Wasaka ubunge ndani ya CHADEMA waanza kumzidi nguvu Tundu Lissu

Wapi Chadema imesema itashiriki uchaguzi mkuu kabla ya katiba mpya? Una clip au press release Mbowe akisema hivyo?

Kama ni hivyo Kulikua na haja gani ya kususia task force ya Rais maana ndio ilitaka tume huru kabla ya uchaguzi!! Then katiba ifuate baadae.
 
Huwezi kupata Katiba Mpya kabla ya 2025 labda iwe Katiba ya Viraka
 
It's not necessarily kuwa, msimamo wa jana uwe ni wa milele..

People change, environment changes too..

Lakini lililo muhimu ni hili:

Kwamba, Kuna mazungumzo (maarufu kama maridhiano) ya kurekebisha mambo na makosa mbalimbali yaliyosababisha ugumu na machungu ya maisha kijamii na kisiasa tangu mwaka 2016 na kilele chake kuwa mwaka 2020 Kwa kilichoitwa "UCHAFUZI MKUU" chini ya yule mtu mbaya John P. Magufuli yamefanyika na bado wanaendelea kuzungumza..

Na kwenye maridhiano huwa kuna KUPATA na KUPOTEZA (lose & get). Kwa hiyo, si ajabu kabisa kama kuna kubadilikq Kwa msimamo..

And honestly, kwa muda uliobaki mpaka kufika 2025 si rahisi sana Kuanza na kuumaliza mchakato wa kupata katiba mpya na Kisha iwe tayari kutumika Kwa uchaguzi mwaka 2025..

Ila kunaweza kufanyika mambo fulani fulani yatakayohakikisha ingalau uchaguzi mkuu wa 2025 unakuwa at least free and fair..
 
Mbowe aliwahi kusema kuna timu itaundwa kila mkoa kwa ajili ya kutoa elimu hiyo, sijui itaundwa lini.

Inavyoonekana kuondoka kwa Lissu ghafla sasa kunaanza kuzua maswali
Wamelewa na Umati uliokuwa staged na hivyo kuamini kuwa ule umati uko nao mpaka 2025 kwenye boksi

PROF. LIPUMBA: KUPIGWA RISASI HAIKUONGEZEI SIFA YA KUWA RAIS WA TANZANIA

Prof. Lipumba wakati anajibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari amemlipua Tundu Lisu kuwa ajue kupigwa risasi siyo sifa ya kukufanya uchaguliwe kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Prof Lipumba amesema kwenye sifa za mtu kuwa Rais wa Tanzania kupigwa risasi haipo, hivyo Lisu angeendeleza sera za kuwaunganisha watanzania na kuwaletea maendeleo na siyo kuimba kupigwa risasi kila siku.

 
CHADEMA kutoshiriki kwao chaguzi ni kukiua chama.
They should stick to what they did best. Wapate strong candidate kutoka CCM kama walivyompata Lowasa, awasaidie kupata wabunge kadhaa, wapate ruzuku, waendelee kula bata.
Habari za kuwazia uraisi, ni ngumu sana tena sana kuitoa CCM madarakani. Si kwa katiba ya zamani wala kwa katiba mpya.
Hata ukichukua katiba ya Marekani, Ufaransa au Uingereza ukaileta hapa, si rahisi wakashinda. CCM wana watu. Namba zinawabeba sana mijini na vijijini.
Katiba mpya waitumie tu kama ajenda ya kuendeshea mikutano ya hadhara lakini haitowasaidia kwa lolote.
 
Mbowe aliwahi kusema kuna timu itaundwa kila mkoa kwa ajili ya kutoa elimu hiyo, sijui itaundwa lini.

Inavyoonekana kuondoka kwa Lissu ghafla sasa kunaanza kuzua maswali
Si tuliwaambia, Kiko wapi sasa? Machadema huwa hamna akilu
 
Principle hazichange.

Kama katiba ya sasa haiwezi kuguarantee uchaguzi huru na haki basi haiwezi kuguarantee uchaguzi huru na haki, jana leo hata kesho. Haijalishi Samia ana tabasamu zuri namna gani kwa akina Mbowe
 
Ni kama mambo yamekuwa mengi na kuwazidi uwezo, nikitazama kauli aliyotoa Lema kuwataka wanachadema wasimpinge Samia, kuwepo na ukimya juu ya Katiba Mpya, kuondoka kwa Lissu ghafla, naona inawezekana kuna jambo inawezekana halipo sawa, muda utaamua.
 
