Kwa hiyo wewe unabagua chuki? Kuchukia watu kwa misingi ya kiitikadi haukuoni wewe? Eti hakuna kupeleka fedha za miradi katika majimbo ya wapinzani na hauoni kuwa huo ni ubaguzi na kupanda chuki? Mbona unakuwa mjinga kupita kiasi?Kuna wahuni na baadhi ya wanasiasa tuliowaheshimu wameonesha kushangilia tetesi hizo! Tabia za kichawi kabisa hata kama huwangi usiku.
Rais wetu ametenda mambo makubwa na yenye manufaa kuliko madhaifu mnayomhukumu nayo na kumtakia mabaya.
Serikali itoe taarifa rasmi badala ya kuacha redio za mbao ziendelee kulisha jamii chuki na tabia mbaya kabisa kuombeana mabaya kwa matamanio binafsi.
Ukweli haupiganiwi bali unajipigania.