Tindikali
JF-Expert Member
- Mar 26, 2010
- 2,086
- 2,823
Leo tuache jazba ? Unaomba poo ???Leo tuwache jazba, kejeli, matusi na ujinga. Hii kwa pande zote mbili, zinzoona DP World haifai na zinazoona DP World inafaaa tujadiliane kiustaarabu tuone "options " zetu ni zipi, zile zenye faida tuishauri serikali izifate, zile zisizo na faida tuishauri serikali isizifate.
Kama una jibu au majibu sawa, kama hauna majibu bali una swali lako pia, uliza tulijadili. Maswali na majibu yawe mafupi ili mjadala unoge.
Wale wa zamani tujikumbushe mijadala ya Jambo Frums ilivyokuwa inanoga na wale wa sasa wapunguze jazba.
Uongozi wa JF, @moderators tunahitaji muulinde huu uzi kwa uwepo wenu wa karibu, ili mjadala uende vizuri. Au nipeni u moderator wa mjadala huu tu ili niuendeshe inavyopaswa, mkiona siuendeshi kwa haki, mauodoa u miderator wangu.
Tuwe great thinkers ambao hata mtu atakaesoma huu mjadala aseme aaah, hyu ana point, aah huyu hili tumeliona.
Tuwe na maswali mengi ya kujiuliza lakini tujikite kwenye mada. Nalianzisha:
1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
FAIZA FOXY HUNA moral authority ya kuasa uchangiaji wa kistaarabu na staha hata siku moja..
Ni kinara wa thread za udini, kejeli, unyanyasaji na dhihaka.
Jina lako ni ubini na utambulisho wa mada zinazoshusha hadhi ya jamvi kama MNAONITAKA NJOONI HUKU MNITONGOZE.
Kwenye sakata la DP World umenywea ghafla kwa sababu umezidiwa hoja, umezidiwa matusi, dhihaka, na idadi ya wachangiaji wanaopinga mkataba; kila kitu kwenye mada hii umezidiwa.
Watanzania wengi huchukulia mambo kijuu juu na kusahau rekodi ya mtu, lakini kwa watu makini huwezi kuwapumbaza na ughafla wa maoni ya kistaarabu.
Again, wewe FAIZA FOXY of all the people, HUNA MORAL STANDING ya kuwa voice of reason hapa JF.