Leo tuwache jazba, kejeli, matusi na ujinga. Hii kwa pande zote mbili, zinzoona DP World haifai na zinazoona DP World inafaaa tujadiliane kiustaarabu tuone "options " zetu ni zipi, zile zenye faida tuishauri serikali izifate, zile zisizo na faida tuishauri serikali isizifate.
Kama una jibu au majibu sawa, kama hauna majibu bali una swali lako pia, uliza tulijadili. Maswali na majibu yawe mafupi ili mjadala unoge.
Wale wa zamani tujikumbushe mijadala ya Jambo Frums ilivyokuwa inanoga na wale wa sasa wapunguze jazba.
Uongozi wa JF, @moderators tunahitaji muulinde huu uzi kwa uwepo wenu wa karibu, ili mjadala uende vizuri. Au nipeni u moderator wa mjadala huu tu ili niuendeshe inavyopaswa, mkiona siuendeshi kwa haki, mauodoa u miderator wangu.
Tuwe great thinkers ambao hata mtu atakaesoma huu mjadala aseme aaah, hyu ana point, aah huyu hili tumeliona.
Tuwe na maswali mengi ya kujiuliza lakini tujikite kwenye mada. Nalianzisha:
1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?