Watanzania tujiulize Maswali muhimu ya Kibiashara kuhusu bandari zetu kwa dunia ya leo

Kweli kabisa. Hakuna biashara isiyo na ukomo. Mpaka sasa hatuna mkataba wa kibiashara, au wewe unaufahamu tunao?

1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
Faiza, hivi Ile Sheria ya bunge ambayo waliitumia inahusu bunge kuijadili mikataba na siyo makubaliano. Acha kupotosha wasomaji. Ikikupendeza itafute ujiridhishe.
Bunge linatakiwa kuijadili na kuridhia mikataba na siyo MoU kwa mujibu wa Sheria!
 
kifupi Bandari yetu hatutaki foreigner amiliki haijalishi awe mchina, mwarabu, mzungu au sijui Mnyarwanda, Bandari yetu ni urithi wetu hivyo no foreigners!
 
5. Hii ni short-time tujifunze sio lazima tubinafsishe mambo yote tunaweza ku-outsource baadhi ya kazi ambazo ni ngumu na

Hakuna hata square meter moja ya banadari zetu itayobinafsishwa. Hivi unaibinafsishaje Ardhi? Wakati sheria zetu za Ardhi hata sisi Watanzania hatubinasishwi.

Hilo halipo wala halitakuwepo.
 
Moja kukubali tu maneno ya PM itakuwa ni uwendawazimu kulingana na kwamba we have been here before...; Once bitten twice Shy; fool me once shame on you, fool me twice shame on me (Na hili tutahakikisha vipi kwamba halifanyiki tena ni pale tu kuwa na transparency kwamba kila kinachofanyika kitawekwa wazi) lakini hili haliwezekani kamwe...; litakuja zimwi la siri za mikataba hence kuna uwezekano kwamba hatutajua abadan katani...

Kuhusu kwamba mtu amewekeza sana tungoje mpaka arudishe pesa zake huenda na alichowekeza by the time muda wake unaenda ukingoni kinakuwa kimeanza kuzeeka - Hatukatazwi kuingia mikataba ya kujua ni nini kinatakiwa kuwekezwa hence kuchangia pesa au kukinunua na uwekezaji / ushirikiano ukawa kwenye uendeshaji; usitegemee kama kinachotakiwa ni pesa muwekezaji atatoa pesa zake mwenyewe; hata yeye atakwenda kukopa kwa financiers kama wewe utakavyokwenda kukopa (hio ndio nature of the game)
 
7. Tuache tabia ya kusema fulani kafanya na sisi tufanye ifike wakati na sisi tuwe mfano waseme fanyeni kama watanzania

Ni kweli katika ushindani kibiashara si vizuri kusema sema ni unachotaka kukifanya kwa sababu fulani kafanya hivi.

Nimeklewa.
 
8. Tu-plan na sisi sio kufanya ndani tu (tuna bandali nyingi sana) maybe ifike wakati sababu tuna mashamba darasa tuwe wabobezi ili na sisi tuitwe kwenye kuwafanyia wengine (sababu tatizo letu kubwa ni ku-settle for mediocrity)

Hayo ndiyo tunatakiwa tuyafanye. tymejifunza kwa TICTS sasa tumekuja kivingine, tujifunze kwa DP World ili wakati uyapofika tuje kivingine, au sisi wenyewe au tutakae vunja nae chawa.

Siku zingine weka post moja swali moja. Unatuchosha .
 
Kwa mfano wako wa Toyota nakupa mfano halisi Toyota anakwambia kuanzia leo hakuna kutumia gari lingine bali Toyota au kama wachezaji mpira wanavyoambiwa kwamba wewe brand yako ni Nike hivyo utavaa Nike maisha yako yote (ndio kama huyu Bwana kama ni kweli kwamba amepewa Bandari zote za Maziwa yote...; Vilevile inategemea shida yetu ipo wapi katika uendeshaji apakuaji meli au ni kitu gani; tunaweza kutafuta muwekezaji / msaidizi katika mambo ambayo ni magumu kwetu; Tunaweza kuamua kumpa DP World Tanga; Dar tukawapa watu tofauti tofauti na Bagamayo mchina (kwa mikataba ambayo ni open na transparent) tukawaacha wakashindana na sio kumpa mmoja yote wala yoyote 100 percent (kama unavyojua hapa what is at stake sio economic factors pekee bali na security factors)
 
Katiba ya nchi inaruhusu Bunge kuridhia makubaliano? Agreement
Hilo la katiba watajuwa wabunge, mimi sifahamu. Mimi nnachojuwa makubaliano yalipelekwa bungeni yakaridhiwa.

Swali langu lipo palepale:

1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
 
Nataka kuamini kuwa Faiza ameanzisha uzi huu kwa nia njema ya kutaka tuelimishane kama tulivyokuwa tunafanya miaka mingi iliyopita.
Lakini wewe unataka kumuaribia kwa kuwatuhumu wengine kuwa wamejaa chuki kabla hata hawajatia neno. Faiza kwa kukukalia kimya kunaonyesha anaweza kushindwa kuongoza majadiliano ya haki na uwazi kwa sababu atapendelea tu upande wake.
Hata hivyo ninampa benefit of the doubt kuwa ana nia njema.

Amandla...
 
Nimejiuliza kuhusu DP World kama taratibu za kumpata ilitangazwa tenda kama taratibu zetu zinavyotaka au utaratibu gani ulitumika?
Hatuna mkataba na DP World kwa hiyo swali lako halina maana.

Nijuavyo kuna makubaliano ya nchi nchina nijuavyo nchi na nchi hazina sababu ya kutangaziana kuwa tunataka ushirikiano wa kimaendeleo.

