Kusini kampeni ashamaliza?Chuma kipo dodoma kimetulia waodhani meli ya mgiriki itatia nanga watasubiri wao
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kusini kampeni ashamaliza?Chuma kipo dodoma kimetulia waodhani meli ya mgiriki itatia nanga watasubiri wao
Ni faida😂😂😂 unazungumziaje na huku Venezuela je Maduro akiondoka ni faida au hasara?
Ni jambo jema wakatolea taarifa. Huu uvumi unanifanya nikose raha kabisa. Yaani hata sielewi kwa nini.
Wanaondoa stress
Hii nchi ukitaka kila mtu ajue habari,ieneze kwanza kwa chinichini kama fununu.
Watu wanapenda sana umbea.
Dikteta aondolewapo ni faida kwa dunia.😂😂😂 unazungumziaje na huku Venezuela je Maduro akiondoka ni faida au hasara?
AiseeeNdiyo shida ya kumtegemea mtu mmoja kufanya maamuzi ya kila kitu.
Sasa mtu huyo mwenye kufanya maamuzi ndiyo huyo labda hajiwezi kwa sasa. Nani aseme?
Watanzania ni watu wa ajabu sana, embu ona issue ya umeme ukikatwa wanashangilia, ukirudishwa wanashangilia! Sijui huwa wanapenda nini.Si mlikuwa mnamtukana kuwa kila siku anataka aonekane yeye tu kwenye tv? Juzi tu hapa alikuwa huko lindi kwenye ziara live tbc mkasema hamuangalii, leo mnamtaka mumuone?
Ni kweli MTAZAMO, kapotea siku mbili tuu maneno mengi ooh yuko wapi mtukufu, mara ooh tuambiwe ukweli.Alafu baadae unawaona makanisani, misikitini!! Mkemea maovu hukemea kila uovu. Hao wanaharakati wanataka wao tu watendewe haki lakini haki za mahasimu wao wanataka hukumu hata za kufa kwa chuki tu!
Kwani mpaka sasa hajaonekana hadharani kwa miezi mingapi
Akionekana kila siku shida asipoonekana shida.Mbona kule Nigeria buhari anaweza kukaa hata miezi 3 bila kujulikana aliko
Si mlikuwa mnamtukana kuwa kila siku anataka aonekane yeye tu kwenye tv? Juzi tu hapa alikuwa huko lindi kwenye ziara live tbc mkasema hamuangalii, leo mnamtaka mumuone?
Naunga mkono hoja, kunapotokea sintofahamu yoyote kuhusu hali ya rais wetu, wananchi tunapaswa kuelezwa.Heshima kwenu wakuu,
Kuna habari zinasambaa kwamba Rais wa Tanzania John Magufuli anaumwa wengine wanasema amekatiza Ziara huko Kusini ili kushughulikia Masuala mengine ya Kitaifa. Hili sina tatizo nalo.
Kinachoniumiza na kunitatiza ni kuona Taasisi ya Rais akiwemo Msemaji Mkuu wa Ikulu na Msemaji wa Serikali kutokanusha au kuweka sawa habari hizi zinazosambaa na kuacha watu waendelee kumsema vibaya Rais wetu. Ukiacha uongo ukaendelea kuongelewa unageuka kuwa kweli.
Rais sio mali ya Ikulu bali ni mali ya Watanzania wote wa vyama vyote, dini zote, rangi zote na Makabila yote.
Msemaji wa Ikulu, Gerson Msigwa huwa ni mwepesi kukanusha na kutupa update za Rais. Ajitafakari kwa hili kama vipi ajiuzulu tu. Kazi imemshinda ya kuwatumikia Watanzania.
Tunapata wakati mgumu kuelewa.
Kama anaumwa sio jambo la kushtua pia kwani maradhi kwa binadamu ni kawaida, kama anaumwa ni haki wananchi wake wakajulishwa na maendeleo yake yakaelezwa kwa uwazi.
Tumefanya hivyo kwa Baba wa Taifa Nyerere, Askofu Mkuu Mwandamizi Yuda Thadeus Ruwa'ichi, Benjamin Mkapa, Kikwete alipoumwa Tezi dume akiwa Rais na wengine wengi.
Rais Kikwete afanyiwa upasuaji wa tezi dume Marekani, hali yake inaendelea vyema
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani. Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya...www.jamiiforums.com
Kama yu mzima wa afya tujulishwe ili roho zetu zitulie.
Ni haki yetu kujua Rais alipo na maendeleo yake sababu anaishi kwa kodi zetu na tulimchagua wenyewe ndio maana Televisheni ya Yaifa inamuonesha popote aendapo bure ili wananchi wajue anachofanya Rais wao.
Hata kama kapumzika Ikulu, hakuna sababu ya kuzua taharuki.
Tunajua Rais wetu anapenda mpira hasa timu ya Taifa, Jana timu yetu imeshinda na kufuzu Michuano ya CHAN, hatujaona anapongeza na kushangilia kama kawaida yake.
Hata Msemaji wa Ikulu hajatuma picha akiangalia mpira wa watoto wake kama kawaida yao.
Tunamtaka Rais wetu.
Asanteni sana
TUJIKUMBUSHE;
"Taifa Stars wameipa heshima nchi yetu. Leo nimeona mpira, sio ule wa siku za nyuma."- Rais Dkt Magufuli akifurahia Tanzania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika #AFCON2019
View attachment 1238150
Hiyo taharuki iko wapi? mbona watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaidaLakini Mkuu kuna sintofahamu na taharuki kwa sasa,kwa nn tusijuzwe tuelewe yu wapi Rais wetu,Kuna maneno mengi sana ya mafumba ambayo yanaendelea kwenye mitandao ya kijamii tujuzwe tufahamu!