We nae hujui nyamaza bwana u showing the height of ur ignorance here, nature ni mwanaume kutafta ale kwa jasho, mke azae kwa uchungu ni vile sahivi most of u mmekua wavivu ndo mana upo hapa kulialia njaa ungekua unaenenda na nature usingeandika vitu virahisi hivi pia kubali kukosolewa na kufundishika, huna haja ya kumwambia mtu hata mnyama anamshinda thats a point of weakness unalazimisha kushindana na kushindwa, baki kwenye hoja ya msingi acha maneno ya hovyo
Kwahiyo wewe ulicholewa kuwa kuzaa kwa uchungu huwa inaishia pale umeshamtoa mtoto katika tumbo lako la uzao then basi?!
Pale picha la kuzaa kwa uchungu ndipo linapoanzia. Utaanza kuwajibika kuwa mama kwa mtoto, mke kwa mwanaume anayetafuta kwa jasho ili apate faraja kupitia wewe na watoto wenu, lakini pia kuwa mkwe kwa wazazi ww huyo mwanaume na wifi kwa dada zake na shemeji kwa kaka na wadogo zake wa kiume.
Jambo la kisaikolojia kuhusu mwanamke wa ulimwengu wa sasa ni ile tabia ya kupenda kuhisi yeye ana privilege inayokuja na jinsia yake jambo ambalo huwa linawapotosha sana na miaka ya hivi karibuni limeanza kutumika vibaya kumrubuni mwanaume na kumtumia vibaya ili mwanamke aneemeke.
Haya manyanyaso ni matokeo ya kutosimamia kile kiapo cha kuzaa kwa uchungu. Kwasababu tazama mfano wewe hapa unasema huwezi nyeyekea mwanaume ina maana umetafsiri kuwa kunyenyekea ni utumwa kwa mwanamke kufanya. Mimi nitakuuliza swali la msingi je unaelewa maana ya neno kunyenyekea (submission)?
Maana unaweza sema ni kitu haukifanyi ila unakifanya kila uchao bila kujijua. Nitakupa mifano hai.
1. Unapokuwa na rafiki zako wakakushawishi muende club kula bata na hautaki ila wakakubembeleza hadi ukaenda bila ridhaa ila kwa ushawishi hiyo ni kusubmit (kuwa submissive),kwa kiswahili kunyenyekea amri ya rafiki zako. Amri ni amri aidha kuambiwa kwa sauti ya upole, au ya ukali zote ni amri na zinafuatiwa na utii as long as upo chini ya himaya ya anayekupa hiyo amri.
2. Konda anapokwambia sogea nyuma au fanya hiki ama kile pale unanyenyekea kwa kutekeleza amri anayokupa.
3. Mnapokuwa kitandani unageuzwa mikao mbali mbali na vyote unavyokubaliana ile yote inatwa ni kunyenyekea au submission.
4. Mtoto anapolia na unakwenda ukikimbia na kumtii amri ya wito kupitia kilio chake hiyo ni kunyenyekea.
5. Kazini kwako unavyoagizwa na kuambiwa ufanye hili na lile iwe kwa kupenda ama kutopenda unatekeleza amri hiyo ni kunyenyekea au submission.
Sasa sijaelewa why unatafasiri vibaya neno kunyenyekea as if ni neno lenye maana mbaya ya kikatili hadi lionekane ni baya kwako tu. Maana hata wanaume wanalifanya sana.
Hiyo unayosema mwanaume ataoe pesa kumhudumia mtoto ambaye ni damu yake pia ni submission na tena wanaume huenda mbali zaidi na kusubmit katika kulea watoto ambao si damu zao mliwabambikia au wamejitolea kulea.
Akikusikiliza hiyo pia ni submission kafanya yaani kunyenyekea. Tatizo mnatazama tone ya sauti ambayo wanaume sisi tunatumia mnasahau matendo yanayofanyika.
Sasa tazama unasema unyenyekee kisa laki mbili au laki tatu, hivi wewe unajua pesa inavyotafutwa kwa shida halafu wewe unasema mtu anayeitoa hiyo laki mbili kumpatia mtoto ambaye baadae hata akifanikiwa na kuwa na uwezo wewe mama mtu ndie una uhakika wa kupata benefits za kuhudumiwa baba mtu akatengwa, wewe unaidharau.
Ni vema wanawake mkajitathimini mnashindana na jambo gani. Muda mwingine huwa mnahisi wanaume wanavichaa ila ni ninyi ndio mnatengeneza mazingira ya hivi vichaa kumea vichwani mwao.
Kuna wanawake ukimpatia elfu 30 anashukuru kama amepewa milioni hadi unaona huyu ananifanyia maigizo ila hapana amefunzwa kwao kunyenyekea na kuheshimu jitihada za mwingine na hii ndio tafasiri ya kuzaa kwa uchungu.
Ndio maana kuna wanawake wameolewa wakiwa na watoto wa Mwanaume aliyeshindwana nae na wakapata mwanaume mwingine na mtoto wake akalelewa vema sana na baba mpya bila shida na familia ikaendelea.
Uchawi upo katika submission. Mleta maada ametoa mfano mzuri pale kasema baba anataka mtoto aende shule A, wewe mama umeona kuna shule B. Kwann usitenge muda mzuri na maneno mazuri kuongea na baba wa mtoto kwa ushawishi na utulivu wa akili ukimpa faida ya kumpeleka shule B na hasara za shule A hadi akusikilize na kusubmit kwako. Kwann wewe usinyenyekee sauti yake ili yeye anyenyekee sauti shauri lako unalompa?
Shida ni moja, nafsi imejazwa na roho ya ushindani na kiburi cha kuwa juu a.k.a Ego. Hakuna mwanaume anayeishi na mwanamke asiyenyenyekea. Ni mawili uchague kunyenyekea ili unyenyekewe au uendelee kubishana na ukweli uishi kwa kutangatanga ukitoka kwa mwanaume huyu kwenda kwa mwanaume yule huku ukisema wewe ni kichwa ngumu hauambiliki ile hali miaka inaenda na wewe ndie unaepoteza utu wako na mengineyo katika maisha yako.
Asante.
Sent using
Jamii Forums mobile app