Mfano sisi tuna maonesho ya sabasaba, akija mgeni wa nchi akakuta mambo fullani mazuri anaweza kusema hili la Tanzania litatufaa Zambia ngoja tuingie nao makubaliano, nao, simple..



Na ndicho kilichotikea 2020, kulikuwa na maoimesho ya kibiashara Dubai, Tanzania ikashiriki, mama akahudhuria akayakuta haya ya bandari yakamvutia. Simpo.
 
Hilo la katiba watajuwa wabunge, mimi sifahamu. Mimi nnachojuwa makubaliano yalipelekwa bungeni yakaridhiwa.

Swali langu lipo palepale:

1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
Ninavyojua mimi ni kuwa hawaendeshi kwa sababu bado hawajaingia katika HGA na TPA.

Amandla...
 
Na haya yamo kwenye msahafu gani ? Narudia tena fool me once shame on you, fool me twice shame on me... ; Kwahio sababu mpaka sasa hakuna kitu kama hicho tuendelee na huu upuuzi kumbuka hizi sio mali za watawala na anayesign...., bali ni mali za wananchi kwahio kuendelea kufungwa na kipengele kama hiki tutakuwa tunaongelea haya haya till kingdom come..... Kuna kipindi Utumwa ulikuwa legal na order of the day haimaanishi wangeendelea kufanya hivyo, sababu mpaka wakati huo hakuna sehemu ambapo watumwa hawakuwepo....;

Na unaongelea NDA; hapa sio kwamba kuna siri fulani za utendaji ziawekwa wazi (tunatumia mashine gani teknolojia gani na meneja wetu tunamlipa ngapi au breakfast ni saa ngapi) bali ni kila kitu kuhusu mkataba kinachohusu mali ya mtanzania faida, utumiaji wa pesa mapato n.k. (Ukizingatia hiyo transparency anayeonyeshwa ni mwenye mali ambaye ni mtanzania) kama vile ambavyo shareholder inatakiwa / ana haki ya kujua kampuni ambayo ana stake maendeleo yake kila quarter to the nitty gritty
 
Tunatakiwa kuwauliza viongozi wetu kwanini wameshindwa kuwashughulikia wezi pale bandarini .Tuliwapa kazi ya kuendeleza uchumi wa Taifa, ila wamewaachia wajanja watafune mapato ya bandarini. Kuwapa wageni kuendesha bandari ni kama viongozi kukwepa majukumu yao. Kimsingi mapato halisi ya bandari zetu hayajulikana kwakuwa wajanja wachache wanachepusha mapato. Inatakiwa tuwafunge na kufirisi Mali za wafanyakazi wasio waaminifu kwanza halafu ndio tufikirie kuleta mbia pale bandarini.
 
makubaliano = agreement. kilichasainiwa ni IGA. Kirefu chake nini?

Mkataba = Contract.


Mimi sijaiona contract yoyote kwenye haya masuala, Kama ipo basi aliyenayo aiweke.
 
1. Ni kweli DP World imetumia IGA ili kukwepa ushindani katika kitafuta mwekezaji?

2. Nani alisaini ule mkataba kwa upande wa Dubai? Na nani alishuhudia utiaji saini wa ule mkataba kwa upande wa Dubai...
Weka post moja swali moja.
 
Unaambiwa mwekezaji walimuona tu kwenye maonesho pale Dubai basi wakampenda na wakagawa aendeshe bandari za bahari ya hindi ukanda wa Tanga hadi mtwara, na bandari za ziwa nyasa, tanganyika na victoria, hawa watu ni wapuuzi wa kiwango cha mwisho
Huo ndiyo ukwe;i, hakukutana nae kwa bahati mbya, Tanzania walishiriki hayo maonesho na Mama alitembelea, na kwa protokali kaenda makamo wa Rais ikabidi apokewe na Makamo wa Rais.

Mbona hilo kawaida sana kwenye maonesho makubwa ya kibiashara. Hata sabasaba Tanzania tumeshapoke Marais na viongozi wengi wa duniani.

Unafikiri sababu za nchi kutumia mabilioni kufanya maonesho ya kibiashara ni zipi? Uende wewe ukanunuwe pipi?

Unaona ajabu kitu amabcho kipo dunia nzima. Dah Watanzania mna maajabu sana.

Wewe hujawahi jutenbelea maonesho ya sabasaba au nanenane au mara kwa mara Dar Diamond Jubilee tunatangaziwa leo Syria wana maonesho, leo Turkey wana maonesho siku nyingine KOREA WANA MAONESHO.

Kwa kukujuza tu, stendi yote ya mabasi ya zamani ya Ubungo sasa hivi ni maonesho ya boiashara za Wachina, wanakwambia China imehamia Tanzania. Uanfikiri ni wajinga wale? Rais wako hatotembelea pale, wewe hutotembelea pale, viongozi wa nje hawatotembelea pale?
 
Na haya yamo kwenye msahafu gani ? Narudia tena fool me once shame on you, fool me twice shame on me... ; Kwahio sababu mpaka sasa hakuna kitu kama...
Sijakuelewa ni swali au au ni maelezo kwa muoni wako?

kama ni swali lifupishe, kama ni maelezo basi yaache kama yalivyo tutakusoma.

1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
 
Hilo la katiba watajuwa wabunge, mimi sifahamu. Mimi nnachojuwa makubaliano yalipelekwa bungeni yakaridhiwa.

Swali langu lipo palepale:

1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
Kwahiyo unatetea jambo usilojua asili yake.
Kufikia hapo nadhani siwezi kuendelea na mjadala kwasababu moja, hujui unatetea nini na kwa ground zipi

Proved umethibitisha nilichokueleza? Swali la msingi halina jibu, tunasababu za kuendelea kujadili kama kuna mkataba au bandari zinaendeshwaje!

I am out
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…