Watanzania tujiulize Maswali muhimu ya Kibiashara kuhusu bandari zetu kwa dunia ya leo

Watanzania tujiulize Maswali muhimu ya Kibiashara kuhusu bandari zetu kwa dunia ya leo

Wewe kaa pembeni huna akili ya kujadili vitu vikubwa,uwezo wako wakuchanganua mambo ni mdogo sana.
Kwa kipi wewe ulichokichanganua?

Kama unataka mjadara uwe mzuri na DPword tuione ya maana,

Utuambie share yetu kama nchi ni ngapi kwa mwezi ama kwa mwaka kwa mjibu wa mkataba?

Utuambie, ni lini mkataba utakoma?

Utuambie, kwa kuwa mkataba unamanufaa makubwa, kwa nini bandari za Zanzibar hazikuingizwa kwenye mkataba huu wenye mafaida kibao?

Utuambie, Ni kwa nini ziwe bandari zote za bara, nchi kavu na majini?

Kwa nini kwa nini kwa nini unashabikia mkataba unaowapa warabu milele yote?

Inasemekana kwamba, kwenye silabas zetu kumeingizwa lugha ya kiarabu, Hii ni kusema tayari tunaanza kuwa chini ya mwarabu au ni kujifunza lugha ambayo itaitawala Tz
 
Tinatakiwa kuelewana kwanza kuwa kilichoridhiwa na Bunge au kulichosainiwa na Serikali ni Mkataba au Makubaliano.
Je, kisheria kuna tofauti gani kati ya Mkataba na Makubaliano?
Baada ya kuelewana kwenye hiyo hoja ndio turudi kwenye vipengele.
Kimsingi huo Mkataba/Makubaliano tayari umeanza kutekelezwa kulingana na kile kifungu kinachozungumzia "entry into force".
 
1. Ni kweli DP World imetumia IGA ili kukwepa ushindani katika kitafuta mwekezaji?

2. Nani alisaini ule mkataba kwa upande wa Dubai? Na nani alishuhudia utiaji saini wa ule mkataba kwa upande wa Dubai?

3. Nini Wajibu wa Dubai katika mkataba ule wa IGA?

4. Kipi kingeathiri IGA endapo IGA ingetoa masharti ya muda kwa ujamla? Mfano "Mikataba yote itakayoungiwa katika HGA itakuwa renewables kila baada ya miaka 15 kama Tanzania itaona inafaa kuendelea na uwekezaji wa DP World katika eneo husika"

5. IGA inatoa mwanya kwa Tanzania kutafuta mwekezaji mwingine kwenye bandari zingine kama Tanga nk?

6. Kutokana na wizi wa madini uliokakithili nchini, 2017 Serikali aliamua kutunga sheria ya "Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Act, 2017 (No. 5 of 2017)." Na sheria hii ikitamka bayana kuwa migogoro yote itakayohusu mali asili za Tanzania basi kesi zake ziamuliwe katika mahakama zetu za ndani.

Sheria hii mpaka sasa inafanyakazi, Je! Ilikuwa ni sahihi kwa Bunge kuvunja sheria kupitisha IGA ambayo inakiuka sheria hii waliyotunga wenyewe ili migogoro itokayo ibuka kati ya DP WORLD na Tanzania ikatatuliwe S Afirca?

7. Kutokana na Bunge kukiuka sheria hii, inatosha kusema mkataba ule ni Batili?

Nipo kwenye usafiri actually, ila mengine yanakuja.
 
Unaambiwa mwekezaji walimuona tu kwenye maonesho pale Dubai basi wakampenda na wakagawa aendeshe bandari za bahari ya hindi ukanda wa Tanga hadi mtwara, na bandari za ziwa nyasa, tanganyika na victoria, hawa watu ni wapuuzi wa kiwango cha mwisho
 
Mkuu, hili la bandari si ni la kimuungano?
Linaweza kuwa ni la Muungano au si la Muungano, jilo halina ubishi.
Wakati TICTS wanasimamia bandari yetu hatukuwalaimisha wakasimamie na za Zanzibar, Zanzibar wakajitafutia kampuni za kuendesha bandari zao, hatukuwapinga.

