HOJA Wataalamu wa kipengele cha uhamisho ndani ya ESS naombeni msaada mnivushe hapa

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Ombi lako lina muda gani tangia lifike utumishi.
Ushauri wangu
PLAN A
wewe rudi kamalizie shule huku kila siku ukipitia page yako ya ESS siku barua ikitoka tu print chap andika barua ya kughairi chuo nenda karipoti ofisi mpya. Fanya kazi mwaka mmoja kumbuka utakuwa na barua yenye kichwa cha habari KUAZIMWA hivyo kuwa mpole wakikupa barua ya kukuthibitisha tu, omba ruhusa ukamalizie masomo yako.
PLAN B
Usirudi kabisa shule andika barua ya kughairi masomo. Baada ya hapo anza kufuatilia Dodoma. Kawaida wanasema ni siku 21. Lakini uzoefu unaonesha kibali kutoka huchukua miezi 6 hadi mwaka mmoja kwa watu wa kawaida kama wewe na mimi.
NB
Kwa hatua ya ombi lako lilipofikia hapo unapotoka umepewa ruhusa na unakoenda umepewa umekubaliwa basi utumishi hawana kipingamizi chochote unless labda ukose vigezo kama vile muda wa kazini n.k
Tuendelee kuombeana wote tuko safarini
ALL THE BEST
 
Sijaelewa hiyo plan A,, barua kuwa na kichwa Cha habari KUAZIMWA kivipi..?

NB, umezungumzia labda kukosa vigezo kama vile muda wa kazini, BUT me najua kama muda wa kazini haukidhi vigezo basi hata mfumo haukuruhusu uweze kuomba uhamisho huo. Labda kama ulimaanisha vingenivyo basi ongezea nyama mkuu tufaidike wote
 
Kama huna vigezo ESS haiwezi kukuruhusu utume maombi.

Ila asante, Nimekupata.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Barua anayosubiri itakuja na kichwa cha habari, YAH:KIBALI CHA KUAZIMWA na sio KIBALI CHA UHAMISHO. Barua hiyo itamuelekeza pia kuwa atakuwa kwenye matazamio kwa muda wa mwaka mmoja na endapo taasisi husika haitaridhishwa na utendaji wake atarudishwa kwenye taasisi aliyotoka.
 
Hiyo inatokana au kwa sababu yuko masomoni, AU kwa ujumla vibali vyote vya uhamisho vinaelekeza hivyo..?
 
Umesema uzoefu wako unaonyesha kibali uchukua miezi 6 hadi mwaka mmoja. Je, barua ya kukubaliwa taasisi X haiwezi kuexpire na wao kuamua kumpa nafasi mtu mwingine?
 
Hiyo inatokana au kwa sababu yuko masomoni, AU kwa ujumla vibali vyote vya uhamisho vinaelekeza hivyo..?
Hii hutokea unapoomba uhamisho unaohusisha kubadili mamlaka ya ajira/kada, mfano uliomba kutoka Halmashauri kwenda TFS
 
Hii hutokea unapoomba uhamisho unaohusisha kubadili mamlaka ya ajira/kada, mfano uliomba kutoka Halmashauri kwenda TFS
Vipi ikiwa labda umetoka Taasisi to Taasisi. Let say TANAPA to TFS..?
 
Vipi ikiwa labda umetoka Taasisi to Taasisi. Let say TANAPA to TFS..?
Hizo ni mamlaka mbili tofauti za ajira,kwa hiyo utaazimwa na baada ya mwaka utathibitishwa au kurudishwa ulipotoka kama mwajiri mpya hataridhishwa na utendaji wako.
 
Hizo ni mamlaka mbili tofauti za ajira,kwa hiyo utaazimwa na baada ya mwaka utathibitishwa au kurudishwa ulipotoka kama mwajiri mpya hataridhishwa na utendaji wako.
Halafu uhamisho kamili au wa Moja kwa Moja unakuwaje mkuu. Endelea kutupa elimu mkuu🙏
 
Halafu uhamisho kamili au wa Moja kwa Moja unakuwaje mkuu. Endelea kutupa elimu mkuu🙏

Baada ya mwaka utaandika barua ya kuomba uhamishiwe moja kwa moja au urudishwe kwa mwajiri wako wa zamani. Hizi ni formality tu lakini unless mwajiri wako mpya umsumbue aamue kuomba urudi ulikotoka
 
Baada ya mwaka utaandika barua ya kuomba uhamishiwe moja kwa moja au urudishwe kwa mwajiri wako wa zamani. Hizi ni formality tu lakini unless mwajiri wako mpya umsumbue aamue kuomba urudi ulikotoka
Sawa mkuu, kumbe mambo ndvyo yanavyokuwa.. Nime-gain kitu muhimu hapa👍
 
Hizo ni mamlaka mbili tofauti za ajira,kwa hiyo utaazimwa na baada ya mwaka utathibitishwa au kurudishwa ulipotoka kama mwajiri mpya hataridhishwa na utendaji wako.
hapo sijakuelewa mtaalam, yani mtu umeomba transfer, badala ya kupewa ya barua ya UHAMISHO, utapewa barua ya KUAZIMWA? why? so far kila ninae fahamu aliewahi kuhama barua yake ina heading ya UHAMISHO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…