Watanzania tujiulize Maswali muhimu ya Kibiashara kuhusu bandari zetu kwa dunia ya leo

Watanzania tujiulize Maswali muhimu ya Kibiashara kuhusu bandari zetu kwa dunia ya leo

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,246
Reaction score
123,145
Leo tuwache jazba, kejeli, matusi na ujinga. Hii kwa pande zote mbili, zinzoona DP World haifai na zinazoona DP World inafaaa tujadiliane kiustaarabu tuone "options " zetu ni zipi, zile zenye faida tuishauri serikali izifate, zile zisizo na faida tuishauri serikali isizifate.

Kama una jibu au majibu sawa, kama hauna majibu bali una swali lako pia, uliza tulijadili. Maswali na majibu yawe mafupi ili mjadala unoge.

Wale wa zamani tujikumbushe mijadala ya Jambo Frums ilivyokuwa inanoga na wale wa sasa wapunguze jazba.

Uongozi wa JF, @moderators tunahitaji muulinde huu uzi kwa uwepo wenu wa karibu, ili mjadala uende vizuri. Au nipeni u moderator wa mjadala huu tu ili niuendeshe inavyopaswa, mkiona siuendeshi kwa haki, mauodoa u miderator wangu.

Tuwe great thinkers ambao hata mtu atakaesoma huu mjadala aseme aaah, hyu ana point, aah huyu hili tumeliona.

Tuwe na maswali mengi ya kujiuliza lakini tujikite kwenye mada. Nalianzisha:

1) Sasa hivi nielewavyo mimi DP World wala Dubai hawaendeshi bandari yetu yoyote, kweli siyo kweli?
 
Waliosaini mkataba wenyewe saahiz wanaona aibu jinsi walivyo saini bogus treat
Lione swali lililoulizwa, unalo jibu au una swali lako tulijadili? Au mawazo yako tuyajadili. Hao wanaoona "haya" achana nao.
 
Kama unataka mjadara uwe mzuri na DPword tuione ya maana,

Utuambie share yetu kama nchi ni ngapi kwa mwezi ama kwa mwaka kwa mjibu wa mkataba?

Utuambie, ni lini mkataba utakoma?

Utuambie, kwa kuwa mkataba unamanufaa makubwa, kwa nini bandari za Zanzibar hazikuingizwa kwenye mkataba huu wenye mafaida kibao?

Utuambie, Ni kwa nini ziwe bandari zote za bara, nchi kavu na majini?

Kwa nini kwa nini kwa nini unashabikia mkataba unaowapa warabu milele yote?

Inasemekana kwamba, kwenye silabas zetu kumeingizwa lugha ya kiarabu, Hii ni kusema tayari tunaanza kuwa chini ya mwarabu au ni kujifunza lugha ambayo itaitawala Tz
 
Huwezi ukajadili jambo na mtu aliyetanguliza chuki,hii issue wengi wanaendeshwa na chuki tu na ubaguzi,

Subiri uone wakakavyokuja na matusi badala ya kujikita kwenye hoja.
Hujui kitu. Kila siku nikikuuliza kama umewahi hata kuusoma ule mkataba wa hovyo wa bandari, unanijibu mimi nilikuwa mpigaji bandarini!.

Nikikuuliza tena, kama mimi ni mpigaji unanifahamu kwanini usiwaite polisi wanikamate, kisha nifunguliwe mashtaka mahakamani, huna jibu!.

Hii inaonesha jinsi mnaotetea ule mkataba wa hovyo, akiwemo FaizaFoxy mlivyoishiwa hoja, mnaruka ruka tu.
 
Sijasoma ila nilipoona bandari basi umeandika upuuzi tu bila shaka!!!
Hiyo kimjadala inaitwa "assumption" au dhana kwaa Kiswahili. Dhana ni mbaya ki namana yoyote ile, jichunge sana kuwa na dhana, ukiwa na dhana kwa muda mrefu itakufunga mawazo yako utakuwa huuoni uhalisia.

Jema unaweza kuliona baya na baya unaweza kuliona jema kwa 'dhana" tu.

Nakushauri isome post ya kwanza vizuri.
 
Chuki iko wapi zaidi ni kwamba huyu ajuza anatumika hivi kuna mtu ambae amempita kwa kufungua thread za kuhusu bandari humu jF?
Chuki ni kama hiyo uliyoiwasilisha hapa,personal attack,kwanini usijikite kwenye mada na ukajadili mada badala ya kumjadili mleta mada?

Kwani mwisho thd ngapi ambazo mtu anaruhusiwa kufungua kuhusu bandari?

Wewe ulitaka mleta mada apitwe na nani kwa kufungua thd za bandari ili wewe uone ndio sawa?

Kwa hiyo ukifungua thd za bandari ndio unatumika? Vipi na wale wanaofungua thd za kupinga nao una amini kua wanatumika? Au unaamini wa upande mmoja tu kua ndio wanatumika?
 
Hujui kitu. Kila siku nikikuuliza kama umewahi hata kuusoma ule mkataba wa hovyo wa bandari unanijibu mimi nilikuwa mpigaji bandarini!.
Wewe kaa pembeni huna akili ya kujadili vitu vikubwa,uwezo wako wakuchanganua mambo ni mdogo sana.
 
Back
Top Bottom