HOJA Wataalamu wa kipengele cha uhamisho ndani ya ESS naombeni msaada mnivushe hapa

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Wakuu nani Leo kapata kibali.. au ndio tusubiri At end of the Month..
 
Wataalamu mnivushe hapa ajira ya 2022 anapanda daraja mwakani 1/7/2027 ni mwalimu Sasa kaanza mchakato tamisemi uhamisho wa kubadilishana anatarajia desemba utakuwa umefika TAMISEMI ila amesikia fununu kwamba ukipewa barua ya uhamisho TU scores zako zinasoma 0% hata jamiiforums walipost kule Instagram, Sasa endapo akipewa barua ya uhamisho mwakani mwezi 3/6 chance yake ya kupanda daraja itakuwaje?
 
Nimekutana na muuguzi aliajiriwa 2022 June hajapanda daraja.

Ila huyu muuguzi alikuja na afisa lishe, huyu afisa lishe kapanda daraja.

Nimekutana na mwalimu wa mwaka huo na mwezi huo kashapanda.

Watu watatu ninaowajua wawili wamepanda na mmoja hajapanda. Halmashauri moja na wamekuja muda sawa.

Ndiyo naona na wewe unasema mwalimu wa 2022 atapanda 2027 hiyo si itakua miaka 5? Au muundo wa walimu wao wanapandaje?
 
Duh pole sana mkuu ,kila la kheri kwenye mipango yako🙏
 
Iko inategemeana na halmashauri ajira ya 2022 ilikuwa tarehe 1/7/2022 Sasa ikotokea afsa utumishi wenu aliandika 30/6/2022 kama siku ya kuajiriwa ndio unapanda, so wife siku Moja ndio ilisababisha halmashauri yao wasipande, naomba msaada unijibu kwenye swali endapo akipata barua ya uhamisho mwakani kabla ya kupanda daraja itakuwaje?
 
Kwanini usitafute Taasisi au Regional secretary Zina posho nzuri pia..? Wajuzi hebu tuambieni
Hakunako chochote isipokuwa tu sina namna.

Tatizo mtoto wa mkulima sina connection yoyote mkuu. Mwezi jana nimepata recategorization kwa tabu sana baada ya kukaushiwa miaka 10 kazini bila kupanda daraja. Baada ya muundo kubadilika nikaitwa na afisa utumishi na kuambiwa kwa sasa hakuna nafasi nitafute transfer.

Baada ya kuambiwa hivyo nikaanza kuomba transfer kila sehemu naambiwa "not budgeted" isipokuwa hapo tu mkoa fulani kule kanda ya ziwa ndipo mfumo ulipokubali.
 
Kwanini ulikaa miaka 10 bila kupanda daraja mzee uliwezaje? Mimi kaka yangu hakupandishwa daraja akaacha na kazi.
 
Kwanini usingeenda utumishi dodoma
 
kwanini miaka 10 wasikupandishe daraja, tatizo lilikua nini
 
Hili sina uzoefu nalo. Ila sidhani kama scores zina mchango katika kupanda
 
Hivi vikwazo vya not budgeted,no designation mnavikwepa vipi?mana kila taasisi tena ambayo unafahamu kabisa ina uhitaji wa mtaalam wa kada yako,bado mfumo una goma.

Mnavukaje hichi kiunzi wakuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…