Wapinzani pelekeni hoja nzito kwa wananchi, sio blaa blaa za Bandari

Bungeni huwa kunapelekwa mikataba au makubaliano? Danganyweni tu na sijui uchumba na ndoa..!!
 
Bungeni huwa kunapeekwa mikataba au makubaliano? Danganyweni tu na sijui uchumba na ndoa..!!
Iliyoandikwa imeandikwa!!! Katiba imetoa mamlaka kwa bunge na wabunge kuamua kwa niaba ya wananchi, kupinga hilo ni kuvunja katiba, na anaevunja katiba ambayo watu wameapa kuilinda lazima aadhibiwe. Hiyo ndio maana ya utawala wa sheria, hakuna kujiropokea tu barabarani. Muulize Mh Job Ndugai kuhusu hili atakwambia kuhusu mkubwa ni nani kati ya Rais, Bunge na Mahakama.
 
Hili swali hujaliona au limekushinda? Bungeni huwa kunapelekwa mikataba au makubaliano?
 
Swali fikirishi sana !
 
Mkuu wa Nchi = Locuta causa finita ! Kwa kilatini !
 
Hili swali hujaliona au limekushinda? Bungeni huwa kunapelekwa mikataba au makubaliano?
Wacha mahakama itoe tafsiri juu ya hilo. Utawala wa sheria unakataa kujichukulia sheria mkononi ya kutuhumu na kuhukumu mitandaoni. Kusema bandari inaunzwa ni sawa na kujichukulia sheria mkononi kutuhumu na kuhukumu mwenyewe. Kifupi ni uchochezi dhidi ya Rais, serikali na bunge. Kumbuka kuwa kama utafanikiwa kuwachochea sawasawa wananchi wanaweza kuichukia serikali Yao na bunge lao, wanaweza ama kuipundua serikali, au kuharibu mali za watu na umma au kusababisha vifo. Ndio maana nasema Kuna Nia ovu kwenye jambo hili kwa baadhi ya wapingaji.
 
Kwahiyo kwako wewe suala la bandari ni blaa blaa? Kweli "Kichwa kisicho na akili ni mzigo kwa shingo."
 
Maelezo mengi lakini hujasema kifungu kipi cha Sheria au Katiba kimevunjwa. Usione Serikali imekaa kimya inajua Sheria haipo upande wake kwenye hili suala labda watumie nguvu tu. Na hilo wanaogopa sababu Mama yako anapenda kwenda Ulaya.
 
Maelezo mengi lakini hujasema kifungu kipi cha Sheria au Katiba kimevunjwa. Usione Serikali imekaa kimya inajua Sheria haipo upande wake kwenye hili suala labda watumie nguvu tu. Na hilo wanaogopa sababu Mama yako anapenda kwenda Ulaya.
Mimi ni muumini wa matumizi ya sheria. Nina hate watu kujichukulia sheria mkononi kindezindezi. Mtu anakwenda mbele ya camera na kusema nchi inauzwa!! Toa ushahidi basi Hana!! Ni watanzania wangapi wanaopinga bandari kubinafsishwa hajui, wako wangapi? kimyaa!!!, wamekutuma?
 
Kama unaamini Sheria na unaona wanazivunja una jukumu kuwapeleka Mahakamani kama raia mwema wa hili Taifa.
 
We kavulata unazunguka tu wala hujibu swali..!!
 
Maelezo mengi lakini hujasema kifungu kipi cha Sheria au Katiba kimevunjwa. Usione Serikali imekaa kimya inajua Sheria haipo upande wake kwenye hili suala labda watumie nguvu tu. Na hilo wanaogopa sababu Mama yako anapenda kwenda Ulaya.
Na alama mojawapo ya kujua wanajiona wamekiuka kitu, wamepeleka muswada bungeni ili kuhalalisha wayatakayo
 
Haya soma katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, ibara ya 63, kifungu cha 3, kifungu kidogo e. Bungeni kunapelekwa mkataba. Hilo neno makubaliano, wewe taja kifungu kiachosema bungeni unaweza kupeleka makubaliano. Kisome hicho kifungu hapo chini;


Kwa kifungu hiki, maana yake ule ni mkataba. Mkataba huo kuuita MAKUBALIANO, ni kutafuta unafuu tu wa kulaumiwa kwamba wamefanya makosa makubwa.
 
 
Wala sio wajinga hata kidogo wanajuwa sana watendalo,ndomana waliambizana pale bungeni ataepinga ahame ccm ,nawalishangilia sana bunge zima,, lakini jiulize wewe kazi ya mbunge niipi? nakwanini wabunge wanapingana na wapiga kura wao? Bunge letu lina historia yakuwa upande wa serikali badala yawananchi,,
 
Alisikika mmoja akisema, wale ni;
1. RUBERSTAMP
2. NDIYOOOO
 
Wewe bilashaka ni msomi, mkataba ni nini? makubaliano ni nini? kuna tofauti gani kati ya mkataba na makubaliano? kuna aina ngapi za mikataba/makubaliano?
 
Kama wabunge hawana sifa, hadhi na uwezo peleka hilo mahakamani kisha subiri hukumu ya wanasheria wako na mahakama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…