Zanzibara tayari wana kampuni zinaendesha bandari na tayari wana kampuni ya KiOman imeshirikiana na Wahina wa[o hatua za awalai za kuwajengea bandari mpya kabisa.

Sasa tuwwalazimishe wao waache amaedeleo yao watusubiri sisi amabo bado bandari yetu tunaiendesha kizamani?

1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
 
Tinatakiwa kuelewana kwanza kuwa kilichoridhiwa na Bunge au kulichosainiwa na Serikali ni Mkataba au Makubaliano.
Je, kisheria kuna tofauti gani kati ya Mkataba na Makubaliano?
Baada ya kuelewana kwenye hiyo hoja ndio turudi kwenye vipengele.
Kimsingi huo Mkataba/Makubaliano tayari umeanza kutekelezwa kulingana na kile kifungu kinachozungumzia "entry into force".

Kilichokubaliwa na Bunge ni mkataba wa awali, kinachofuata hapo ni mikataba ya utekelezaji ambayo kimsingi mikataba hiyo itafuata msingi mama wa mkataba wa awali, ambao ndio ushahidi wa uwekezaji, na. Ndio maana watu tunapiga kelele sana wajirekebishe hatukatai uwekezaji lakini janja janja ndio hatutaki
 
Leo tuwache jazba, kejeli, matusi na ujinga. Hii kwa pande zote mbili, zinzoona DP World haifai na zinazoona DP World inafaaa tujadiliane kiustaarabu tuone "options " zetu ni zipi, zile zenye faida tuishauri serikali izifate, zile zisizo na faida tuishauri serikali isizifate.

Kama una jibu au majibu sawa, kama hauna majibu bali una swali lako pia, uliza tulijadili. Maswali na majibu yawe mafupi ili mjadala unoge.

Wale wa zamani tujikumbushe mijadala ya Jambo Frums ilivyokuwa inanoga na wale wa sasa wapunguze jazba.

Uongozi wa JF, @moderators tunahitaji muulinde huu uzi kwa uwepo wenu wa karibu, ili mjadala uende vizuri. Au nipeni u moderator wa mjadala huu tu ili niuendeshe inavyopaswa, mkiona siuendeshi kwa haki, mauodoa u miderator wangu.

Tuwe great thinkers ambao hata mtu atakaesoma huu mjadala aseme aaah, hyu ana point, aah huyu hili tumeliona.

Tuwe na maswali mengi ya kujiuliza lakini tujikite kwenye mada. Nalianzisha:

1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
Leo umeacha kushambulia wanaopinga mkataba? Maana Tangu awali wanaopinga kwako walikuwa Wahaini?
 
Leo tuwache jazba, kejeli, matusi na ujinga. Hii kwa pande zote mbili, zinzoona DP World haifai na zinazoona DP World inafaaa tujadiliane kiustaarabu tuone "options " zetu ni zipi, zile zenye faida tuishauri serikali izifate, zile zisizo na faida tuishauri serikali isizifate.

Kama una jibu au majibu sawa, kama hauna majibu bali una swali lako pia, uliza tulijadili. Maswali na majibu yawe mafupi ili mjadala unoge.

Wale wa zamani tujikumbushe mijadala ya Jambo Frums ilivyokuwa inanoga na wale wa sasa wapunguze jazba.

Uongozi wa JF, @moderators tunahitaji muulinde huu uzi kwa uwepo wenu wa karibu, ili mjadala uende vizuri. Au nipeni u moderator wa mjadala huu tu ili niuendeshe inavyopaswa, mkiona siuendeshi kwa haki, mauodoa u miderator wangu.

Tuwe great thinkers ambao hata mtu atakaesoma huu mjadala aseme aaah, hyu ana point, aah huyu hili tumeliona.

Tuwe na maswali mengi ya kujiuliza lakini tujikite kwenye mada. Nalianzisha:

1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
Leo umeacha kushambulia wanaopinga mkataba? Maana Tangu awali wanaopinga kwako walikuwa Wahaini?
 
Kwa kipi wewe ulichokichanganua?

