Watanzania tujiulize Maswali muhimu ya Kibiashara kuhusu bandari zetu kwa dunia ya leo

Unajua mipasho tu, empty head.
 
Chuki iko wapi zaidi ni kwamba huyu ajuza anatumika hivi kuna mtu ambae amempita kwa kufungua thread za kuhusu bandari humu jF?
Sijazihesabu, wewe zihesabu utuletee jibu.


Wakati unazihesabu, Sasa rudi kwenye mada. Achana na ajuza.

Akili kubwa inajadili maendeleo.
Akili ya kawaida inajadili matukio.
Akili ndogo (mbovu) inajadili watu.
 
Bandari za zanzibar hazimo kwa sababu wanasema kila mmoja anasimamia bandari zake
 
Jambo ni jepesi sema upande mmoja umezidiwa na sababu ni ile ile toka enzi za bwana(Transparency).

Hakuna anayepinga uwezekaji ata waje waarabu wainvest kila kona ya nchi hii hakuna anayepinga ila maswali ni haya: Je,mkataba au makubaliano kama wasemavyo ukomo wake lini?Je,kuna maelezo yoyote ya namna watanzania watapata kitu cha ziada tofauti na ilivyokuwa mwanzo kabla ya ujio wa hawa wazee mashariki ya kati
 
Aloo
 
Kwa nini unatumia nguvu nyingi kulazimisha watanzania wakubali hiyo Dp word?
1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
 
Unapotanguliza "mooring" ya jahazi lako kwa kuandika wale wa JAMBO watoe mawazo na "wapya" wa JF watulize mizuka,una maanisha hao watu wa pande mbili wana akili tofauti na Uraia tofauti?Nimeanza kuamini "uzee ku..anin."!
 
Ulishaonyesha msimamo wako lkn huyohuyo bado unaleta mjadala wa nini tena, au umegundua upepo utabadirika soon.
Msimamo wangu upo wazi, pia ntaka nifahamu na misimamo na sababu za wengine.


Ulewa wako na wangu ni tofauti, au tupo sawa kiuelewa? Unaloweza kuliona wewe jema mimi naweza kuliona baya, na nnaloweza kuliona mimi jema, wewe uanweza kuliona mabaya. Ndiyo maana tnajadili hapa.


Lazima ifike pahala tuwe na "common grounds" zinazozungumzika kwa faida ya Tanzania.

1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
 
  1. Only give out Short leases
  2. Hakuna kumpa mtu exclusivity watu tofauti wanaomba tender za muda mfupi mfupi
  3. Transparency kila kitu kiwe wazi
  4. Percent yoyote atakayopewa mdau yoyote isizidi 49 percent (state bado iwe na say na sio vinginevyo)
  5. Hii ni short-time tujifunze sio lazima tubinafsishe mambo yote tunaweza ku-outsource baadhi ya kazi ambazo ni ngumu na tu-concentrate kwenye rahisi sio kuwaachia the kitchen sink
  6. Tuache tabia ya kusema fulani kafanya na sisi tufanye ifike wakati na sisi tuwe mfano waseme fanyeni kama watanzania
  7. Tujiulize kwanini hatuwezi ili tutibu huo ugonjwa ili kesho tuweze
  8. Tu-plan na sisi sio kufanya ndani tu (tuna bandali nyingi sana) maybe ifike wakati sababu tuna mashamba darasa tuwe wabobezi ili na sisi tuitwe kwenye kuwafanyia wengine (sababu tatizo letu kubwa ni ku-settle for mediocrity)
 
JokaKuu Bams Kalamu Nguruvi3
 
FaizaFoxy afadhali Leo umekuja kwa utaratibu mzuri. Kwa mtazami wangu, hili la Bandari baada ya Serikali kuchakata na kufikia uamuzi wa uendeshaji wa bandari uwe chini ya wageni ingetangaza nia yake ya (intention) kuwapa wawekezaji bandari zake huku ikitoa manufaa ya kufanya hivyo na muda wa uwekezaji huo. Hiyo ingefanya wananchi ktk makundi kutoa maoni, ushauri na mapendekezo yao. Bunge nalo lingepata fursa ya kushauri Serikali.

Lakini Sasa hali ni tofauti, gizani tayari Serikali ilishasaini makubalino ambayo huwezi kuyabadilisha tena. Mwekezaji tayari ana mamlaka makubwa ya kuingia HGA bila kuathiri IGA ambayo ni dira yake. Hapo wananchi watashauiri nini sasa zaidi ya kukataa uwekezaji huo?!

Ilitakiwa illetwe rasimu (draft) IGA ili wananchi wachakate na kushauri. Then inakuja IGA yenye mapendekezo ya wananchi wa Tanganyika.
 
kutoendesha hao Dpw haimaanishi kilichokubaliwa hawakipati. Ni suala la muda tu.
Muhimu vipengere tatanishi viondolewe katika hayo makubaliano/mkataba kificho; ila sipingi uwekezaji wa Dpw
Hilo mbona limeshatolewa ufafanuzi mara nyingi sana.

Mfano kipengele kipi kimoja amabacho majibu yake hayajakuridhisha na unataka kiondolewe. Tuwe "specific".
 
Hilo unalosema mbona siyo jipya kwa banadari ya Dar, ilikuwepo kampuni imesahiliwa Tanzania inatwa TICTS lakini hiyo ni kampuni ya nje.

Na hilo hilo ndilo litafanyika kwa DP World, limejibiwa sana hilo, kuwa wafunguwe kampuni, tena juzi Possy kasema hawa wameambiwa kampuni itayofunguliwa Tanzania na iwekwe pia kwenye soko la hisa ambapo kila Mtanzania atakuwa na fursa ya kununuwa hisa, kitu ambaxho TICTS hawakukifanya kwa miaka 22.

Silioni tatizo hapo kwa kuwa mkataba wa uendeshaji bado haupo.

1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…