Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Status
Not open for further replies.
Kuna wahuni na baadhi ya wanasiasa tuliowaheshimu wameonesha kushangilia tetesi hizo! Tabia za kichawi kabisa hata kama huwangi usiku.

Rais wetu ametenda mambo makubwa na yenye manufaa kuliko madhaifu mnayomhukumu nayo na kumtakia mabaya.

Serikali itoe taarifa rasmi badala ya kuacha redio za mbao ziendelee kulisha jamii chuki na tabia mbaya kabisa kuombeana mabaya kwa matamanio binafsi.

Ukweli haupiganiwi bali unajipigania.
Kwa hiyo wewe unabagua chuki? Kuchukia watu kwa misingi ya kiitikadi haukuoni wewe? Eti hakuna kupeleka fedha za miradi katika majimbo ya wapinzani na hauoni kuwa huo ni ubaguzi na kupanda chuki? Mbona unakuwa mjinga kupita kiasi?
 
Lakini Mkuu kuna sintofahamu na taharuki kwa sasa,kwa nn tusijuzwe tuelewe yu wapi Rais wetu,Kuna maneno mengi sana ya mafumba ambayo yanaendelea kwenye mitandao ya kijamii tujuzwe tufahamu!
Sababu Kigogo amesema. Nothing more. Hakuna lingine lolote. Hivi Kigogo yeye yuko perfect?
 
Hivi kikwete na walivokuwa wanaumwa watu walishangilia hivihivi? Kama hawakushangilia basi kuna tatizo.
Kuna wahuni na baadhi ya wanasiasa tuliowaheshimu wameonesha kushangilia tetesi hizo! Tabia za kichawi kabisa hata kama huwangi usiku.

Rais wetu ametenda mambo makubwa na yenye manufaa kuliko madhaifu mnayomhukumu nayo na kumtakia mabaya.

Serikali itoe taarifa rasmi badala ya kuacha redio za mbao ziendelee kulisha jamii chuki na tabia mbaya kabisa kuombeana mabaya kwa matamanio binafsi.

Ukweli haupiganiwi bali unajipigania.
 
Wakati mwingine si serikali tu, hawa watu ni marafiki, washirika, waumini, majirani zetu. Tukemeane kwenye ujinga kama tunavyolipuka viongozi wakikosea.

Wale waliokuwa wanalaani waliokuwa wakimbeza Lissu baada ya yale matatizo wengine ndio wanashangilia hizi tetesi na hata huoni wakikemea kama wanavyojinasibu kama watetezi wa haki. Tena wengine wanataka Urais! Shame!

Huyo Lissu matatizo yaliyompata kuna watu walifurahia tena waziwazi, na hukajawahi kutolewa karipio lolote na wala kwako haijawahi kuwa tatizo, sasa unashangaa nini hivi leo kwa jambo linalofumbiwa macho likimpata mpinzani? Juzi Lissu amesema kabisa hawezi kurudi mpaka ahakikishiwe usalama wake, wahusika wamejibu lolote? Mbona hukuonyesha kuumizwa roho kama huu uvumi tu? Ukiwa na mahaba niue ni vyema ukakubaliana na hiyo hali maana kila mtu anaweza kupata matatizo.
 
Ni jambo jema wakatolea taarifa. Huu uvumi unanifanya nikose raha kabisa. Yaani hata sielewi kwa nini.
Naona huko Twitter ndio kabsaa.Serikali izime mitandao ya kijamii mpaka hapo watakapokuwa tayari kutupa taarifa.
 
Kama data (CPU) zilizoibiwa ofisini kwa DPP zinamuhusisha Rais kwa namna moja au nyingine, ni lazima akatishe ziara na kurudishwa Zero Ground kiusalama..!!
 
Kuna wahuni na baadhi ya wanasiasa tuliowaheshimu wameonesha kushangilia tetesi hizo! Tabia za kichawi kabisa hata kama huwangi usiku.

Rais wetu ametenda mambo makubwa na yenye manufaa kuliko madhaifu mnayomhukumu nayo na kumtakia mabaya.

Serikali itoe taarifa rasmi badala ya kuacha redio za mbao ziendelee kulisha jamii chuki na tabia mbaya kabisa kuombeana mabaya kwa matamanio binafsi.

Ukweli haupiganiwi bali unajipigania.
Mliposhangilia lissu alipo pigwa risas kama mnyama mlikuwa mnashangilia kula nyama sio, mmelikiroga wenyewe, lazima mlinywe
 
Anza kumfundisha huyo ambaye unataka tumnenee mema. Mwambie atende haki.
Alafu baadae unawaona makanisani, misikitini!! Mkemea maovu hukemea kila uovu. Hao wanaharakati wanataka wao tu watendewe haki lakini haki za mahasimu wao wanataka hukumu hata za kufa kwa chuki tu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom