Wanawake wa Pemba na Kanda ya Ziwa wapigwe sindano ya uzazi wa mpango kwa lazima, wanatesa watoto

Wanawake wa Pemba na Kanda ya Ziwa wapigwe sindano ya uzazi wa mpango kwa lazima, wanatesa watoto

Hata asipojaa ufukara lini uliwahi kuwezesha hao wasio mafukara ilihali bado hupambana wenyewe kujipatia rizki kuliko kuwashwa washwa na maisha ya Watu?
Sindano imechoma mfupa, punguzeni presha kwa wengine basi kuombaomba misaada kwa kuelemewa na familia ambazo hamuwezi kuzimudu, tumia vizuri hilo fuvu.
 
China pekee ina 1.3 bilioni ndiyo nchi inayokuwa kwa kasi kiuchumi kutokana na ukuwaji wa soko/watu.

Nyie hao wazungu mwaka 1974 England walikuwa zaidi ya miaka 80 leo Tanzania mupo 60 mil mnajiona mpo wengi.

Mmetawaliwa na wazungu
 
ah ah job hapa tuna mpemba ajira ya kawaida tu kaweka wake wanne..wakati mi huyo mmoja tu shida.....hawa wadau wana maamuzi magumu...utasikia wanamstiri mwanamke
Mimi naona kama mtu unajimudu hali zaa hata mia mbili, lakini siyo kazi yako kufyatua na kuwa mzigo kwa ndugu na kwa jamii, maana haya mambo huwa yanaleta hadi migogoro kwenye familia, mtu ananuna kisa kuna ndugu kakataa kumsaidia ada ya mtoto wake.
 
ah ah job hapa tuna mpemba ajira ya kawaida tu kaweka wake wanne..wakati mi huyo mmoja tu shida.....hawa wadau wana maamuzi magumu...utasikia wanamstiri mwanamke
Hawaogopi hao
 
Dar ina zaidi ya watu Milioni 5
Pemba ina watu chini ya laki 7
Point yako ni nini ? Kama ungetumia akili hata usingeandika ulichoandika. Ovu linalofanyika katik watu wachache ni rahis kuonekana kuliko maovu meng yanayofanywa palipo na watu weng, ni vgm kuyafichua.
 
mwaka 2014 mwezi wa 12 nilifanikiwa kua mgumu..ni bonge ya expirience...nashauri kila anayeweza aende hata kuja jilaumu
 

Attachments

  • 417065_3148265959298_1610340338_n.jpg
    417065_3148265959298_1610340338_n.jpg
    109.9 KB · Views: 4
  • 423745_3148260239155_89959155_n (1).jpg
    423745_3148260239155_89959155_n (1).jpg
    64.7 KB · Views: 3
Vipi kuhusu mwamko wa elimu kwa wanawake wa maeneo hayo ?
Mwanamke asiyejua kalenda yake ya hedhi unapata picha moja kwa moja kuwa hana elimu,mtoto anazaa au kuolewa na miaka 16 moja kwa moja mwamko wa elimu hakuna.
Hakuna mwanamke msomi atakubali kuzaa kila mwaka
 
Kusema kweli ni kuomba Mungu kama kakujalia chakula unakula na wanao ushukuru niliwahi kufika shinyanga vijijini kipindi Cha kiangazi kwenye Kijiji Fulani nikaona nikashuhudia watt walivyochoka nikajua ni kwann watt wengi kule wanakataa kwenda kidato Cha kwanza..... Boda boda miaka 24 wake wawili na ana wtt SITA.
 
Naandika nikiwa Simiyu baada ya kutoka safarini Pemba

Nimetembea mikoa mingi Tanzania ila haya maeneo tajwa yanashangaza.

Karne hii mwanamke anazaa watoto kumi!!!

Nilichogundua, wanawake wengi huku hawajui mensturation cycle inafanyaje kazimama mtu mzima hajui tarehe yake ya kuwa hedhini, hajui siku za hatari na salama ni zipi.

Unakuta mama ana mtoto wa miezi mitatu tayari ana mimba. Kabla hajakaa sawa binti yake wa miaka 15 naye ni mjamzito. Yaani unakuta mjomba ni mdogo kiumri kuliko mpwa wake. Imetokea mara kadhaa mama na binti yake wanakutana labor kujifungua, sasa, sasa mtoto wa huyu binti unakuta wakati mwingine ananyonya maziwa ya bibi yake maana nae ananyonyesha.

Itungwe sheria watoto mwisho watano tu.

Hali ya chakula sio nzuri siku hizi, mabadiko ya tabianchi yameathiri kilimo, watoto hawashibi, wakishiba ni vyakula visivyo na virutubisho

Mtoto mpaka anavunja ungo hajawahi kula yai, soseji, nyama mpaka mbuzi afe,maziwa mpaka unywe sumu bahati mbaya,mtoto hajui hata kiatu kinavaliwaje.

Acheni kutesa watoto mtoto ana haki ya kunyonya miaka miwili
Sherehee n watu.

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Njia za uzazi wampango zina mtu na mtu, unaweza ukatumia zikakupa athar ukajutia ila zikikuendea sawa unatumia tu, lakini mkuu wengine hawataki wanakwambia tu aka tumeambiwa tujaze dunia na kila mwana huja na rizikie
Ambao angalau tunajua A B C, tukomae na Kalenda ingawa inahitaji Uzalendo.

Hawa wengine tuwaelimishe
 
Back
Top Bottom