Yaani unatunga tu uongo kwa vile JF ni jukwaa huru !
 
Mbona una presha sana, ziara iliyobaki Bado magharibi, Kanda ya kati, kusini, kaskazini n.k wakishazindua mikutano Kila Kanda ndio Sasa hizo timu za katiba mpya zitaundwa.

What's the rush, everything is under control.
Naona suala la Katiba Mpya halihitaji kuremba, kwasababu madai ya Katiba Mpya ni sawa na kukimbizana na muda, ili lifanyike before 2024, kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kwasababu baada ya hapo utakuwa umebaki mwaka mmoja pekee kufanyika uchaguzi mkuu, sidhani kama ndani ya huo mwaka mmoja.Katiba Mpya inaweza kupatikana.

Na nikizingatia Chadema walishajifunga wenyewe, kwamba bila Katiba Mpya hakuna uchaguzi, nahofia wasijekujiingiza kwenye mtego mwingine wakajikuta wanazalisha Covid wapya ifikapo 2025, kwasababu inavyoonekana kwa nje, kwa Samia mambo hayatakuwa magumu kushiriki uchaguzi na kushinda, kama ilivyokuwa awamu ile iliyopita, hivyo hili linaweza kuzua mtifuano ndani ya chama.
 
Msimamo wa Lissu nauunga mkono, ni Bora tusiende bungeni, kuliko kwenda bungeni na Katiba hii, hakuna maajabu tutayofanya, Bali tutakuwa sehemu ya tatizo na tutaendelea kulalamika

Hapo mnamkomoa Nani?
Mlitakiwa kuwaza hivyo kama chadema ingekuwa ni chama chenye nguvu na ushawishi mkubwa

Unaongea hivyo wakati hata kuita maandamano hamuwezi?

Nyie kama mkisusa vyama vingine vitapeleka wabunge na mambo yataenda

Nyie endeleeni kuwaza katiba mpya
 
"People change, environment changes too"

Huu ndio mtego naouona unaweza kuwanasa Chadema, kama ambavyo tayari umeshakunasa wewe, ni muhimu Chadema waipiganie Katiba Mpya sasa na wasitegemee fadhila za mtawala, kwani huyo mtawala hatadumu milele, kuweni makini.
 
Hilo la No katiba mpya no Uchaguzi mbona limepita hasa baada ya Rais Samia kasema wanifanyia kazi serikali na upande wa pili.
Sasa mlitaka Chadema waendelee kujikita kwenye hilo badala ya watafanya Nini baada ya uchaguzi?
Au mlitaka hayo wayaseme baada ya katiba mpya?
Kule kwetu wanasema, MWANAUME ANAGEUKA KITANDANI TUU NA SIO KAULI.
Hilo mbona limeisha!
 
Ni kama mambo yamekuwa mengi na kuwazidi uwezo, nikitazama kauli aliyotoa Lema kuwataka wanachadema wasimpinge Samia, kuwepo na ukimya juu ya Katiba Mpya, kuondoka kwa Lissu ghafla, naona inawezekana kuna jambo inawezekana halipo sawa, muda utaamua.

Ninadhani mapokezi yalikuwa freestyle ambapo watu walikuwa huru kusema lolote na kwa vyovyote.

Ninadhani mikutano ya mapokezi haikuwa mikutano ya kazi. Zaidi ya kuwa ilikuwa ya kukutana na wapendwa baada ya muda mrefu.

Hatua inayofuata ni muhimu sana. Mtu asiseme lolote au vyovyote kama ambavyo angependa bila uratibu.

Kumbuka Lissu akiongea chawa hupoteana.

Wako kwenye rekodi kina johnthebaptist kuwa, "Lissu siyo size yetu."

Kwa Lissu waliomba usaidizi kutoka kwa jamaa wa majalani.

Erythrocyte hatujachelewa bado.
 
Siamini kama ni suala la kulewa au vinginevyo, kwasababu Chadema kujaza "nyomi" kwenye mikutano yao haliwezi kuwa suala la kujadili na kubishana, ile ni fact, ambayo kila mwenye macho haambiwi tazama.
 
Nina imani kama kiti kingekuwa bado kinakaliwa na shetani mkuu, chadema wasingetamani kushiriki uchaguzi wowote. Kabla ya shetani kukalia kiti chaguzi zilikuwa zinafanywa at least kwa 60% zilikuwa zina ukweli

Saafari hii mambo ya kupita bila kupingwa hatatayakubali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…