Watanzania tujiulize Maswali muhimu ya Kibiashara kuhusu bandari zetu kwa dunia ya leo

Sijazihesabu, wewe zihesabu utuletee jibu.


Wakati unazihesabu, Sasa rudi kwenye mada. Achana na ajuza.

Akili kubwa inajadili maendeleo.
Akili ya kawaida inajadili matukio.
Akili ndogo (mbovu) inajadili watu.
huo mkataba umesainiwa lini?
Unakodishwa kwa muda ghani?
Na inatoa shingap kwa mwaka?
Na vipi hatia ya wafayakazi wa tanzania wasije wakajaa mashehe bandarini
 
DP World ni taasisi inayomilikiwa na Falme ya Dubai, kama vile TPA inavyomilikiwa na Serikali ya Tanzania, na zote zzimetajwa kwenye makubaliano. Kama hukuiona, hii hapa nimeitoa kwenye tafsiri yamakubaliano:

(C) KWA KUZINGATIA matakwa yaliyotolewa katika Mkataba wa Makubaliano kuhusu maeneo ya ushirikiano kati ya TPA na DPW kwa ajili ya kuendeleza na/au kuboresha uendeshaji na usimamizi wa miundombinu ya kimkakati ya Bandari za Bahari na Maziwa Tanzania, kanda maalum za kiuchumi, hifadhi za usafirishaji na ukanda wa kibiashara wa Serikali ya
 
Nilijua unazo akili kumbe nawewe chenga.
 
Kwanza nakusikitikia kwa kutokuelewa. Pili nashukuru kuwa hjapinga kuwa makubaliano yamehadiliwa bungeni.

Kutokuelewa kwa sababu, hakuna mahali katiba ilipokatazza makaubaliano yoyote yawayo kujadiliwa bingeni. Nioneshe ni wapi katiba imekataza makubaliano kutokujadiliwa bungeni.

Mkaubaliano mengi tu yameshajadiliwa kiaaina yake bungeni.

Umeruka weee lakini uzi ni uleule, bado hujajibu swali langu:

1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
 
Unaambiwa mwekezaji walimuona tu kwenye maonesho pale Dubai basi wakampenda na wakagawa aendeshe bandari za bahari ya hindi ukanda wa Tanga hadi mtwara, na bandari za ziwa nyasa, tanganyika na victoria, hawa watu ni wapuuzi wa kiwango cha mwisho
Siyo unaambiwa tu, ndivyo ilivyo imeainishwa hiyo hata kwenye makubaliano yaliyopitishwa bungeni, jsomee kifungu hicho kama ulikuwa hujayasoma makubaliano:

(B) KWA KUZINGATIA Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na DP World (DPW) uliosainiwa katika ziara ya Mh. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Maonesho ya Dubai 2020 (Dubai Expo) tarehe 28 Februari, 2022;
 
We si ulisema mambo ya dp yanaendelea bandarini na inaanza kazi soon mjadala wa nini tena yani we bibi hujitambui
Tena kuna mengi sana kwenye makubaliano, si bandari pekee. Jisomee:

I) KWA KUZINGATIA mikataba mbalimbali ya miradi inayokusudiwa na Nchi Wanachama kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali itakayokubaliwa kupitia Mikataba ya Serikali Mwenyeji (HGAs), mikataba mahususi ya maafikiano au
mikataba mingine ya miradi kati ya Tanzania na kampuni husika za mradi;


Hayo nimekunyofolea na kukuwekea kutoka kwenye makubaliano yaliyotafsiriwa kwa Kiswahili, bofya chini hapo ukita kuyasoma yote yaliyomo kwenye makubaliano:

 

Mikataba ijayo bandarini kutokana na makubaliano yaliopitishwa bungeni ni mingi sana. Jisomee, kama Kingereza kinakupa shida, sema tukutafsirie:

TPA director general Plasduce Mbossa also said there was misinformation being spread by those opposed to the plan.
He was clarifying several issues in connection with debate on social media with regard to the Intergovernmental Agreement (IGA) between Tanzania and the emirate of Dubai on social and economic partnership for the development and improving the performance of sea and lake ports in Tanzania.


