Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Status
Not open for further replies.
Kaka si wewe, nasikia machozi yananitoka kwa rais anayeipenda nchi yake halafu, wanatokea watu wa aina hii kuleta maneno ya uzushi na kejeli kubwa hivi. Hata kama kuna shida si wasubiri protocal zifanye kazi?!!!
Ni jambo jema wakatolea taarifa. Huu uvumi unanifanya nikose raha kabisa. Yaani hata sielewi kwa nini.
 
Jana watu wamekesha twitter 😂 nusu iliyopita kigogo kuvuruga tena watu. Watu wamevurugwa haswa, comments zinafutwa,nyuzi zinayeyuka.
 
Alafu baadae unawaona makanisani, misikitini!! Mkemea maovu hukemea kila uovu. Hao wanaharakati wanataka wao tu watendewe haki lakini haki za mahasimu wao wanataka hukumu hata za kufa kwa chuki tu!
Ni kweli MTAZAMO, kapotea siku mbili tuu maneno mengi ooh yuko wapi mtukufu, mara ooh tuambiwe ukweli.
Wakati Ben Saanane miaka mitatu sasa hajaonekana wala nguo zake hazijaokotwa. Azory miaka miwili katoweka kama ndege ya Malaysia.
Mie naamini sana katika maombi, najiuliza hivi yule Mkurugenzi wa Nachingwea kama hana kosa na hakusikilizwa bali alipokea matusi hadharani, jee akiwa mtu wa maombi na akawa kaomba kwa Mungu wake amlipie uonevu ule itakuwaje? Sio yeye tuu wako wengi kama yeye maombi yao hayawezi kutimia kwa sababu Mungu anaona kanunua Airbus? Au Bombardier?
Tafakari!
 
Huyu wetu haiwezekani akae miezi mitatu bila kuonekana. Hata wiki moja itazua taharuki kwasababu yeye mwenyewe si MTU wa kujifungia ndani kama mwali.
Kwani mpaka sasa hajaonekana hadharani kwa miezi mingapi

Akionekana kila siku shida asipoonekana shida.Mbona kule Nigeria buhari anaweza kukaa hata miezi 3 bila kujulikana aliko
 
Si mlikuwa mnamtukana kuwa kila siku anataka aonekane yeye tu kwenye tv? Juzi tu hapa alikuwa huko lindi kwenye ziara live tbc mkasema hamuangalii, leo mnamtaka mumuone?

Kwa taarifa yako hata mleta mada sio kammiss bali anachimba tu ili apate taarifa juu ya huu uvumi. Alikuwa anatukanwa na nani, acheni ujinga, watu walisema kweli iweje awe anaonyeshwa kila siku yeye, tena wakati wa kazi huku akiwa amepiga marufuku bunge live kuwa watu wafanye kazi? Hamna wa kummiss labda aliowapa maisha.
 
Huenda kupanda airbus kuelekea st Thomas uk
 
Naunga mkono hoja, kunapotokea sintofahamu yoyote kuhusu hali ya rais wetu, wananchi tunapaswa kuelezwa.

Hata JK alipoanguka julwaani tulielezwa ni tatizo dogo tuu la fatigue amepumzika na yuko ok.

Hata baada ya tetemeko la Bukoba, kina sisi tulihoji ukimya wa rais. Rais sio mtu tuu huyu ni taasisi.
P
 
Lakini Mkuu kuna sintofahamu na taharuki kwa sasa,kwa nn tusijuzwe tuelewe yu wapi Rais wetu,Kuna maneno mengi sana ya mafumba ambayo yanaendelea kwenye mitandao ya kijamii tujuzwe tufahamu!
Hiyo taharuki iko wapi? mbona watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…