HOJA Wataalamu wa kipengele cha uhamisho ndani ya ESS naombeni msaada mnivushe hapa

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Kabisa Mimi naona inawezekana sababu kuu ni ule mkeka ambao aukuwa official hivyo wameamua ku reject waliotumia
Yaani wametuacha njia panda tunaspeculate tu. Mimi niliomba vacancy hata kabla ya huo mkeka sijauona.
 
Yaani wametuacha njia panda tunaspeculate tu. Mimi niliomba vacancy hata kabla ya huo mkeka sijauona.
Mkuu, wewe Umejibiwa tarehe ngapi, kuwa Rejected.

Na vacancy yako ilikuwa Auto au walipitisha Taasisi husika..?

Pia ombi lako lilikaa siku ngapi hadi kujibiwa..?
Asante
 
Nafikiri huenda hii ikawa ndio sababu, niliiwaza pia. Japo niliwapigia simu utumishi wakasema kitu kikubwa wanachoangalia wao hasa ni ikama.

Kwa namna hii ndio maana watu wanahama kiharamia au kuacha kazi.
 
Mkuu, wewe Umejibiwa tarehe ngapi, kuwa Rejected.

Na vacancy yako ilikuwa Auto au walipitisha Taasisi husika..?

Pia ombi lako lilikaa siku ngapi hadi kujibiwa..?
Asante
Nimejibiwa tarehe 1 juzi, vacancy ilikua approved na destination institution.

Ombi limekaa miezi mitatu na siku 4
 
Nafikiri huenda hii ikawa ndio sababu, niliiwaza pia. Japo niliwapigia simu utumishi wakasema kitu kikubwa wanachoangalia wao hasa ni ikama.

Kwa namna hii ndio maana watu wanahama kiharamia au kuacha kazi.
Walisema ni Ikama ya wapi, unakotoka au unakokwenda..?
 
Hizi "Rejected" zimekuwa nyingi hata watu wa nje wasiokuwepo humu JF tunawasikia.
Sasa zile nafasi za kuhamia zote zile zitajazwa na kina nani kama watu wanakosa

Utumishi tuoneeni huruma hizo taasisi zenye Maokoto tunazihitaji hebu punguzeni masharti ambayo hata watumishi hawayajui, Muda mwingine Sheria zinafaa kupindishwa ili kupisha maslahi ya Umma jamani😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭
 
Upo sahihi...wengi wenu humu wanaamini auto accept ni kigezo Cha kukosa ,kitu ambacho c kweli
 
Shida kubwa ninayoiona ni kule mtu anakotoka. Mkurugenzi anaweza akakwambia nimeshapitisha anakuchekea kabisa na wewe ukaona imeshapita lakini kwenye kupitisha huko ametoa comment gani.
Mwingine anapitisha lakini comment yake anayoweka inakuwa genuine mpaka utumishi wakiangalia wanaamua wasikutoe wakuache hapo hapo.
Lakini tujue pia hawa wakuu wa taasisi na wakurugenzi wanakuwa na vikao vyao kila mwaka na kwenye hivyo vikao wanalalamika sana kuhusu uhamisho kwamba watu wanakimbia hivyo ufanisi wa taasisi unapungua. Mfano sasa hivi mtumishi kuhama kutoka mkoa wa Lindi labda mganga wako awe mzuri sana au agizo litoke moja kwa moja kwa katibu mkuu.
Haya malalamiko yanawafanya utumishi waogope pia kuhamisha watu kiholela na mwisho wa siku ndio hizo REJECTED
 
Nakubali kweli kabisa maoni ya kule unapotoka letter of no objections ndio inawaponza wengi
 
Hapo kwenye maoni ya unapo Toka nakubali wewe unafurahi amepitisha kumbe kaandika Nileteeni mbadala
 
Sasa hapo tunafanyaje kuama ni jambo la kawaida wewe mtu amesha kaa Mika zaidi ya 10 Bado
 
Kabisa aisee Sasa hapo duh hatari sana
Miaka yangu 10 ndani ya utumishi wa umma nimeshuhudia mengi sana na mimi mwenyewe ni muhanga wa comment mbaya za waajiri. Nikiwa mwajiriwa wa halmashauri moja niliandika barua ya kuomba kazi TAEC. Ile barua mkuu wangu wa idara alicomment HE HAS NO QALIFICATIONS TO HANDLE THE APPLIED POST
Mkuu waidara yule alikuwa ana miezi mitatu tu hanijui jina wala sura yangu kwanza nilikuwa siripoti kwake wala mimi sikuwa Headquater kwahiyo hatufahamiani. Sijui kwanini alikuwa na roho mbaya namna ile.
 
Yaani wametuacha njia panda tunaspeculate tu. Mimi niliomba vacancy hata kabla ya huo mkeka sijauona.
Kila mwaka wa fedha unapoanza huwa na mkeka wake, na wengi huomba kupitia mikeka hiyo hiyo na baadhi hupata na wengine hukosa. Kwani mkeka wa mwaka huu wa fedha umekuwaje? au hawakutaka muupate?
 
Hivi Moderator na Maxence Melo mwenye JF yake wanaufuatilia kweli huu Uzi...?
Naona Kuna umuhimu kabisa wa kuupeleka viral kwenye majukwaa mengine huko Instagram na Facebook ili habari iwafikie na wahusika.
Sasa watumishi mpaka wanalia hivi na kuwapigia magoti UTUMISHI...!!
Utumishi huruma ni muhimu jamani toeni vibali kwa watumishi. Hii ina athirinsana utendaji kazi kazini..
 
so kwenye mfumo aliomba kwenye transfer request ama vacancy request???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…