The coming negotiations will culminate in actual investment coming into Tanzania.
“We are talking of the Host Government Agreement between the country and the company; Concession Agreement or Lease Agreement for the various issues to be implemented such as information and communication technology, training, port development, port operations. That is when we will sign other contracts. These implementation agreements have not yet been signed. They have neither been negotiated,” Mr Mbossa said.
The HGA and the Concession or Lease Agreements will have specific time frames. “What the IGA says is that the agreement will cease to operate as soon as the HGA or the Concession/Lease Agreement/Project ends. What this means is that actual time for the contract will be known from the HGA or Concession/Lease agreements that will follow.”
According to Mr Mbossa, what the IGA does was to give rights to the two countries and allow the implementation to be conducted swiftly.

Chanzo: TPA: Truth about port agreement with Dubai firm
 
Msingi wa mkataba ni wakipuuzi sana
Tuoneshe huo mkataba wenye "msingi wa kipuuzi sana". uusemao. Maana mkataba wa utendaji sijauona hata mmoja na tunaitegemea iwe mingi sana. Kama mwenzetu unao japo mmoja tuoneshe na sisi tufaidike na hu upuuzi.

Bado lakini hujajibu swali langu:

1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
 
Ngoma ikivuma sana kinachofuata nikupasuka.....
Usijali, washajulikana wote na washajulikana kwanini wanafanya hivyo.


Hawa wa hapa JF twende nao hivyo hivyo huku tunawaelimisha taratibu.
 
Serikali haina makubaliano na DP World. Serikali ina makubaliano na Serikali ya Dubai.

Dp World hivi unavyoongea wanakaa chini siku zote na PTA, hao ndiyo walioainishwa kwenye makubaliano wakae chini na kuiongelea mikataba.

Na mkurugenzi Mkuu wa PTA kaelezea vizuri sana, kinachoendelea. Jisomee: TPA: Truth about port agreement with Dubai firm
 
Kwanza mkataba urekebishwe mengine yanazungumzika. Hilo tu basi.
 
Kwani mkataba siyo makubaliano?

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
Tatizo halipo kwenye makubaliano aua mkataba, hata uwe kwa mdomo tu ukiwa na masgahidi basi unaweza kutafsirika kama makubaliano au mkataba.

Hapatunatofautisha Agreemenyt kuwa ni makubaliano kwa sababu IGA haioneshi vipengele vingi kwa details. Mkataba au Mikataba ya utendaji yaani "Contracts" ndiyo itakuwa imeenda kwa kina, itaonesha kazi hiii, muda wake huu, kipato chake hiki, kaokodushwa hiki, yeye katukodusha hiki, waganyakazi watakuwa hivi au vile.


Natumai umeelewa tofauti?


Kiswahili bado kinakuwa na ni vigumu kutafsiri makubaliano neno kwa neno neno. Ingekuwa kuna wepesi filani ingekuwa wote tunaojadiliana hapa tungekuwa tunaujadiliana kwa Kingereza lkama yalivyo makubaliano.
 
Kwanza mkataba urekebishwe mengine yanazungumzika. Hilo tu basi.
Huo mkataba uusemao, mimi binafsi sijauona, kwa hiyo ukiuzungumzia ni kama unampigia mbuzi guitar. Labda uuwekke hapa tuuone.

Sasa tufuyte mkataba hewa? Chukulia umeshafutwa. Tungoje mpya sasa. Au unasemaje?
 
Bibi ameamua kuturudisha utumwani kwa masultan wa UAE.
Siyo mada iliypo hapa, lakini utumwa lini ulikwisha? Iliyobadilika lugha tu, utumwa uko palepale, tena wa sasa ndiyo mbaya zaidi.

Unaonaje ufunguwe mada ya hilo la utumwa tuje kuujadili. Maana juzi serikali ya Tanzania imesaini mkataba na serikali ya Oman kupeleka watu huko. Unalijuwa hilo?
 
Huo mkataba uusemao, mimi binafsi sijauona, kwa hiyo ukiuzungumzia ni kama unampigia mbuzi guitar. Labda uuwekke hapa tuuone.

Sasa tufuyte mkataba hewa? Chukulia umeshafutwa. Tungoje mpya sasa. Au unasemaje?
Sasa hata hayo unayotaka tuyazungumzie hayana nafasi kwasasa maana hatuyajui mkataba unasemaje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…