Wasukuma punguzeni huu ulaji wa chakula kingi namna hii

Wasukuma punguzeni huu ulaji wa chakula kingi namna hii

Habari za jumapili wakubwa.
Juzi kati nikamtembelea jamaa yangu flani hivi ni msukuma anaishi nje kidogo ya mji.
Ebana sijawahi kuona watu wanakula kama hawa watu.
Imeletwa nguna ya watu watatu tu mezani lkn hiyo nguna kwa wanaume wazembe kama wa dar wangeweza kula mwezi mzima.
Tumepiga nguna weeeee me nikasarenda nikawaacha wenyeji wakaisukuma mpaka ikaisha nikabaki mdomo wazi tu.
Ndugu zangu punguzeni huu ulaji wa hovyo namna hii.

Rekaga kuyomba ma mihayo ga basaji. Bebe utanyaga? Jaga ukanye ukuje nhumbi urye,
 
Wanaona sifa kula chakula kingi, wanasema kwao hakuna njaa wanalima sana. Mtoto mdogo anaanza kulishwa chakula kingi ili tumbo lipanuke awe anapakia chakula kingi hatimaye akiwa mkubwa awe na umbo kubwa. Mshangao ni pale wakienda chooni mtu anashusha kimba la kilo mbili! Kwa ulaji huo choo kitaachaje kujaa haraka?
Aisee hadi mimi nilishangaa kuona binti mdogo tu ameshusha mzigo mithiri ya gogo asee😂😂
 
Mtoa thread hapo kuna mambo mawili unatakiwa utambue
1. Anaishi kijijini au mjini
2. Hali ya kiuchumi ikoje

Tuchambue sasa kwa kifupi
1. A. Kijijini maranying watu wanakula milo miwili yaani mchana na jioni alafu wanafanya kazi ngumu kwahyo mwili unahitaji chakula kingi ili kukizi mahitaji ya mwili
B. Mjini maranyingi hawafanyi kazi ngumu na milo ambayo wanakula ni zaidi ya tatu tena ambayo haina mipangilio ndio maana wanaota vitambi 😄😆. Kwahyo ukipiga hesabu unakuta wa mjini anakula chakula kingi kuliko yule msukuma wa simiyu
2. Hali ya kiuchumi kwa watu wengi waishio mjini ni mbaya sana hata kama anakula milo yote mitatu lakini ni kwa shida sana.
Unakuta familia ya watu watano asubuhi wanakula mihogo ya mia tano na chai nusu kikombe
Mchana wanakula nusu kilo ya unga
Usiku wanakula nusu kilo ya mchele kwa idadi ileile ya watu na siku imeishia hapo. Huyo mtu akienda usukumani walimaji anakuta ndonga ya watu watano wanaokula huko mjini inapigwa na watu wawili lazima ashangae na kuona kitu cha ajabu sana

Ngoja nikale kwanza nitakuja kuendelea.......
 
Chooni huwa unafuatilia.
Binafsi mimi ni Msukuma, kwa miaka 15 liyopita nimehamia Uchagani huku. Na niko huku nakula kama niliyokua nakula nyumbani. Tunatwanga ugali maziwa, na mboga za kutosha.

SIna overweight km wanaokula kidogo.Huku wanawache wanavutambi ila usukukumani hakuna mwanamke mwenye kitambi.
kabisa mkuu, usukuman wanawake wenye vitambi kama uchagan hakuna na watu wanakula chakula cha asili wana nguvu nyingi na ni imara hata akizeeka, nimewahi kukaa na wasukuma nakuunga mkono uliyosema ni ya kweli.
 
Binafsi isingekuwa haya maisha ya Kisasa na kufata mambo ya Dini ya Mke mmoja, ningeshakuwa na Watoto 20 saivi

Ukienda Vijijini unauziwa ekari 50 Kwa shilingi milioni 2.5 tu, wastani wa ekari Moja shilingi 50,000

Hapo ukijenga yale maboma kila Mke na boma lake, Kila boma umefunga Umeme wa Solar kwaajili ya mwanga

Wakati huo umenunua majembe ya kuvutwa na ng'ombe, ni mwendo wa kulima tu

Chakula hakikauki ndani, magunia na magunia

Siku hizi Elimu ni bure, watasoma kuanzia Shule ya msingi hadi wanafika Chuo Kikuu ambapo wanakutana na boom la Serikali
Maisha ni zaidi ya kula, wabongo tujaribu kuwa na imaginations pana zaidi ya kuzaa na kushiba tu.
 
Ni jamii ya wafugaji wote ni walaji wazuri. Juzi nilienda umasaini kwa jamaa mmoja kununua ng'ombe.

Ilibidi niende asubuhi kabla ng'ombe hazijaenda machungani. Nimemkuta mke wa jamaa amesonga ugali wa dona mkubwa sana. Cha ajabu yule mama alauacha ugali uungue jikoni kwa muda mrefu hadi ukabadilika rangi. Then akawaletea jamaa waule
Ule ugali ni mwingi sana na jamaa walikula wakiwa nyama huku na maziwa mgando lita 1 kila mmoja.
 
Maisha ni zaidi ya kula, wabongo tujaribu kuwa na imaginations pana zaidi ya kuzaa na kushiba tu.
Soma Biblia, Ibrahim Baba wa Imani alikuwa na Watoto wangapi?

Mfalme Suleiman alikuwa na Watoto wangapi

Mtume Mohamed SWS, alikuwa na Watoto wangapi

Maisha yafaa nini kama hatuli na kuzalisha ili Koo zetu ziendelee
 
hiyo ilikuwa ni misingi tuliyoachiwa na Mitume wetu, ni lazima tuifate
Sio lazima muifuate, mnaamua wenyewe kuifuata au kutoifuata kwa kuangalia uhalisia, pia itafika wakati nyakati na hali halisi zitawafanya mshindwe kabisa kuifuata.
 
Je, kuna namna yyte ulaji wao unawasababishia njaa? Mkuu ebu kuwa na hoja basi yaani unataka msukuma ambaye akienda shambani saa kumi na mbili asbuhi natoka saa kumi na moja jioni huku amelima nusu heka ale sawa sawa na mtu ambaye amekaa ofisini au kijiweni? Unajua nguvu alizopoteza? Maana nyie watu wa daslamu mnakoelekea utasema waanze na kula sembe dona sio chakula.
Kila mtu aishi kwenye mfumo wake wa chakula na ndio matabaka ya maisha wewe hapo unakula kidg unajiona mjanja wakat kuna watu wanakushangaa pia
Watu awajui kuwa injini ya tractor ni tofauti na injini ya IST
 
Back
Top Bottom