuna aliyeuawa waalim waliwaokoa