Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Status
Not open for further replies.
Raisi lazima ategemewe ktk nchi iwe isiwe unajua gharama za kumchagua raisi mpya endapo litatokea la kutokea?(japo siombei)
Raisi akiondoka leo basi makamu wa raisi anaapishwa. Hivi huwa unasoma hata katiba kweli?
 
Kuna wahuni na baadhi ya wanasiasa tuliowaheshimu wameonesha kushangilia tetesi hizo! Tabia za kichawi kabisa hata kama huwangi usiku.

Rais wetu ametenda mambo makubwa na yenye manufaa kuliko madhaifu mnayomhukumu nayo na kumtakia mabaya.

Serikali itoe taarifa rasmi badala ya kuacha redio za mbao ziendelee kulisha jamii chuki na tabia mbaya kabisa kuombeana mabaya kwa matamanio binafsi.

Ukweli haupiganiwi bali unajipigania.
watu wakiamua mambo yao hata utembee na uzio wa chuma wana kumaliza tu. na uzio wote ule anaotembea nao haikufua dafu?
Damu ya kijana yule wa makambako itamwandama popote alipo.
 
Kushangilia ni kosa?
Ni kweli mkuu!
Mi nimeona kule twitter,maria sarungi,zitto kabwe na account yake ya kigogo na hata yule mama fyatu karume woote wameshangilia uvumi ule ,
Lakini bi vema kumjua adui yako kabla.
 
Ni vizuri jambo hili likawekwa wazi.wako watu wanasema kila Mara rais huzidiwa na taarifa huwekwa siri.wananchi waelezwe wazi nini kinamsumbua rais wao mpendwa.
 
Watu wa nchi hii wajinga sana. Sijui kwanini nimezaliwa nchi hii. Akionekana kila siku mnasema rais anapenda media. Mnapiga sana kelele kusema hata jambo dogo rais anapenda attension media kibao. Leo hajaonekana siku mbili tu mnapiga kelele sijui haonekani mlienda ikulu mkamkosa? Au mnataka tena aonekane kwenye media
 
Kama kuna matatizo tuambiwe kwani yeye ndo wa kwanza kupata matatizo?
Kaka si wewe, nasikia machozi yananitoka kwa rais anayeipenda nchi yake halafu, wanatokea watu wa aina hii kuleta maneno ya uzushi na kejeli kubwa hivi. Hata kama kuna shida si wasubiri protocal zifanye kazi?!!!
 
Raisi akiondoka leo basi makamu wa raisi anaapishwa. Hivi huwa unasoma hata katiba kweli?
Nikuulize wewe unasoma katiba? Unajua makamu wa raisi anakaa kwa muda gani kabla ya kuitisha uchaguzi mwingine kumtafuta raisi atakayerithi wadhifa wa raisi aliyeondoka?
 
Kwani mpaka sasa hajaonekana hadharani kwa miezi mingapi

Akionekana kila siku shida asipoonekana shida.Mbona kule Nigeria buhari anaweza kukaa hata miezi 3 bila kujulikana aliko
Buhari alishapotea mpaka wakazusha kuwa Buhari alifariki wakamweka mtu anayefanana naye akalie kiti. Nakumbuka ilikuwa kazi sana kuwashawishi wanigeria.

images.jpeg.jpg

jubril.jpg
 
Tusiwe watu wa matukio, anaumwa au haumwi hakuna sababu ya kuelezwa...
 
Lakini Mkuu kuna sintofahamu na taharuki kwa sasa,kwa nn tusijuzwe tuelewe yu wapi Rais wetu,Kuna maneno mengi sana ya mafumba ambayo yanaendelea kwenye mitandao ya kijamii tujuzwe tufahamu!
Hiyo taharuki kaleta nani?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom