Unavyoishi na watu pindi unapopata matatizo ndio muda muafaka wa kupata mrejesho. Haya ni automatic by nature. Kama kuna mazuri kafanya huo ni wajibu wake, ila hilo halizuii watu kuonyesha hisia zao, hasa kama hakuwatendea sawa. Kama wewe unaona ana mazuri muombee maana hiyo ni haki yako, sio lazima na wengine nao wafanye utakavyo ww.
Kuna habari zinasambaa kwamba Rais wa Tanzania John Magufuli anaumwa wengine wanasema amekatiza Ziara huko Kusini ili kushughulikia Masuala mengine ya Kitaifa. Hili sina tatizo nalo.
Kinachoniumiza na kunitatiza ni kuona Taasisi ya Rais akiwemo Msemaji Mkuu wa Ikulu na Msemaji wa Serikali kutokanusha au kuweka sawa habari hizi zinazosambaa na kuacha watu waendelee kumsema vibaya Rais wetu. Ukiacha uongo ukaendelea kuongelewa unageuka kuwa kweli.
Rais sio mali ya Ikulu bali ni mali ya Watanzania wote wa vyama vyote, dini zote, rangi zote na Makabila yote.
Msemaji wa Ikulu, Gerson Msigwa huwa ni mwepesi kukanusha na kutupa update za Rais. Ajitafakari kwa hili kama vipi ajiuzulu tu. Kazi imemshinda ya kuwatumikia Watanzania.
Tunapata wakati mgumu kuelewa.
Kama anaumwa sio jambo la kushtua pia kwani maradhi kwa binadamu ni kawaida, kama anaumwa ni haki wananchi wake wakajulishwa na maendeleo yake yakaelezwa kwa uwazi.
Tumefanya hivyo kwa Baba wa Taifa Nyerere, Askofu Mkuu Mwandamizi Yuda Thadeus Ruwa'ichi, Benjamin Mkapa, Kikwete alipoumwa Tezi dume akiwa Rais na wengine wengi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani. Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya...
www.jamiiforums.com
Kama yu mzima wa afya tujulishwe ili roho zetu zitulie.
Ni haki yetu kujua Rais alipo na maendeleo yake sababu anaishi kwa kodi zetu na tulimchagua wenyewe ndio maana Televisheni ya Yaifa inamuonesha popote aendapo bure ili wananchi wajue anachofanya Rais wao.
Hata kama kapumzika Ikulu, hakuna sababu ya kuzua taharuki.
Tunajua Rais wetu anapenda mpira hasa timu ya Taifa, Jana timu yetu imeshinda na kufuzu Michuano ya CHAN, hatujaona anapongeza na kushangilia kama kawaida yake.
Hata Msemaji wa Ikulu hajatuma picha akiangalia mpira wa watoto wake kama kawaida yao.
Tunamtaka Rais wetu.
Asanteni sana
TUJIKUMBUSHE;
"Taifa Stars wameipa heshima nchi yetu. Leo nimeona mpira, sio ule wa siku za nyuma."- Rais Dkt Magufuli akifurahia Tanzania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika #AFCON2019 View attachment 1238150
Ni kweli MTAZAMO, kapotea siku mbili tuu maneno mengi ooh yuko wapi mtukufu, mara ooh tuambiwe ukweli.
Wakati Ben Saanane miaka mitatu sasa hajaonekana wala nguo zake hazijaokotwa. Azory miaka miwili katoweka kama ndege ya Malaysia.
Mie naamini sana katika maombi, najiuliza hivi yule Mkurugenzi wa Nachingwea kama hana kosa na hakusikilizwa bali alipokea matusi hadharani, jee akiwa mtu wa maombi na akawa kaomba kwa Mungu wake amlipie uonevu ule itakuwaje? Sio yeye tuu wako wengi kama yeye maombi yao hayawezi kutimia kwa sababu Mungu anaona kanunua Airbus? Au Bombardier?
Tafakari!
Kama ni kwelj Mh Rais wetu mpendwa anaumwa au anatatizo lolote la kiafya binafsi namuombea sala njema apone haraka aje aendelee kulitumikia taifa. Km si kweli basi mliomzushia magonjwa yawarudie ninyi.
Ni kweli mkuu!
Mi nimeona kule twitter,maria sarungi,zitto kabwe na account yake ya kigogo na hata yule mama fyatu karume woote wameshangilia uvumi ule ,
Lakini bi vema kumjua adui yako kabla.
Yaani hao uliowataja huo utofauti wake na wao ni mpaka apate tatizo ndio ifahamike? Kwani yeye anawapenda hao uliowataja mpaka wao waonyeshe kumpenda? Tena ni vyema hao walioonyesha hisia zao kuliko wanaccm wanaotamani huo uvumi uwe kweli.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.