Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Babu walizalisha watoto 12 lakino waliachia wake zao wawalee kwa kukatia kila mmoja shamba na kuwapa ng'ombe. Wengine wakarogana, watoto wengine wakakosa privilege ya kusomeshwa kisa wa kike, sasa saivi tunataka kuwaiga huku 20X20 unanunua milioni 10 na Dar sijui bei gani.Sio Wasukuma pekee ndiyo Walaji wa chakula kingi. Nafikiri ni mikoa yote ya Kanda ya Ziwa ni Walaji wazuri wa chakula kingi.
Ulaji wa chakula kingi unategemea na shughuli mtu azifanyazo, kama utakuwa unafanya kazi nyingi za nguvu huna budi kula chakula kingi ili kupata energy ya kutosha kwenye shughuli zako.
Mimi pia nilikuwa Mlaji sana wa chakula nikiwa kule, baada ya kuja DSM nikapunguza kabisa.
Juzi nilipoenda Musoma kusalimia, nikakutana na msosi wa kula watu sita wa DSM lakini tukatakiwa kula watu watatu.
Kwanza walipakua wali Samaki tukala.
Baada ya dakika 15 wakaleta mezani ugali Samaki, eti walisema ule wali ilikuwa ni wa kuonja tu 🙌
Kwa kweli tunaoishi mijini ni kama hatuli kabisa, haiwezekani ule Chipsi sahani Moja eti ushibe, hizo nguvu za kuzalisha watoto 12 kama Wazee wetu zinatoka wapi 🙌
Binafsi isingekuwa haya maisha ya Kisasa na kufata mambo ya Dini ya Mke mmoja, ningeshakuwa na Watoto 20 saiviBabu walizalisha watoto 12 lakino waliachia wake zao wawalee kwa kukatia kila mmoja shamba na kuwapa ng'ombe. Wengine wakarogana, watoto wengine wakakosa privilege ya kusomeshwa kisa wa kike, sasa saivi tunataka kuwaiga huku 20X20 unanunua milioni 10 na Dar sijui bei gani.
We inakuathirije katika shughuli zako Kila siku za kutafuta mkate???Habari za jumapili wakubwa.
Juzi kati nikamtembelea jamaa yangu flani hivi ni msukuma anaishi nje kidogo ya mji.
Ebana sijawahi kuona watu wanakula kama hawa watu.
Imeletwa nguna ya watu watatu tu mezani lkn hiyo nguna kwa wanaume wazembe kama wa dar wangeweza kula mwezi mzima.
Tumepiga nguna weeeee me nikasarenda nikawaacha wenyeji wakaisukuma mpaka ikaisha nikabaki mdomo wazi tu.
Ndugu zangu punguzeni huu ulaji wa hovyo namna hii.
Kama hauwachangii kwenye huo msosi huna haki ya kuwasimanga
Kule Kijijini wali ni kama starter tuKwamba wali ni starter?
Unawatafutia Hadi uwapangie???Unakuta mtu anakula kilo moja ya mchele, chai jagi, chapati nane peke yake, je akila pasi ndefu atakula kiasi gani? Wajifunze kushiba chakula kidogo
kula chakula kingi ni aibuUnawatafutia Hadi uwapangie???
kula chakula kingi ni aibu
Aisee hadi mimi nilishangaa kuona binti mdogo tu ameshusha mzigo mithiri ya gogo asee😂😂Wanaona sifa kula chakula kingi, wanasema kwao hakuna njaa wanalima sana. Mtoto mdogo anaanza kulishwa chakula kingi ili tumbo lipanuke awe anapakia chakula kingi hatimaye akiwa mkubwa awe na umbo kubwa. Mshangao ni pale wakienda chooni mtu anashusha kimba la kilo mbili! Kwa ulaji huo choo kitaachaje kujaa haraka?