Kama unataka mjadara uwe mzuri na DPword tuione ya maana,

Utuambie share yetu kama nchi ni ngapi kwa mwezi ama kwa mwaka kwa mjibu wa mkataba?

Utuambie, ni lini mkataba utakoma?

Utuambie, kwa kuwa mkataba unamanufaa makubwa, kwa nini bandari za Zanzibar hazikuingizwa kwenye mkataba huu wenye mafaida kibao?

Utuambie, Ni kwa nini ziwe bandari zote za bara, nchi kavu na majini?

Kwa nini kwa nini kwa nini unashabikia mkataba unaowapa warabu milele yote?

inasemekana kwamba, kwenye silabas zetu kumeingizwa lugha ya kiarabu, Hii ni kusema tayari tunaanza kuwa chini ya mwarabu au ni kujifunza lugha ambayo itaitawala Tz
Rubbish,
Ukisha weka neno "Inasemekana" ina maana umeleta maneno ya kwenye vijiwe vya kahawa.
 
Kilichokubaliwa na Bunge ni mkataba wa awali, kinachofuata hapo ni mikataba ya utekelezaji ambayo kimsingi mikataba hiyo itafuata msingi mama wa mkataba wa awali, ambao ndio ushahidi wa uwekezaji, na. Ndio maana watu tunapiga kelele sana wajirekebishe hatukatai uwekezaji lakini janja janja ndio hatutaki
Umeeleza vizuri sana mkuu. Wenzetu ndio wanakaza fuvu hawataki kukielewa hiki. Mkataba mdogo hauwezi kwenda kinyume na mkataba mama.
 
Ni ukurasa wa ngapi kwenye mkataba unaozungumzia masilahi ya Tanganyika?
Sijaona hilo kabisa, wala sijaona hata neno "Tanganyika", sidhani hata kama kuna nchi inayoitwa "Tanganyika" leo hii.

Hata Kimataifa utaingia na nchi nyingine mkataba au makubaliano na nchi isiyokuwepo?

Nakupa darsa dogo tu:

Ukiona kuna mkataba wowote unaohusisha nchi mbili zilizo wanachama wa Umoja wa Mataifa, (integovernment au Bilateral agreements)elewa kuwa huo mkataba unalindwa na sheria na maazimio ya Umoja wa Mataiafa. Usiwe na shaka, hata uwe na upendeleo kwa mmoja au una mnyima haki mmoja basi haki yake utapatikana kwa nguvu za Umoja wa Mataifa.
 
Ndugu Faiza mimi naona serikali ikae chini tena na hao DP World na kukubaliana terms zenye manufaa pande zote. Kama kuna mambo hayako sawa hadi tulipofikia basi yarekebishwe. Hakuna mtanzania kutoka CCM au upinzani anayeweza kuendesha bandari kwa ufanisi. JPM alipambana sana kuwabana bandarini ila hakuweza. Hawa DP nadhani ndo komesha ya mchwa waliopo bandarini. Jiulize kama CHADEMA huwa wanavurugana kwenye ishu ya viti maalum bungeni vipi kwa mfano wakipewa bandari? Yule Mama Tibaijuka aliyesema milioni 10 ni hela ya mboga itakuwaje akipewa usimamizi wa bandari? ILI KUONDOA LAWAMA BANDARI AENDESHE DP. Sisi tuchukue tu mgawo wetu. Marehemu Steve Jobs pamoja na kuwa mwanzilishi wa Apple Company ila wadau walishawahi kumtimua.
 
Msingi wa mkataba ni wakipuuzi sana
sawa, hayo ni mawazo yako, hatukupingi kwa mawazo yako.

1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
 
Leo umeacha kushambulia wanaopinga mkataba? Maana Tangu awali wanaopinga kwako walikuwa Wahaini?
Ndiyo.

Nataka kufahamu sababu a za wanaopinga ni nini kibiashara na kipi wanachokipinga.

mMaana mtu aki[pinga tu kitu ambacho hakipo na mimi nikianza kubisha nae, tunakuwa sote wenda wazimu, tunapingana hewa.

Ndiyyo kusudio la huu mjadala, tujielewe tunapingana au tunabisha nini.
 
Back
Top Bottom