Tuna mchango wetu katika kujaribu kuleta amani ya Congo, ingawa ni changamoto
TOKA MAKTABA :
29 January 2024
VITA MASHARIKI YA CONGO: Kikosi Kipya cha battalian ya Kitanzania Kilichopo Kivu Kaskazini Kikiwa na Mamlaka ya Kulazimisha amani
View attachment 3214140
Kikosi kipya cha wanajeshi wa Tanzania kimetumwa katika jimbo la Kivu Kaskazini lililokumbwa na vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kama kikosi cha pili cha ujumbe wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Kikosi cha Tanzania kitachukua nafasi ya jeshi la kikanda la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki EAC na kuchukua jukumu la kushambulia, kulingana na vyanzo vya kijeshi.
"Wanajeshi wa Tanzania wanawasili ili kuongeza nguvu ya askari wa SADC ambao wana mamlaka ya kulazimisha waasi wakubali amani ," alisema Luteni Kanali Guillaume Ndjike, msemaji wa gavana wa kijeshi wa Kivu Kaskazini.
“Uko pale kupigana na adui, waasi wa M23. Haupo kwa doria za jiji au kufahamiana na watu wa Kongo. Tuko hapa kushughulikia lengo letu,” alisema Meja Jenerali Monwabisi Dyakopu wa Afrika Kusini SADF mkuu wa kikosi cha nchi wanachama wa SADC, katika hotuba yake ya kuwaribisha.
Wanajeshi hawa wa SADC, wakiwa na mamlaka ya kushambulia, watachukua nafasi zilizoachwa na jeshi la kikanda la EAC (Burundi, Sudan Kusini, Kenya na Uganda) kama ilivyoamuliwa na serikali iliyotaja kutoridhika na kuendelea kuwepo uasi katika maeneo yaliyovamiwa M23 na kutokuwa na utulivu.
Wakati huo huo, kikosi cha Afrika Kusini cha SADC ambacho kilikuwa cha kwanza kuwasili Goma Desemba 2023, hivi karibuni kilishambuliwa na kundi la waasi la M23.
Kutumwa kwa wanajeshi wa SADC mashariki mwa DRC kuliidhinishwa wakati wa Mkutano wa 43 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali huko Luanda, Angola.
Kikosi hicho kipya kitaundwa na wanajeshi kutoka Malawi, Afrika Kusini na Tanzania kufuatia kuondolewa kwa wanajeshi 89 wa mwisho wa Kenya wa Jeshi la Kanda ya EAC ambao waliacha ardhi ya Kongo Alhamisi Desemba 21 kupitia Goma