Mimi sio mkazi wa Dar, ila natembelea Dar mara kws mara. Siandiki haya kwa kuwatetea vijana wa kiume wanaoshi Dar ila ku-deal na reality sio mihemko.
STYLE YA UHALIFU WAO NI AMBUSH WAKIWA KATIKA KUNDI KUBWA:
Kutokana na ushuhuda hawa wadogo wanakuwa katika kundi kubwa lenye vijana kuanzia 10 hadi 20. Wanakuja katika ambush ya kasi wakivamia nyumba hadi nyumba.
Kwa maana hapo tayari umeshawekwa mateka ukizungukwa na wajinga 10 hadi 20, wakiwa wamekuja kwa kushtukiza na silaha kama mapanga.
So, kwa mara ya mwisho hapo ulipo mkoani ulishawahi kuwa mhanga wa style hii ya uharifu? uliamka ukaanza kugombana na nao na kuwashinda wote.
UHALIFU WA NAMNA HII UNATOKEA GHAFLA THEN KUPOTEA KWA MUDA MREFU:
Hawa madogo wakishafanya haya matukio kwa style hii, haichukui hata wiki wanapotea hewani. So ni ngumu kuwa track hawa wajinga, mtaweka ulinzi shirikishi kwa mwezi au miezi mitatu then mtaanza kupwaya wenyewe. Sio kwa sababu nyie ni wajinga ila hio ni human nature, pamoja na polisi kuwa promise ulinzi mna hisi mtakuwa very safe na pia factors nyingine zitawabana kuwa sincere wakati wote
LIFESTYLE YA DAR SIO RAFIKI KWA USHIRIKIANO KATIKA ULINZI SHIRIKISHI
Watu wanarudi nyumbani saa nne au saa sita, mwanaume kachoka, wife anataka unyumba etc. Dar is the busiest town na the most tiring sio kama mikoani kwetu huku, Dar watu wanapigana na muda wakati wote.
Sawa utasema dar kuna watu wengi hawana mishe, sasa hao ndio wengi wao panyaroad. Sasa hauwezi ukamkamata out of suspicion kwamba ni kibaka labda mfukuze mtaa, whih is not simple.
JAMII YA MIKOANI SIO KAMA YA DAR:
Hapo ulipo wilayani mnafahamiana karibiana na kila mtu, ni rahisi kusimamia uhalifu.
Hapo mkoani kwako kuweka ulinzi shirikishi ni rahisi kutokana na kupata muda kwa kiasi kikubwa na uwepesi kufanya doria kutokana na miundombinu ya mitaa kuwa rafiki sio kama na temeke.
LASTLY:
So kabla mjawaita wanaume wa Dar ni mayai sana, fikiria factors nyingine za kimaisha na mji kiujumla.