Wanawake wanawahi kuchoka, Mwanaume unatoa wapi ujasiri wa kuoa mwanamke mnayelingana umri?

Wanawake wanawahi kuchoka, Mwanaume unatoa wapi ujasiri wa kuoa mwanamke mnayelingana umri?

Bado mnajiuliza ni kwa nini babu zetu walikua wanaoa mke zaidi ya mmoja, majibu yake ndio hayo, huyo aliyefikisha 40 unampandisha cheo, then unamtafutia msaidizi mwenye 30 years, mmoja anakuwa manager mwingine CEO familia inastawi vyema kabisa
Sasa kama mwenye 40yrs amekushinda sasa huyo mdogo utamfanyia nini akuelewe!
 
Mwanamke mkilingana, hata stories zenu zinafanana. Marafiki wanakuwa agemates, mnakumbushiana habari za Amina Chifupa alipokuwa Clouds FM au Akina Daz Baba wakati anasoma Azania. Sasa wewe ulizaliwa 1985 unaona dada wa 2001 utapiga naye story gani wakati wa usiku??
Kwani lazima mpige story za zamani?
 
Oa mwanamke unayeweza kuwa comfortable naye. Oa mwanamke anayeweza kukupa amani ya moyo wako mpaka ndani ya nyumba. Mtu kama mimi sipendi mwanamke anayenipigia kelele na kunifokea. Ninaweza kumchoma kisu hata cha shingoni. Sasa nikipata mwenye umri kama wangu wa miaka 29 lakini ananipa amani ya moyoni, hanifokei, kwanini nisimuoe??
Sizani kama Mme anatimiza wajibu wake mke mwenye utimamu aanze tu kupiga makelele tu! Baadhi ya wanaume hawasimami kwenye nafasi zao mke akiongea anaonekana anampigia kelele .
 
Sasa mwanaume ukishazeeka kumzidi mke wako yeye ananza kumtafuta kijana wakutimiza mahitaji, Aisee mimi Naona Ni vyema Kuoana Mliolanga Hamna Tabu, Kwan Unataka ufanye mapenz mpaka Ukiwa na miaka 70 au? kuna mambo mengine
Waache ndiyo wale Mme umri umeenda na magonjwa juu maana ujana wake kachapa sana, umri ndiyo huo, mke damu inachemka ndiyo ile peshen anaenda nunua kijana ili atimiziwe haja zake
 
Maisha ni kuzingatia upevu wa akili,mfano mkiwa aged 30 wote wawili mtawaza kuanza ujenzi wa nyumba ya familia yenu wakati ukiwa na wa miaka 20 yeye atakuwa bado anawaza kuringishiana models za iPhones na kubadilisha mavazi huku wewe umri unaenda nguvu zikipungua akija kufika 30 wewe una 40 hapo ameshapevuka akili anaanza kuwaza ujenzi hapo mna watoto watatu wanasoma unadhani kuna kitu utafanya tena?

Mwanamke akila vizuri akilala pazuri hazeeki shida mnawatia stress kuchepuka lishe yenyewe hamtoi inavyotakiwa mnazeekea nyumba za kupanga hizo changamoto hataacha kuwa bibi akifika 43.
Umeona eee mke kila siku analia na kuumizwa halafu hapo anategemea aendelee kuwa msichana
 
Mwanamke mkilingana, hata stories zenu zinafanana. Marafiki wanakuwa agemates, mnakumbushiana habari za Amina Chifupa alipokuwa Clouds FM au Akina Daz Baba wakati anasoma Azania. Sasa wewe ulizaliwa 1985 unaona dada wa 2001 utapiga naye story gani wakati wa usiku??
Amina Chifupa enzi zile na kipindi chake cha African Bambataa Clouds FM kuanzia saa moja usiku nlikuwa sibanduki kwenye redio.
 
Nitoe mfano, majina yakiwa ya kutunga.

Mwaka 2008 Fred akiwa na miaka 26 alifunga ndoa na Recho mwenye miaka 25. Wote walikuwa bado ni vijana wabichi kabisa wanavutia.

Kufikia Leo Fredi ana miaka 41 huku Recho ana 40, unaweza kuhisi Fred alioa dada yake.

Fred ni rafiki yangu, anakiri kwamba alikosea kufanya huo uamuzi hasa ukizingatia yeye bado kijana ambae huvutiwa bado na mabinti wenye muonekano wa ujana bila make up, ambao wengi ni chini ya miaka 32.

Muda huu ni ngumu hata kwa Recho kuzaa na kuzaa akiwa na miaka 41 na kuanza kulea watoto, ule umri mzuri wa kuzaa ushampita, hivyo inakuwa kizuizi hata kwa Fred.

Pia wote kwa pamoja wapo katika hatari ya magonjwa nyemelezi ya miaka ya 40 kama kisukari, homa ya ini, presha, n.k.
Usimsingizie Vunja Bei, Huyo ni wewe
 
Back
Top Bottom