HOJA Wataalamu wa kipengele cha uhamisho ndani ya ESS naombeni msaada mnivushe hapa

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Mimi ningekua wewe ningeomba kazi kabisa kama naona sifa ninazo.
 
Kuna ajira mpya iliajiriwa mwaka jana hapa halmashauri ndani ya miezi minne ikahamia taasisi Dodoma bila hata kuthibitishwa.

Yenyewe ilihama kwa makaratasi.

Wiki iliyopita imerudi tena baada ya utumishi kuitumia barua ya kurudi kituo chake cha kazi alichoajiriwa mwanzoni.
 
Nyinyi jamaa mpo level ya kusubiri majibu na mna wasiwasi hivi mmetuwazia ambao ess inakuambia haujatimiza miaka 3? šŸ˜…

Siyo hivyo tu, na hata miaka 3 ikitimia najua nitakutana na changamoto aliyopost jamaa hapo ya "staff deficit" kwakua sisi tupo wawili tu na mwongozo unataka tuwe angalau 15.

Sasa shida ni maslahi, roho mbaya na kukua career wise. Mimi nimetoka private so kuna attitude fulani nilikuja nayo serikalini lakini kwa hapa nilipo hapana kubababake.
 
Jaribu kutafuta taasisi mbalimbali one day Mungu atakujalia utakuta taasisi Moja ombi litakubalika tu pia kwa kozi Yako jaribu nafasi kama TA, Warden, Examination officer, Admissions officer nk tafuta sehemu sahihi kwako ,usitafute sehemu yenye mshahara mkubwa
 
Taasisi ya elimu ya watu wazima mbona ina nafasi nyingi za kuhamia muhimu ni kwenye mfumo wakati wa kuomba vacancy bonyeza kipengele cha recategorization then chagua kada kama Instructor, Tutorial Assistant, Assistant lecture na kadhalika ila pale nafasi zipo mzee
 
Kama Ajira portal wanatangaza za kuhamia kada kama yako kwanini usiombe via that channel..?
Hizo pambania, kikubwa upitishe tu barua kwa Mwajiri, nimeona hata jana wametangaza za HR's
 
Ina maana huo kibali Cha uhamisho wa mwanzo hawakutoa hao UTUMISHI, kwanini wamrudishe au kumsumbua mtumishi..?
 
Ina maana huo kibali Cha uhamisho wa mwanzo hawakutoa hao UTUMISHI, kwanini wamrudishe au kumsumbua mtumishi..?
Kuna mwezi fulani Utumishi walitangaza wanarudisha watumishi waliohama bila utaratibu
 
Kaka uliajiriwa taasisi straight au ulihamia na ndiyo umehamishwa tena?
 
Duuh kwel kaka hii n changamoto
 
Aiseee hivi huruhusiw kugomea uhamisho wa utumishi, happ labada na weww uanze kupambana kuomba uhamisho, ila unaonekana umetokea kwenye taasisi nzuri sana ilikuwa inalipa vzur sana hata TRA hawafiki huko
 
Mkuu embu nenda Sumbawanga nasikia kuna waganga wazuri usikae kinyonge.

Wamekufanyia roho mbaya sana kumamae'
 
Nakuelewa mkuu.

With 15 years of experience wewe ni principal officer ulihamishwa ili uwe mkuu wa idara huko halmashauri?
 
Mkuu hii ni NSSF au PSSSF..? maana kwa hiyo salary na posho inaweza kuwa ni Moja ya Taasisi kati ya hizi..?
Nawaza hiyo posho 2.5 M.. yaan hata basic ya mshahara wangu haifiki halafu huko wanapokea kama posho. Uwiiiiiiih kuna taasisi watu wanakula maisha hii BongošŸ¤”

Sisi wengine tunapambania uhamisho Taasisi zenyewe hata posho hazieleweki na Bado hatupewi Vibali tunasugua😁
kinondoniilala
 
Kwenye hizo taasisi umetaja kuna mojawapo kuna senior wangu kaenda anakuambia mshahara wake ni mkubwa kuliko hata wa DED na kamzidi mkuu kada yetu kitaifa.
 
Mwanzo nilikuwa naomba kwa ku create transfer vacancy ikawa inagoma kwa kuandika "not budgeted", ila baada ya kupitia uzoefu wa watu humu nika delete ile transfer nakuomba kupitia normal transfer naona imekubali kwenda. Ngoja nijaribu kusikilizia
 
Mwanzo nilikuwa naomba kwa ku create transfer vacancy ikawa inagoma kwa kuandika "not budgeted", ila baada ya kupitia uzoefu wa watu humu nika delete ile transfer nakuomba kupitia normal transfer naona imekubali kwenda. Ngoja nijaribu kusikilizia
sawa
 
Si uache kazi brother? Mimi kaka yangu alikuwa kigoma dc akahamishiwa sehemu wanapaita njia za maji ndani ndani akwenda akafungua case mahakamani yuko mtaani tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…