Wataalam wetu wamefikia hatua gani kuhusu kinga ama tiba ya Corona?

Ubarikiwe sana mkuu wangu aseee naona umemaliza kabisa mpk kwa wale wa Kilimo teh teh teh kama ulivyosema nmeleta hii as a challenge tujipime tunakwama wapi mbn kipindi hiki cha Magufuli ndo kipindi cha uthubutu wajaribu wataweza. Wapo wanaoona kuwa tunawadhalilisha kama Baba Swalehe naomba anisamehe wala sina maana hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kitu mzee kwenye mfumo wetu na hii ni afrika nzima. Wanatusisitizia kutumia sanitizers badala wao washinde lab kushusha madude.

Sent from my TECNO WX3 using Tapatalk
 
Pole Sana mkuu !!
 
Eeenh, umejitakia mwenyewe.

Sasa umechokoza wenye fani zao, sijui yakikupata utakimbilia wapi.

Maticha ngangari...; ukigeuka huku, ukajisikia kama corona unaye, Baba Swalehe anakusubiri kukutia adabu, hata kiapo chake "First Do No Harm" hana habari nacho!
Anakwambia waziwazi kwamba yeye anao uwezo wa kuamua uishi au ufe! Haya makubwa.

Nawe itumie ya kwako mkuu wangu 'shark'. Ndivyo nchi yetu inavyokwenda hivyo.

Pole sana waTanzania. Hasa wakulima, maana wao kiboko yao ni 'walanguzi' wa mazao yao na hawana pa kukimbilia kujiokoa.
 
Really! unataka NIMR Waseme nini kwenye hili janga! Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma na Waziri Wanatosha! Msijipe Presha bila sababu! NIMR!???
 
It is more complicated than that!

Hao ma'intellectuals' unaosema wako "in deep slumber" nyinyi mlio serikalini ndio mmewalazimisha wawe katika hali hiyo. Kuwa serikalini na kwenye uongozi ndani ya nchi ndiko kunakoanzia maono ya mwelekeo mzima wa nchi.

You must be jocking when you think you can have a 'proposal' and sell it like a glass of juice!
 
Kwa mujibu wa sheria magonjwa ya mlipuko hutangazwa na waziri wa afya au rais, siyo mtu unaibuka tu untangaza bila kuwasiliana hata na wizara husika
 
Tanzania has some of the weakest PhD s. Mtu yuko tayari kujisifu ana PhD lakini ukimuuliza kwanini mavi ya mbuzi ni punje punje wakati ya ng'ombe ni li moja hawana jibu. We have PhD that don't even know shit...
Itakua research ya covid 19?
 
Kutengeneza dawa inataka research and it can be a very expensive and lengthy process from research to human usage ndio maana zinawekewa patents (well unless kwa wahindi wanao subiri wenzao wagundue waje na knockoff products na hata hao kila siku wanashinda mahakamani kuthibitisha ni zao).

Nchi za Africa labda kwa makaburu tu ndio kuna pharmaceutical companies zenye research centres zilizobaki hazina hata pharmaceutical companies zenye uwezo huo hizo dawa watagundulia wapi hao Phd wetu.

Sanasana Africa ukikuta kiwanda basi kimenunua patent ya kuzalisha dawa tu.
 


Ni kitu rahisi isipokuwa sisi ngozi nyeusi tumelelewa ndani ya "realm of impossibilities", our mentalities are reared to believe in impossibilities on many if not all things. Hicho ndicho chanzo cha tatizo.

Mfano, mtu uwe na technology na uitafutie "patent" na uipeleke sokoni, ni mfano huo ndio unao apply kwenye nyanja za taaluma zingine za tafiti, unapeleka propasal za tafiti zako na kabla hawaja toa funds zao ni lazima wajiridhishe kwanza hiyo tafiti yako imekaaje na je itawafaidisha wao???!!! It is not just as selling a glassful of juice or a bottleful of liquor, it just a matter of assessment and finally sit on the table for negotiation for mutual benefits of both parties.

Waafrika hatuna vitu vya kuumiza vichwa ni wazungu tu ndio wanavyo vichwa vya kuumiza kwa ajili yao na sisi na ndiyo maana walitutawala na bado wanaendelea kututawala this time in a spectacular fashion.🤣
 
Mimi sizungumzi uafrika au kulaumu uafrika kwa hayo unayoyaandika hapa kinadharia.
Zaidi ya yote hayo ni nyenzo zilizopo kukuwezesha na mazingira uliyomo; ndio maana nikaandika na kukupa mfano huo wa kuuza glasi ya juisi, kufuatana na nadharia ya kiujumla uliyotumia.

Patenti hata leo nenda ofisi zipo, sijui tena ni wizara gani, inatoa patent kama una ugunduzi wowote uliotaka kuulinda. Na kama unaugunduzi wowote katika mazingira haya, utabaki kwenye makaratasi hadi muda wa kuulinda unakwisha kabla hujaufikisha sokoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…